Holly Star
JF-Expert Member
- Aug 25, 2018
- 4,373
- 8,284
Duh uaan ukimwona mnyama unatafuta ishara. Haya bana
Niliambiwa hivi na baba yangu mdogoHao wadudu ni alama ya bahati.
NIMEKUELEWA VIZURI SANA MKUU, UMENIONGEZEA MAARIFA MAPYA NA MAKUBWAMkuu Mr Director asante kwa maelezo yako na mimi ngoja nichangie kidogo. Hili la bundi anapokuja nyumbani watu wanaoanisha na kifo lina ukweli fulani. Ngoja nikupe maelezo ila niseme kwanza mimi siamini hizi mila za kipuuzi hata kidogo. Ni hivi: Zamani kulikuwa hakuna hospital. Hii ina maana kuwa watu wengi walikuwa wanaugua na kufia nyumbani. Sasa basi, kwenye kuugua kuna wale ambao pengine walikuwa wanaweza hata kutokewa vidonda au kuugua mahututi kiasi ambacho walikuwa wanatoa harufu. Na walipofariki, hakukuwa na mochwari, hivyo wengi walikuwa wanahifadhiwa nyumbani kusubiri maziko. Pia kuna jamii zilikuwa na utamaduni wa kukaa na miili ya marehemu kwa muda kabla ya kuzika. Tukirudi upande mwingine ni kuwa bundi siku zote wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu za mizoga. Kwa hiyo basi kulipokuwa na mgonjwa mahututi au mtu aliyefariki kwenye jamii fulani, bundi walikuwa wanasogea baada ya kusikia harufu ya ''mzoga'', hivyo jamii ikajenga imani kuwa bundi ndiyo wanaleta uchuro.
Hapana ni mnyama mdogo sana na umbo lake halizidi ukubwa huo... Japo ana miba midogo isiyo na madhara kama ya kinyonga...Samahani ndio kaka kuona au??