NIMEMUONA MUNGU MUUMBAJI (ELOHIM) KUPITIA PAKA WANGU

Pridah

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
1,495
Reaction score
3,453
Juzi nikiwa nimejilaza kibarazani ghafla nilimuona paka wangu akifanya kitu ambacho sijawahi kumuona akifanya kabla wala kumuona paka mwingine yeyote akifanya hivyo.Nilishangaa sana nikamchukua ka clip nikiamini paka wangu ana talent ya ajabu na niliamini watu watashangaa sana kuona paka akifanya hivyo.Ningekua mpumbavu ningemuogopa paka wangu nikihisi ni jini.

Hata hivyo,japo sikujua nitatumia neno gani ku google ila nikasema ngoja ni google nione kama kuna sehemu wameongelea hichi kitu alichofanya paka wangu.Baada ya kusearch kwa maneno tofauti tofauti nikaibukia youtube na nilishangaa kuona kumbe hiyo ni moja ya tabia/matendo ya paka na kwamba paka wangu sio wa ajabu wala hana kipaji bali amefanya alichofanya sababu yeye ni paka.

Nilitafakari vile ambavyo ni ajabu kuwa ukiwachukua paka wote wa dunia hii bila kufundishwa wala kuona popote wana vitu vinavyofanana watafanya kwa sababu wao ni paka.Nikawatafakari na wanyama wengine wengi na mwishowe nikaanza kujitafakari mimi.

Wakati najitafakari nikajiuliza hivi kuna mashine inayochakata mambo mengi magumu na kwa ufanisi kama mwili wangu?Nikamkumbuka jirani yangu ambae ana siku ya nne leo kapata stroke na moja ya mkono wake hauwezi chochote lkn wiki mbili zilizopita tulikua nae msibani mimi na yeye tukipika jungu moja la ubwabwa tukisaidiana kukoroga na kuchochea kuni kwa mikono yetu bila shida.
ikajiambia kwa namna huu mwili unafanya kazi NAKATAA NA NINAPINGA VIKALI kuwa tumetokea tu randomly.There is A MAKER.Huu mwili umetengeneza na kitu ambacho kina akili nyingi kupita upeo wetu unqvyoweza kufikiri.Kitu chenye ubunifu mkuu.

Hata hivyo,my MAKER sio yule wa kina Mwampopo na kiboko na wengine jumlisha kobazi..Kamwe sitakua Zombie,sitanunua udongo,sitakanyaga mafuta wala hakuna wa kuna sadaka yangu.

Pia bado naamini kuwa Biblia na Quran ni vitabu vya mchongo vilivyoandikwa na wajanja kwa ajili ya wajinga.

FELIZ Aร‘O NUEVO๐Ÿพ๐Ÿพ๐Ÿ™๐Ÿผ๐Ÿ™๐Ÿผ๐Ÿฅ‚๐Ÿฅƒ๐Ÿฅ๐Ÿธ๐Ÿฝ๐Ÿ’ƒ๐Ÿผ๐Ÿคธ๐Ÿฟโ€โ™‚๏ธ
.
 
Ambavyo sipendi paka ningemtimua ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Mpenzi Pridah natamani na nimesoma habari yako kwa shauku labda useme paka amefanya nini ili na Mimi nijue maajabu ya paka mapya nisiyoyajua maana nawahusudu mno Hawa viumbe .

Lakini pia mwaka unaenda kuisha Sina Raha dada na mpenzi maana ni wiki sita nyuma mbwa wangu walihama kwangu wakahamia kwa jirani na Mara nyingi usiku nikirejea kutoka madhambuni na mbwa wangu wanashiriki na wengine kunibwekea na kunifukuza ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ

Sasa haitoshi Sasa ni wiki ya pili mpenzi paka wangu ,aitwaye Zuu ametoweka nyumbani simuoni ,nimeuliza kwa kila jirani wa karibu Ila hayupo hata mmoja aliyeweza kusema kamuona .

Najiuliza ameuawa ? Je nilifanya kosa gani asilopenda mpaka atoweke ? Je ameenda kwa majike atarejea hakika inaniuma naumaliza mwaka na machungu ya hawa ndugu ,rafiki na wanangu sijui mwaka mpya nitaishije bila wao .
 
Kwakuwa hautupii ka clip nimeamua kugoogle. "Alivyofanya paka wa Pridah" naona imenipeleka YouTube. Nimeiona aisee kweli ni amaizing
Usha sub scribe lkn !!๐Ÿ˜ฌ
 
Sasa mkuu huyo Mungu wako unamuona yuko sawa? Ana upendo?
Yaani ameruhusu jirani yako apate stroke?
Sasa hapo upendo wa Mungu uko wapi?
 
Pridah Again
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