Nimemuajiri mtu ndani ya mwezi 1 kaanza kuniibia


Nitakutafuta mkuu tufanye kazi
 
Nimefungua biashara mpya na nimetengeneza ajira kwa mtaaalmu mmoja lakini katika mwezi wa kwanza ananiibia kama tuna hisa naye. Tufanyeje wajasiriamali?
Niwashukuru nyote mlionipa mawazo tofauti katika kuboresha na kukabiliana na hii hali.Jambo moja kubwa ni kuwa sisi Watanzania hatuna uwezo wa majadiliano hasa katika ajira.Mtu anakubali na kusaini mkataba lakini hasomi vipengere vya mkataba na kavielewa.Jambo la pili ni kuwa fursa ni nyingi na wenye uwezo wa kuzitumia fursa wapo ila watu waaminifu wa kusimamia ni tatizo.UAMINIFU ni zero kabisa.
Mimi nilijtahidi sana kuitafiti biashara hii kabla ya kuanza na niligundua baadhi ya mianya na nikajaribu kupunguza faida yangu kwa kutumia technolojia ya ghali zaidi.Kwa mfano badal aya kutumia blood slide natumia MRDT kupima malaria.Baala ya kutumia widal test natumia Rapid test ya typhoid na vingine vingi.Hata hivyo ukifanya reconciliation bado unakuta mapungufu makubwa.Vilivyopimwa na vilivyorekodiwa ni tofauti.
Tujadiliane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…