Nimemwambia jamaa yangu hili suala akae alitafakari. Hajaelewa. Hajiulizi kwa nini Iwe hivi kwa Wakwe na Mashemeji zake.

Nimemwambia jamaa yangu hili suala akae alitafakari. Hajaelewa. Hajiulizi kwa nini Iwe hivi kwa Wakwe na Mashemeji zake.

.
 

Attachments

  • Right1.jpeg
    Right1.jpeg
    11.6 KB · Views: 5
Yaani kajitambulisha week mbili ago. Wakwe zake watarajiwa wanamsumbua kuwa atamwoa mtoto wao lini? Hazipiti siku mbili wanampigia au kumtumia msg kuwa asimsahau mwenzie pale kwao.

Mashemeji zake nao wanamwambia shem mchukue dada yetu muanze furahia maisha. Yaani huyu mchumba kifupi pale kwao wamemchoka sana.

Wanamwambia jamaa yangu asiwaze sana mambo ya sherehe watamsaidia sana na pia afanye ya kawaida tu. Kikubwa ni kufunga ndoa. Nliona siku ya kutoa Mahari walikuwa kama wanatamani jamaa aondoke kabisa na binti.

Kwanza hawakuamini kama jamaa anatoa mahari. Na walimpangia mahari ndogo sana kwa kweli...ndogo sana. Jamaa mpaka akashtuka na wakamwambia wao mahari si issue sana kama hajajipanga apeleke hata mbuzi mmoja na mkungu wa ndizi wachome nyama na ndizi. Nyingine atamalizia akipata.

Yaani ni kama huyu bint wamemchoka pale kwao... Sasa nawaza jamaa atawezana naye kweli kuishi naye milele? Maana si hata wakifanikiwa kwenda Mbingu bado atakuwa mkewe? Na wakienda jehanamu bado nako jamaa atakuwa anendelea kukamua?

Nimemcheki kwa kukaza macho...demu anaonekana mwingi sana....macho yake makavu na yanazunguka zunguka muda wote. Nikasema tu....hiiiiii.

Ila jamaa ndo kapenda kweli...hata pamoja na kuwa demu mwenyewe ni alasiri...jua limeshaanza poteza nuru...najiuliza miaka hii yote wenzie hawajataka kuoa....yeye ndo anataka kuoa demu mwenyewe nyakati zinaenda jioni....

Nimemwambia tu atafakari.isije ikawa wanataka kumwangushia jumba bovu. We ukiona unaoa ndugu wazazi hawalii kwa kumpoteza mwana wao...anza jiuliza. Pengine ndo umeenda kuokoa jahazi. Kuna mtu anakaa kwao mpaka wanasema "we huolewi tu uondoke? Tumechoka kwa kweli"

Halafu unatokea Niga unataka weka ndani....unataka kukalia misumali....sisi wanaume tuna mabalaa si kidogo.unaoa binti nusu zimwi nusu mtu.

Yaani mabinti kama hao wanaweza wakakupa hadi mahari ukalipe kwao....au wazazi wakakupa zawadi ya pesa kumbe ndo wanakupa pesa za harusi. Uoe msheherekee uwaondolee mzigo....

Anyway...NIMEKAA [emoji117][emoji117][emoji117] PALEEE NAKUNYWA JUICE YA NAZI NA MIWA.
Muache tu akahangaike na mzigo wake,.....
 
unataka kukalia misumali....sisi wanaume tuna mabalaa si kidogo.unaoa binti nusu zimwi nusu mtu.

Yaani mabinti kama hao wanaweza wakakupa hadi mahari ukalipe kwao....au wazazi wakakupa zawadi ya pesa kumbe ndo wanakupa pesa za harusi. Uoe msheherekee uwaondolee mzigo...
😂😂😂 Nimecheka kifala eti nusu mtu nusu zimwe 🤣
 
Ndoa siku hizi watu huwa wanaleta mambo ya ajabu sana. Ndoa ni swala la watu wawili wakihusisha familia zao.

Sio swala la kucomplicate na kuleta mambo mengi wakati resources haziruhusu.
 
usipende kuwa mshauri kwenye maswala ya mapenzi na vitu vinavyoendana na hisia za upendo utakuja umbuka vibaya sana sio kila unachoona kipo kama ulivyotafsiri kwenye ubongo wako kua pevuka komaa akili[emoji41]
 
Jamaa comedian sana ww nimecheka kifala sana
 
Wewe ni Mnafiki, M'mbeya na Mfitini....!!!
Wewe na wale Wachawi wanaologa Usiku ni sawa sawa...!

Una roho mbaya na Ulojawa na Wivu, Husda ikiwa ndani yako kwa kificho....!
 
Back
Top Bottom