Nimemzidi umri kwa miaka 12

Nimemzidi umri kwa miaka 12

Mkuu..mm mwenyewe nilikuwa najiuliza kama 44yrs kwa mwanamke anaweza kuzaa bila matatizo..ulaya sawa but huku Africa.!.kuwa makini..na nadhani ungeenda kwa daktari akakucheki akupe na advise kabisaa..I hope sasa huna jinsi umefikia the point of no return..doctor akisema upo ok wewe zaa..sidhani kama utashindwa kumlea mtt hata kama ataingia mitini!
Daktari alishaniambia sina matatizo long time ago, ila sikuwa na wakunipa mbegu. Asante kwa ushauri.
 
Usithubutu kuzaa
, huu ushauri wa bure tu nakupa!
Kwani wangapi wamezaa na wameachwa?.

Km kweli yupo serious na ni mpango wa Mungu itakua tu dada yangu!!...

Huyo Dada ako nae ataingiliaje mapenzi ,hajui ni makubaliano ya watu 2!
.sorry,huyo Dada ako kaolewa?

Huyo kaka anasema kwao wataleta zengwe,kwahiyo ataenda kuwatangazia ndugu zake kuwa umemzidi?..
If so,hayupo tayari kukudefend huko kwao!?

Dada Yangu muombe Mungu,ukipata amani moyoni jua ndie ,na km ndie hakutakuwa na chochote kitakachozuia,means kila mmoja wenu atakua tayari kudefen penzi lenu!!

Nb:naona anataka kujua km unaweza kuzaa.
Mtazamo wangu tu!!!

Hivi miaka 44 wanazaa bila shida?

nafikiri ana wasiwasi akikuoa atapata watoto?
ndo maana anataka mzae kwanza

na wewe ukuendelea kusubiri utazaa na mika 50?

nafikiri huna choice...zaa nae hata asipokuoa angalau utakua na mtoto

tena zaa nae watoto wawili kwa haraka haraka halafu muache mwenyewe aamue kukuoa au kutokuoa.....

hapo sasa kila mtu ana point nzuri mnampa kazi mtoa mada
 
Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika taasisi ya serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja. Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulishabadishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula. Semina iliisha Ijumaa na tuligwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.

Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi ninamiaka mingapi? Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alistuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka. Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je ninamtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye anamiaka 31, anakazi nzuri sana.

Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwasababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake. Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza anamiaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu!! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao. Ushauri jamani.

At this age, u a desperate, even Aki n Popo u don't care!
 
Inaonekana umeshafanya kosa la kwanza kumpa tunda mpaka saa nane? Kuzaa itakuwa kosa kubwa utajutaaaa

Ndoa na iheshimiwe na watu wote
 
shukrani mkuu!....hili lidemu kumbe lijinga sana!....
 
Tokea nijue hii thread yako umetunga si kweli nimekua disappointed sana!!!....ila nilikua najiuliza kweli mwanamke amngojee mwanaume hadi astuke amefika 44?????Hata aliyeishia darasa la pili hawezi sema anamsubiri mtu hadi anafika age ya 44.

P'se usirudie uongo, aaaaaaaaaaaaaaggggggggggggghhhr nilikomaa kushauri kwenye uongo dah
 
Asante kwa ushauri wako, nilichoandika ni maisha yangu halisi siyo hadith ya kutunga.
 
Umri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika taasisi ya serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja. Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulishabadishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula. Semina iliisha Ijumaa na tuligwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.

Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi ninamiaka mingapi? Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alistuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka. Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je ninamtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye anamiaka 31, anakazi nzuri sana.

Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwasababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake. Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza anamiaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu!! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao. Ushauri jamani.

Achana na mtoto wa watu ndugu! Muache atafute watoto wenzake. Kwanza atakutesa huko mbele nina hakika ukizaa mtoto mmoja basi kwisha habari. Utaanza kujishtukia uzee utamkwaza na wivu atakua hata kazini tabu. So tafuta amani yako muache kijana wa watu aishi maisha yake. Mueleze ataelewa asipoelewa leo time itamuelekeza
 
Back
Top Bottom