Nimemwachia Kunguru, wenye mitego naseni...

Magulumangu

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
3,051
Reaction score
461
Nilimnasa kwa tundu bovu, nilitegesha misosi, mazagazaga kibao, nalo likanasika, likafugika ingawa kwa tabu na maumivu mingi kwangu, Kunguru kila mwanya likipata ujue hutoroka hadi usuke mtego kulikamata, Sasa Natangaza rasmi, NIMELIAHIA KUNGURU mwenye mtego alinase.....
 
Deuces Lyrics

All that bullshit's for the birds
You aint nothin but a vulture
Always hopin for the worst
Waiting for me to **** up
You'll regret the day when I find another girl, yeah
Who knows just what I need, she knows just what I mean
When I tell her keep it drama free
Ohohohohohohohoh… x2(Chuckin up them(deuces)
I told you that im leaving (deuces)
I know you mad but so what?
I wish you best of luck
And now im finna throw them deuces up............
 
Deuces Lyrics

All that bullshit's for the birds
You aint nothin but a vulture
Always hopin for the worst
Waiting for me to **** up
You’ll regret the day when I find another girl, yeah
Who knows just what I need, she knows just what I mean
When I tell her keep it drama free
Ohohohohohohohoh… x2(Chuckin up them(deuces)
I told you that im leaving (deuces)
I know you mad but so what?
I wish you best of luck
And now im finna throw them deuces up............

Kunguru halitaka watunga Verse mkuu, linataka wazee wa EPA maana minyama kwao litapata....Limepaa Kunguru kwenda Unguja kwa mashehe
 
Nilimnasa kwa tundu bovu, nilitegesha misosi, mazagazaga kibao, nalo likanasika, likafugika ingawa kwa tabu na maumivu mingi kwangu, Kunguru kila mwanya likipata ujue hutoroka hadi usuke mtego kulikamata, Sasa Natangaza rasmi, NIMELIAHIA KUNGURU mwenye mtego alinase.....
Magulumangu.....ninachoweza kusema ni kuwa wewe si mfugaji mzuri umekurupukia mifugo usoiweza........wangapi tumewaona wamechukua mikunguru tena ile ya zanzibar na wameibadilisha ikawa njiwa kama wale waofugwa enzi za wana Israel wakati njiwa wakiitwa Hua.
pole
 
hehehehehe mkuu duh yaweza kuwa mie na mifugo basi, ila huyu Kunguru mwache aende zake, dege lisilofugika hili jamani
 
Nilimnasa kwa tundu bovu, nilitegesha misosi, mazagazaga kibao, nalo likanasika, likafugika ingawa kwa tabu na maumivu mingi kwangu, Kunguru kila mwanya likipata ujue hutoroka hadi usuke mtego kulikamata, Sasa Natangaza rasmi, NIMELIAHIA KUNGURU mwenye mtego alinase.....

Kabla hujamwacha alikua kasuku?
Haya mambo mengine jamani... Kwani huwezi kusema umemwacha Kasuku?
 
Kasuku mhhh naye lakini kiama chake kwa majirani, kila linalotokea mtaani yeye, lifanyikalo mjini analijua...ila huyu Kunguru kakaaaa usiombwe kumfuga utakoma...
 
Nilimnasa kwa tundu bovu, nilitegesha misosi, mazagazaga kibao, nalo likanasika, likafugika ingawa kwa tabu na maumivu mingi kwangu, Kunguru kila mwanya likipata ujue hutoroka hadi usuke mtego kulikamata, Sasa Natangaza rasmi, NIMELIAHIA KUNGURU mwenye mtego alinase.....

kunguru ana wenyewe, humuwezi asilani
atakutia kiwewe, kuzidi umasikini
ulimtega mwenyewe, sielewi ni kwanini
una matatizo wewe, kutojuwa vya thamani?

limtegea mizoga, hilo pia ni tatizo
nyamu tamu ametega, jamaa kaja anazo
wajua kunguru mwoga, ila bingwa wa mizozo
amevunja lako bega, mwishowe mepata wazo

sio tu wa zanziba, kunguru tabia yao
hata wale wa Bukoba, na huruma hawanayo
na hupiga hadi roba, kupata chako niyao
kunguru hawana baba, kubali hawana kwao
 
kunguru ana wenyewe, humuwezi asilani
atakutia kiwewe, kuzidi umasikini
ulimtega mwenyewe, sielewi ni kwanini
una matatizo wewe, kutojuwa vya thamani?

limtegea mizoga, hilo pia ni tatizo
nyamu tamu ametega, jamaa kaja anazo
wajua kunguru mwoga, ila bingwa wa mizozo
amevunja lako bega, mwishowe mepata wazo

Navyojua ni muwoga,na sumu hutotumia,
Mitego kutokutega, akili hutotumia,
sikuhitaji mshenga,wala sikudhamilia,
sina matatizo mimi, navijua vya thamani,

acha liende zake, likutane na waovu,
nililipa vitu mwake, likaona mi mchovu,
halina hata yake, heshima japo chovu,
hata wazo sina, ni kiuno sio bega,,

acha niende kwa bibi, nikalione chabivu,
nitaliita habibi, likijibu kwa maivu,
nitalipa hanibi, lipokee bila wivu,
Acha walile huko,mtungo litajiju,

uvuvuzela naacha, narudi kitaani,
wengi kunakokucha, kunguru wako vitani,
marefu yake makukucha,hata huko utosini,
Mtego wako ukinasa, kama kunguru achia
 
Back
Top Bottom