Mr Kactus
JF-Expert Member
- Jan 7, 2021
- 510
- 2,965
Jana katika pita pita zangu mjini nilipita mitaa ya karume kule ilala kwa vile wkt nipo mkoa niliskia soko liliungua basi nikasema kwa vile nipo mjini nakula likizo ngoja nikashangae mji.
Sasa ktk tembea tembea pale sokoni nikaiona pisi kali inachagua chagua blauzi za buku buku. Moyo ukafanya "chwaaaaaaaah!!!" Mamamamaaa aisee mjini kuna watoto wakali mazee. Alikua amepiga vile visketi flani vya mpira mpira hips zimechomoza kama vile zinapambana zitoboe ile sketi pembeni zipotelee kusikojulikana. Juu alipiga top halafu kifuani saa sita zimechomoza dizaini kama hakua amevaa bra. Nikajikuta kama nimeduwaa shetani akanishika mkono akaniambia "blaza blaza usinikemee, hakika mm ni rafiki yako wa kudumu [emoji39]"
Nikaanza kujivuta mdogo mdogo kuelekea alipokua anachagua nguo. Mapigo ya moyo yalikua yanaenda kasi mno mpaka nilikua nayaskia hapa kifuani "tu tu tuuuu!!!" Nikamsogelea
Mimi "hello bestie, habari"
Yeye "safi"
Mimi "samahani kama nakufananisha hivi"
Yeye "sio mimi"
Mimi "okay, nina shida nahitaji kuwasiliana na ww.. sijui naweza kupata namba yako?"
Akaniangalia kuanzia juu mpaka chini kisha akanipa kasimu kake ka smart ka Samsung nichore namba yangu. Nikaandika. Nikajibip. Nikamshukuru. Nikasepa.
Huyoooooo nikaenda kituo cha gerezani kudaka mwendo kasi nirudi kitaa. Nikasema simtafuti kwanza mpaka jioni. Usiku nikamtext kumpanga for the next appointment. Ila akawa ananijibu kimkato mkato tu. Nikampandia hewani akakata akaniambia subiri nipo na kaka ntakupigia. Ikabidi nimpige sound ktk sms, akatiki lkn kwa masharti nisimuumize maana mahusiano yake yaliyopita alitendwa na hatopenda kupata experience kama ile. Nikamtoa hofu!
Leo asubuhi nimeamka nimekuta amenitumia bonge la text "baby sorry jana jioni wkt tunaonana nilikua na ela ktk mkoba mzee alinituma nikazitoe benki za mafundi hapa home, kama laki tano. Leo asubuhi kaja fundi nataka nimpe sizioni, nahisi niliibiwa pale Karume... Nimemuambia baba hanielewi, sijui nifanyeje naomba nisaidie..." Text nyngne akaweka vikopa kopa na vile vi emoji kama anaona aibu vile...
Nimeshindwa nimjibu nini aisee