kunguru ana wenyewe, humuwezi asilani
atakutia kiwewe, kuzidi umasikini
ulimtega mwenyewe, sielewi ni kwanini
una matatizo wewe, kutojuwa vya thamani?
limtegea mizoga, hilo pia ni tatizo
nyamu tamu ametega, jamaa kaja anazo
wajua kunguru mwoga, ila bingwa wa mizozo
amevunja lako bega, mwishowe mepata wazo
Navyojua ni muwoga,na sumu hutotumia,
Mitego kutokutega, akili hutotumia,
sikuhitaji mshenga,wala sikudhamilia,
sina matatizo mimi, navijua vya thamani,
acha liende zake, likutane na waovu,
nililipa vitu mwake, likaona mi mchovu,
halina hata yake, heshima japo chovu,
hata wazo sina, ni kiuno sio bega,,
acha niende kwa bibi, nikalione chabivu,
nitaliita habibi, likijibu kwa maivu,
nitalipa hanibi, lipokee bila wivu,
Acha walile huko,mtungo litajiju,
uvuvuzela naacha, narudi kitaani,
wengi kunakokucha, kunguru wako vitani,
marefu yake makukucha,hata huko utosini,
Mtego wako ukinasa, kama kunguru achia