Nimemzidi umri kwa miaka 12

Nimemzidi umri kwa miaka 12

Mnaweza kuoana kwasasa, ila kubali tu kesho kutwa utakapokua fifty yrs utaletewa dogo dogo ama kukimbiwa na kuambiwa kua wewe mzee na kusema alikosea kukuoa. Blive me kwa sasa kakutamani sana kwa umri uo simply bcoz hamjaishi pamoja kama husband and wife. Ukimpa amege tu na mkikaa kidogo ataanza iyo sababu ya umri,na tofauti ya umri wenu itakua silaha yake kukuadhibu.
Ushauri : Tafuta age mate wako aliyekwisha tumia ujana wake na kutulia, ambaye kwasasa hana mke, 42-50yrs uko labda ita work out,..........But imekuaje umechelewa hivi?jua limezama dada yangu dah. Anyway All the Best

Sikupenda kuchelewa, nilimsubiri mtu ambae mwisho wa yote alikutana na mwingine akaoa ila yote ni mipango ya Mola.
 
Mkuu Upo?
Ulikuwa Kimya Sana

Yaani Watu Kwenye Hii Thread Wanashangaa Huyu Dada Kuwa Na Umri Mkubwa Wakat
Haya Ni Mambo Ya Kawaida Sana

Ajaribu Kuwa Makini Shida Kubwa Watu Hupenda Slope Mno

Nipo mkuu!
Nilikuwa napita tu bila michango,ila nipo!!

I wonder wakati kawaida tu umri huo wengi wapo hawajaolewa!!

Yes cha muhim awe makini sn maana vijana sikuhizi mmh!
BT kasema Ana kazi nzuri pia huyo kijana!
So naona kijana anataka kupata uhakika wa uzao kwanza kabla hajaweka ndani!!!
 
Miaka 44 unaweza shika mimbaa kweli na je tangu ujana wako hujawahi kuwa na mpenzi?
 
Sikupenda kuchelewa, nilimsubiri mtu ambae mwisho wa yote alikutana na mwingine akaoa ila yote ni mipango ya Mola.

Usijari yupo mtu sahihi kwa ajili yako...mi na doubt kwa uyo jamaa, maana ku date mnavyo date ni tofauti sana na kuishi pamoja forever, kwanza tu kaanza na mbwembwe za kutaka uzae kwanza. Kwa Mtu mzima hayo ya kuzaa angeweka kapuni na kukuoa kisha ya mtoto yangekuja baada ya ndoa. Kasha ku doubt kama je utaweza zaa so anataka ajue tu, iyo ya kusema sijui nyumbani watasema nini ni kisingizio tu, 31yrs old ni mtu matured mwenye maamuzi yake ktk mapenzi otherwise labda awe mtoto wa mama
 
Hivi miaka 44 wanazaa bila shida?

nafikiri ana wasiwasi akikuoa atapata watoto?
ndo maana anataka mzae kwanza

na wewe ukuendelea kusubiri utazaa na mika 50?

nafikiri huna choice...zaa nae hata asipokuoa angalau utakua na mtoto

tena zaa nae watoto wawili kwa haraka haraka halafu muache mwenyewe aamue kukuoa au kutokuoa.....

Akikatumia hako ka-boy kama dume la mbegu ni bora kuliko IVF! Vinginevyo kajamaa kataongeza idadi na kusepa!
 
Sikupenda kuchelewa, nilimsubiri mtu ambae mwisho wa yote alikutana na mwingine akaoa ila yote ni mipango ya Mola.

Mkuu Pole Sana
Umetoa Ufafanuzi Vizuri
Wengine Wanadhani Ni Makosa Yako Tu
Maana Wewe Mwenyewe Yaliyokupata Ni Makubwa
Umemsubiri Mtu Kakimbia Hiyo Haikuwa Ridhiki

Mungu Ni Mwema Wakati Wote.
 
