Nimemzaba kofi 'wife' sababu ya Prof.Lipumba. Kamaindi, karudi kwao Kinyerezi

Nimemzaba kofi 'wife' sababu ya Prof.Lipumba. Kamaindi, karudi kwao Kinyerezi

Anarudi kwao kufanyeje mkuu na je akikosana na huko kwao Hata kabla ya kuolewa alikuwa ana solve vipi tatizo kama hilo?? Hapa ndipo ndugu zetu huwa hawajui maana ya ndoa na lile ñeno wanalokuwa wakiimba kuwa Leo/ kesho ni send off yangu.hapa wabongo na tusio wajuzi wa neno OFF kiuhalisia.mke umemuoa na amefanyiwa SEND OFF kweli anarudi kwao kisa ya kufinywa. Send off mana yake ni kuwa ametolewa kwao mazima hana habari napo tena Hata àkikosana nawewe anatakiwa atafute namna ya kutatua mgogoro huo kama amekomaa na àmekuwa MTU mzima na sio miaka mingi hapa wapo watakaonielewa. MTU mzima lazima ujue kukwaruzana kupo Hata baina ya wanandugu. Baina ya wewe na mama/baba/kaka/dada . swali je ukikorofishanà na hao utaenda wapi au utàkimbia kwenu.pia marriage ni lazima I we chemical bond tena electro valent bond na hapa wachache watatnielewa. Hapa ndipo nàpompendea mwanamke wa kimasai/kimasai mana akishaolewa Hata umfànyie nini kwao harudi ng'o.yaani ukikosana na mwanamke wa hizi kabila ambapo anajua kuwa umekasirika kabisa waweza muumiza utàmkuta kaenda kwa shemeji/wifi kama sio wazazi wako hapa lazima ataenda kwa ndugu wa Mme na kuishi huko na kumwambia kuwa ndugu yenu kanifanyia ubaya/kosa Fulani ila sio tena kurudi kwao alikozaliwa. Ni kwa nini arudi na huku alifanyiwa send off au ni kwa vile tunatumia maneno ya English bila ya kuelewa manaye. Hapa utamkuta mama wa kiswahili àkisema huyu ndo my first born wangu wa kwanza kuzaliwa. Hajui bila anarukia tu hilo neno.kama mmeshindana na mkeo hapa bora anatafuta makazi mengine anaenda kuishi ila kwao harudi Hata ufanyeje.kwa walio karibu au wameishi na hayo makabila mawili mtakuwa mashahidi wàzuri wa Hata nayosema. Viva Kurya&Masai societies

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe huyu ni mkeo anatadizia ile mbaya, coner bar ebu njoo maramoja, mbona hana hata shida, wewe mpigie umwambie malim sefu amekupigia simu kwajiri ya kutoa ushahidi kisutu jumainne, na tayari amekutumia check ya ten million, so unaitaji kampani ya kwenda kuzitoa hizo hela,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimecheka sana hasa hapo alipo kwambia uko cuf tena ya lipumba hahahahahahahha!

nilikuwa na kombati flani ya bluu, kuna dada kila akiniona ananiita wewe mfuasi wa cuf (anadai cdm hawavai bluu labda cuf) ananisalimia fresh baadhi ya watu wakawa wanajua kweli mi cuf. umenikumbusha mbali
 
Tulio na miaka miaka mingi kwenye ndoa tunajua hapo hamna kosa...
Kama kunakosa angeanza kukushitaki na kusema kilicho tokea kinaga ubaga
Lakini kinyume chake atakuwa amesema kanipiga tu sujui kosa langu..
Sasa wewe nenda sema kilichotokea uone kama wakwe watapenda wewe kufananishwa na jini mkata kamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yupo hapa BL ananihadithia..inavyoonekana nitaondoka nae kwenda kupumzika
 
Sasa kofi moja tu ametoka Hapo Kwako Kibiti mpaka Kinyerezi?? Ungeamua kushika mashine si ndio angefika bagamoyo kama harmonize?
 
Wanajamvi,

Ivi wenzangu hamnaga matani kwenye mahusiano yenu huko?? Iko hivi....

Nipo na wife tumekaa kitandani, wife anakunja nguo mie nachezea simu iko kwenye chaji huku nimejilaza. Hapa na pale wife kaniambia kiutaniutani tu eti "..afu we unaonekana upo CUF ...tena CUF ya Lipumba. Mie kwa ghadhabu nikanyanyuka nikamzaba kofi moja mpaka akaangukia kitandani, mie nilizan ni masikhara tu kajiangusha. Nikarud kitandan nikaendelea kuchezea sim, nikamwambia "Lipumba hana CUF... kuna CCM na CCM ya Lipumba"

Wife akaamka, katoka nje kapiga yowe moja. Inavoonekana, lile kofi kachukulia serious ameondoka amekimbilia kwao Kinyerezi. Kama nusu saa sasa naona simu ya Mamaake Mdogo inanipigia. Sijapokea. Bila shaka wife kaishafika kwao...

Hapa majirani wawili wamekuja home wanauliza kunani yowe hilo; nimewambia pako shwari tu, labda waliskia vibaya.Sasa najiuliza; kama kwel kachukulia serious hadi ameenda kushtaki kwao, hii kesi mbona ni ngumu sana. Ivi kweli inawezekana kumwelezea mtu mzima mwenye akili timamu huu wehu wa prof kua ndo chanzo cha ugomvi? Nikiwaeleza wakwe haya mambo ya Lipumba afu eti nikamzaba kikofi binti yao, wataniona niko timamu kweli? Au nifanyeje jaman; asalaaaleh?
jiandae kuitwa na msajili wa vyama
 
Huu upumbavu wenu wa siasa kuingiza ktk mambo ya msingi matokeo yake ndo hayo......ndoa ni kitu kikubwa sana haiwezekani siasa isababishe ndoa kuvunjika ni upumbavu kiwango cha lami

Naomba upigwe faini takatifu tena ulipe kwa dolla mwehu ww unampigaje mkeo kisa sijui ccm cuf chadema sijui ujinga gani........hayo mavyama yenu hayana tija kwa mungu ndoa ni kitu cha kueshimika duniani na mbiguni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom