Nimemuona mnyama aina ya Kalungeyeye sijajua ni ishara gani

Nimemuona mnyama aina ya Kalungeyeye sijajua ni ishara gani

ikerege

Member
Joined
Jun 21, 2022
Posts
22
Reaction score
13
Jana majira ya jioni ghafla nikamuona mdudu au mnyama anaitwa kalungeyeye, sikumtarajia maana kwangu hakuna hata kichaka.

Nilimuomba Mungu tu, sijajua kama alikuwa wa heri au lah, kama kuna anayefahamu zaidi ya huyu mnyama na ishara zake anijuze.
 
Janan majira ya jioni ghafla nikamuona mdudu au mnyama anaitwa kalungeyeye, sikumtarajia maana kwangu hakuna hata kichaka, nilimuomba Mungu tu, sijajua kama alikua wa heri au lah,kama kuna anaefahamu zaidi ya hyu mdudu na ishara zake anijuze.
Hao wadudu ni alama ya bahati.
 
Nashukuru kwa majibu ingawa mengine ni kejeli, km hujui kaa kimya tu si lazima uandike.
 
Janan majira ya jioni ghafla nikamuona mdudu au mnyama anaitwa kalungeyeye, sikumtarajia maana kwangu hakuna hata kichaka.

Nilimuomba Mungu tu, sijajua kama alikua wa heri au lah,kama kuna anaefahamu zaidi ya hyu mdudu na ishara zake anijuze.
Hiyo ni mboga mkuu wala usiogope vip hujamkamata?
 
Inasemekana Ni bahati, sasa inaweza kuwa nzuri au mbaya
 
Kuna baadhi ya maeneo wanapatikana sana, maeneo mengine wanaonekana kwa nadra sana, mimi nilikua nabahatika kukutana nao kwa mara moja moja sana nilikua sijui lolote nikawa nawachukulia poa.

Nakumbuka mwaka fulani nikiwa wilaya fulani Arusha alfajiri nimesimamisha bodaboda nawahi stand nikapande bus, wakat tupo njian kigiza cha alfajiri huku boda ikiwa imewasha taa dereva boda na mimi wote tukamuona Kalunguyeye amekatiza mbele yetu.

Yule jamaa akaniambia kaka inaonekana huko unapoenda kuna bahati huyu mnyama ukikutana nae maana yake kuna jambo zuri litakujia.

Kiukweli mimi sinaga hizo imani kwahio nikamuitikia tu ila nikaongeza maarifa kumbe huyu mnyama baadhi ya watu wana imani naye, nikafika stand nikapanda bus maisha yakaendelea kiukweli sikuzingatia chochote.

Baada ya kama miaka 2 nikarudi tena ktk hiyo wilaya, nikafanya mambo yangu nikamaliza siku yakuondoka ikawadia, nilikuwa sina pesa ya kutosha zaidi ya nauli ya Bus ili nirudi mkoa ninaoishi, sikuweza kupanda hata boda inipeleke stand, nikaamka alafjiri nikaanza kutembea haraka kuelekea stand nipande bus, nikiwa njiani gafla nikakutana na Kalunguyeye akakatiza mbele yangu speed nikashituka nikidhan labda mdudu mkali nilivyo muona nikajiambia kumbe ni haka kamnyama.

Nilitembea kama mita 100 nikaokota 30,000 😊😅 I was like whaaat..? Nikamshukuru Mungu nikaendelea kutembea, ila gafla nikakumbuka maneno ya yule jamaa wa bodaboda kwamba huyo mnyama ni bahati... All in all still siamini na sizingatii imani za namna hiyo.

Kuna mwaka nikiwa kijana mdogo nyumban jiji fulani kubwa hapa Tz nyumban mida ya jioni alitua Bundi juu ya paa letu Mmmmh tukawa tunaogopa kwasabab bundi watu wanamsema akitua kwenu basi kuna kifo, fala yule alikaa siku 2 juu ya paa wazaz wakasema nyoko zake kama katumwa ameshindwa kwa Jina la Yesu, hakufa hata kuku mwaka mzima.

From there nikapata confidence yakupuuzia hizi imani za kiafrika


images-1.jpeg
 
Mtuwekee na picha za huyo kalunguyeye
Naendelea kusoma comments
 
Janan majira ya jioni ghafla nikamuona mdudu au mnyama anaitwa kalungeyeye, sikumtarajia maana kwangu hakuna hata kichaka.

Nilimuomba Mungu tu, sijajua kama alikua wa heri au lah,kama kuna anaefahamu zaidi ya hyu mdudu na ishara zake anijuze.
Tegemea kuwa Tajiri sana hivi karibuni.
 
Janan majira ya jioni ghafla nikamuona mdudu au mnyama anaitwa kalungeyeye, sikumtarajia maana kwangu hakuna hata kichaka.

Nilimuomba Mungu tu, sijajua kama alikua wa heri au lah,kama kuna anaefahamu zaidi ya hyu mdudu na ishara zake anijuze.
Hawa mbona wapo wengi tu. Nakumbuka maeneo kama Kilimanjaro, migombani huko kuwaona usiku ni jambo la kawaida kabisa. Ila hawana shida na ni wapole sana. Watu wengi wanasema wana bahati. Yaani kama bundi alivyo na sifa mbaya ya uchuro basi na karunguyeye naye ana sifa nzuri ya bahati.
 
Hawa niliwaona Home dar akiwa na watoto wakeee...!! Sijui wapo bado au walipotelea wapi...
 
Ila huo ndo mwezi niliopata ajiraaa...!!![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sema nimeangalia tarehe nilizopiga pichaa ni baada ya kupata ajiraa ndo nilimuonaa...
Screenshot_20220711-190415_Gallery.jpg
 
kuna baadhi ya maeneo wanapatikana sana, maeneo mengine wanaonekana kwa nadra sana, mimi nilikua nabahatika kukutana nao kwa mara moja moja sana nilikua sijui lolote nikawa nawachukulia poa...
Nakumbuka mwaka fulani nikiwa wilaya fulani Arusha alfajiri nimesimamisha bodaboda nawahi stand nikapande bus, wakat tupo njian kigiza cha alfajiri huku boda ikiwa imewasha taa dereva boda na mimi wote tukamuona Kalunguyeye amekatiza mbele yetu... Yule jamaa akaniambia kaka inaonekana huko unapoenda kuna bahati huyu mnyama ukikutana nae maana yake kuna jambo zuri litakujia... Kiukweli mimi sinaga hizo imani kwahio nikamuitikia tu ila nikaongeza maarifa kumbe huyu mnyama baadhi ya watu wana imani naye, nikafika stand nikapanda bus maisha yakaendelea kiukweli sikuzingatia chochote...
Baada ya kama miaka 2 nikarudi tena ktk hiyo wilaya, nikafanya mambo yangu nikamaliza siku yakuondoka ikawadia, nilikua sina pesa ya kutosha zaidi ya nauli ya Bus ili nirudi mkoa ninaoishi, sikuweza kupanda hata boda inipeleke stand, nikaamka alafjiri nikaanza kutembea haraka kuelekea stand nipande bus, nikiwa njiani gafla nikakutana na Kalunguyeye akakatiza mbele yangu speed nikashituka nikidhan labda mdudu mkali nilivyo muona nikajiambia kumbe ni haka kamnyama... Nilitembea kama mita 100 nikaokota 30,000 😊😅 I was like whaaat..? Nikamshukuru Mungu nikaendelea kutembea, ila gafla nikakumbuka maneno ya yule jamaa wa bodaboda kwamba huyo mnyama ni bahati... All in all still siamini na sizingatii imani za namna hiyo... Kuna mwaka nikiwa kijana mdogo nyumban jiji fulani kubwa hapa Tz nyumban mida ya jioni alitua Bundi juu ya paa letu Mmmmh tukawa tunaogopa kwasabab bundi watu wanamsema akitua kwenu basi kuna kifo, fala yule alikaa siku 2 juu ya paa wazaz wakasema nyoko zake kama katumwa ameshindwa kwa Jina la Yesu, hakufa hata kuku mwaka mzima... From there nikapata confidence yakupuuzia hizi imani za kiafrika
Mkuu Mr Director asante kwa maelezo yako na mimi ngoja nichangie kidogo. Hili la bundi anapokuja nyumbani watu wanaoanisha na kifo lina ukweli fulani. Ngoja nikupe maelezo ila niseme kwanza mimi siamini hizi mila za kipuuzi hata kidogo. Ni hivi: Zamani kulikuwa hakuna hospital. Hii ina maana kuwa watu wengi walikuwa wanaugua na kufia nyumbani. Sasa basi, kwenye kuugua kuna wale ambao pengine walikuwa wanaweza hata kutokewa vidonda au kuugua mahututi kiasi ambacho walikuwa wanatoa harufu. Na walipofariki, hakukuwa na mochwari, hivyo wengi walikuwa wanahifadhiwa nyumbani kusubiri maziko. Pia kuna jamii zilikuwa na utamaduni wa kukaa na miili ya marehemu kwa muda kabla ya kuzika. Tukirudi upande mwingine ni kuwa bundi siku zote wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu za mizoga. Kwa hiyo basi kulipokuwa na mgonjwa mahututi au mtu aliyefariki kwenye jamii fulani, bundi walikuwa wanasogea baada ya kusikia harufu ya ''mzoga'', hivyo jamii ikajenga imani kuwa bundi ndiyo wanaleta uchuro.
 
Ila huo ndo mwezi niliopata ajiraaa...!!![emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sema nimeangalia tarehe nilizopiga pichaa ni baada ya kupata ajiraa ndo nilimuonaa...View attachment 2287375
Nimewahi kumla huyu mnyama nyama yake ni tamu sana. Pia hiyo ngozi yake na miiba hukaangwa na kupatikana unga mweusi ambao ni dawa nzuri sana kwa mtu anaesumbuliwa na matatizo ya kifua km pumu nk.
 
Arusha wapo wengi sana migombani.

Mimi huwa naumia roho sana Nikimkuta ameuawa ama kwa kukanyagwa na gari au kwasababu nyingine yoyote

Ni kiumbe kisicho na shida yeyote, ni kama kinyonga tu.
 
Janan majira ya jioni ghafla nikamuona mdudu au mnyama anaitwa kalungeyeye, sikumtarajia maana kwangu hakuna hata kichaka.

Nilimuomba Mungu tu, sijajua kama alikua wa heri au lah,kama kuna anaefahamu zaidi ya hyu mdudu na ishara zake anijuze.
Yani una hofia mboga kabisa mkuu... sisi kwakikwetu tunaita ...shensee nyama yake tamu sana una kwama wapi tena mafuta yake ni dawa nzuri sana
 
Back
Top Bottom