Nimemuonea huruma mume wangu baada ya kukagua simu yake

Nimemuonea huruma mume wangu baada ya kukagua simu yake

Status
Not open for further replies.

Kalpana

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2017
Posts
32,603
Reaction score
62,269
Katika kagua kagua simu nimekutana na msg ya mchepuko anakumbushia ile biashara aliyoambiwa aaangalie kama itafaa afunguliwe biashara tayari mbona kama mume amenyamaza? Jibu la mume ni kwamba "Tutaongea mama".

Nilipata ka mshtuko na ka hasira kidogo lakini baadae nikaingiwa na huruma sana nikimuangalia mume wangu.

He is so good kwetu mimi na watoto yaani hakuna kitu tuombe asitimize. Ila huruma imenijia kwa sbb ana majukumu mazito mbele yake kwa sasa na huyu mchepuko hajui anawaza hela ya biashara.

Na kuhusu kumwambia nimepanga nimwambie yeye aendelee na mambo yake hela ni zake bwana ila chonde chonde asiniletee magonjwa as kwangu mimi nimetulia na najiamini kwa asilimia 100.

Na kupambana eti na mchepuko sijui kupambana na mume siwezi kisasi ni cha Mungu. Halafu kwa nature ya wanaume walivyo ntagombana na wangapi. Au mnasemaje wadau?

Mie ninamuonea sana huruma maskini unakuta anawaza familia kumbe kuna ka mchepuko kanampa stress tena naogopa kasije kakamroga akatusahau, Nifanyeje?
 
Katika kagua kagua simu nimekutana na msg ya mchepuko anakumbushia ile biashara aliyoambiwa aaangalie kama itafaa afunguliwe biashara tayari mbona kama mume amenyamaza? jibu la mume
Sasa na wewe unaonaje ukafanya kama unaniuhurumia na mimi ukani-PM ili iwe kama kwenye kubeti vile "both team score"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom