Nimemwachia mali zote, naanza upya

Pole Sana kwa kweli. Pambana utoke kwenye hiyo Hali, usiruhusu ikuharibie mambo Yako.
 
Liverpool VPN njoo huku utoe ushauri

Huu uzi bila mchango wa Liverpool VPN ni batili

Ndugu zangu Offisho_Kid na Uchira 1 ukimsoma huyu mwamba inaonyesha yupo kwenye "Maumivu makubwa ya roho na moyo"

Unaweza kumuona kwa nje yupo ""smart na vizuri and so on"" ila kiuhalisia mwamba anateketea rohoni.

Siku hizi Kuna ma feminist wengi sanaa wanaojiona wameelimika na wanaweza ku control wanaume.
Ole wako ukutane nao Hawa...!!!!!

In the second side, Ukiwauliza Espy Atoto Noelia et al., (2020) Wana msemo wao ""Ndoa ni kwa wanaume wenye akili"" ila sijui kama wanao olewa nao wanatakiwa kuwa na akili..!!

Hapohapo uki "cite" hizo post mbili hapo juu za mwamba, utaona kuwa huyu jamaa alijitoa kwa moyo na pesa ili mke wake aridhike ila badala yake kawa mwiba.

Huyu ndio wale walioambiwa "mwenye kuoa ndio ana akili" basi na yeye akajifanya ana akili na kuoa ila LEO YAMEMKUTA.

Ndugu yangu Mtoto wa nzi Mimi ni mtumishi mwenzako mwenye miaka 32 na miaka 10 Utumishini.

Inaweza kuwa umenipita miaka (umri) na muda wa Ajira au "the vice versa".

Ndugu, katika jambo ambalo nasisitiza na naendelea kusisitiza kwa watumishi wenzangu ni kwamba USIOE USIOE USIOE.

Una mshahara na muda, basi tafuta biashara au uwekezaji "and go for it".
Tafuta hela uishi maisha yako.
Pesa itakupeleka kokote utakako, hata huko kwa Mungu ukitaka kwenda ni rahisi kwenda kama una pesa. Si utakua unatoa sadaka na zaka na kusaidia wahitaji?

Sasa mnaoa ili mtafute nini? MTAKUFAAA.
Mambo ya kuweka mtoto wa watu ndani ili aje kukuumiza na kukutoa roho "Ya nini yote?"

Wanawake wa siku hizi wamefundishwa haki sawa.
Na hili wameli-apply kwenye kila kitu.

Ukitaka kufa mapema dunia ya sasa WE OA.

Ma-feminist WATAWAUAAAA.

Nimemaliza.

Mwenye sikio na asikie.

#YNWA
 
Dharau zilianzia hapo kwenye kumsomesha na kumfungulia biashara
 
Mtoto wa nzi mm ni rafiki yko sana kwenye jukwaa letu la Vita vya urusi na ukraine
ila tatizo lipo kwenye dini yenu kuruhusu mke mmoja kiukweli Mwanamke mmoja ni Mama mzazi tu
Uislamu haukukosea ulivosema tuoe wa4 mna Muumba anawajua hao viumbe
All in All tafuta usahihi katika hizi dini mbili
 
Kwamba kutooa mwanamke ndo utakuwa umekwepa hizo changamoto?

Muoane nyie kwa nyie ndo hamtapata changamoto za ndoa
 
Mkuu usilianini kamwe chozi la Mwanamke ...alicho kifanya sio kwamba hakijui . Hivyo vikao vyote ni yale maumivu ya kuachwa yanamtesa kwa sababu wewe umeanza kumuacha. Na ninacho kushauri kanyagia hapo hapo .

Endapo ukatudiana nae yeye ndio atakuacha Sasa huku na Mali zote umempa utalia kilii Cha mbwa mwitu
 
Why umuachie malii???? Huyo ni wa kufukuzaa akajifunzeee namna ya kuishi na mwanaumeee... ingekuwa nyumba ya kupanga sawaaa ila sio nyumba ya kujenga umzirie mwanamke..
 
Mzee hiyo hatua uliyochukua ni ya kijasiri sana na itakusaidia wewe.

Kwamba ndoa haina hata mwaka na mmeanza kunyimana mbususu ujue mke siyo wako. Lazima uchomoke.

Tatizo ni kwamba siku utakapowasikiliza ndugu na kuamua kurudi ndo utakuwa umeingia kingi. Utateseka sana. Bora uondoke mapema.

2020 nilimsaidia mshkaji wangu mmoja alinunua nyumba na mwanamke wake (siyo mke halali) ila tifu lilianza baada ya kuhamia kwenye ile nyumba. 5 bedroom apartment iliyogharimu around 400,000 €.

Mpaka leo jamaa anaishi kwenye apartment amepanga huku anaendelea kulipa mkopo wa ile walionunua pamoja maana ametambua hana mshirika kwa yule mwanamke mzungu.

Mwanaume ni maamuzi! Tena maamuzi yawe magumu na ya kuumiza kwa wakati huo ila ni dawa.
 
Acha ujinga...kachukue mali zako umuache na zake...usimsusie mali ulizohangaika nazo..achaba na moyo tumia akili...
 
Nenda mahakamani vunja ndoa.

Hii post ni ya 2022 na unasema ndoa ina mwaka ila mmeoana 2016? How? Mna watoto?

Kwanza huyo mwanamke hana akili umeoa failure ukailazimisha kusoma ili akufae ila mwisho wa siku anakugharimu.

Piga mali pasu then sepa kihalali.
 
Kunywa maji

Shusha hasira

Kaa na mkeo mzungumze

Akwambie yanayomkwaza na wewe useme yanayokukwaza

Ndoa ni wawili

Kwa njni muache issue zenu zisambae kwa ndugu wachungaji na jamaa

Kuna sababu akawa anakunyima kuwavtayari kumsikiliza

Umpe nawewe za kwako

Muamue kwa pamoja kuyajenga

Ndoa sio lele mama ndugu. Na hasa kama mna watoto.

Kuna kipindi unaweza kumuangalia mwenzio ukawaza hii ng'ombe umeitoa wapi!!!
 
Unamuachiaje mwanamke kila kitu...? Hapo umempa uhuru wakufanya anacho jisikia unachotakia ni kumrudisha kwao atulue kidogo
 
Aiseh pole
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…