Nimemuona Sabaya mahakamani leo, hakika anastahili huruma

bwaiseekwetu

Senior Member
Joined
May 29, 2022
Posts
144
Reaction score
431
Wandugu,

Leo nilipita kwenye Viwanja vya Mahakama ya hapa Moshi kwa ajili ya kufuatilia suala langu fulani.Bahati nikiwa pale karandinga kutoka Magereza likiwa na watuhumiwa mbalimbali akiwemo Jenerali Sabaya likawa limefika na nikamuona Live Sabaya.

Ni kwamba ana Bandeji kichwani (nadhani alifanyiwa Operation ule uvimbe wake) na hali yake kiafya inaonekana kabisa sio nzuri. Huyu dogo naamini amejifunza sana kwa kweli, asamehewe tu lakini wale wote waliodhulumiwa kwa namna yoyote walipwe tu fidia.
 
Daah hadi huruma.
 
Na bado, damu alizomwaga ni nyingi hastahili huruma hata chembe

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
 
Ye si alikuwa anaona sifa kuonea watu. Awaombe kwanza msamaha aliowaonea , wakikubali ndio afikiriwe.
 
Unamwonea huruma jambazi? Na alowaua je?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…