Sikupenda kuchelewa, nilimsubiri mtu ambae mwisho wa yote alikutana na mwingine akaoa ila yote ni mipango ya Mola.

Pole sana ila hilo linatosha kukupa akili ya kudeal na MMU zaidi ya dogo.

Nakushauri uafanye uamuzi unaoendena na umri wako na usijaribu ukikumbuka kwamba uko mbele ya washindani wako kwa zaidi ya miaka 20. Vigezo na malengo yako lazima yaakisi hilo.

Ushauri wa The Boss ni muhimu sana.
 
Last edited by a moderator:
Duh!! hawa wanaokushauri ni watoto wako ujue.
wengi wao bado wana muda wa kutosha kumsubiri huyo Mungu awaletee mume mwema.
yawezekana wewe ndio Mungu kakuletea hivyo.

Hata ukizaa na huyo jamaa akakuacha haina shida utabaki na mtoto ambaye atakupa faraja ukizeeka.

mwanamke kujidai gambe ujue kuna ukomo. kuna umri utahitaji wa kukufariji hupati, watoto wa ndugu zako umelea wamesoma wamekuhama wana kwao.
ndugu wanakusimanga na huna msaada.

utaishia kufuga mbwa na paka na kulala nao chumbani.
bora hata ukiwa na mtoto mmoja unaweza lazimisha hata akuletee mjukuu umlee. hao wa ndugu hawatakuletea hata mjukuu kukusalimia.

wadada ukiona wakati unaishia na jamaa wamekuzingua we zaa tu hata upate mtoto wa kukupa faraja. tafuta hata wa kwenye sperm bank.
hata kusuguana na wenzio kuna mwisho wake. lesbian wanaongezeka kila leo na style mpya we na uzee wako watakuhama
 
Duuh..44 kwa 31!! Hebu jamani nipe uzoefu mi mshamba hivi mama wa miaka 44 anaweza kweli kuwa hata na hisia na kijana wa rika hilo...mwwee mjini mna vituko! Mama tafuta japo wa fourty..mwee ndio maana nchi inakuwa na majangaaaaa! Watu wana walaani watoto wa wenzao!
 
Dah... Huyo kijana!!! Mimi Nina uhakika anakutapeli kimapenzi, sijui kwa nini nahisi hivyo. Anataka kukufanyia utapeli wa kimapenzi.

Kama kweli yupo settled na kipato cha uhakika, na wewe una maisha yako, msome kwanza...give it some time..wewe ni mtu mzima, sidhani kama unaendeshwa na mihemko kivile. Mda utakupa majibu yote...ila nna wasiwasi anakutapeli kimapenzi
 
duh!! hawa wanaokushauri ni watoto wako ujue.
wengi wao bado wana muda wa kutosha kumsubiri huyo Mungu awaletee mume mwema.
yawezekana wewe ndio Mungu kakuletea hivyo.

Hata ukizaa na huyo jamaa akakuacha haina shida utabaki na mtoto ambaye atakupa faraja ukizeeka.

mwanamke kujidai gambe ujue kuna ukomo. kuna umri utahitaji wa kukufariji hupati, watoto wa ndugu zako umelea wamesoma wamekuhama wana kwao.
ndugu wanakusimanga na huna msaada.

utaishia kufuga mbwa na paka na kulala nao chumbani.
bora hata ukiwa na mtoto mmoja unaweza lazimisha hata akuletee mjukuu umlee. hao wa ndugu hawatakuletea hata mjukuu kukusalimia.

wadada ukiona wakati unaishia na jamaa wamekuzingua we zaa tu hata upate mtoto wa kukupa faraja. tafuta hata wa kwenye sperm bank.
hata kusuguana na wenzio kuna mwisho wake. lesbian wanaongezeka kila leo na style mpya we na uzee wako watakuhama

Ni ushauri mzuri sana kwa wasichana. Hata safari ya matumaini lazima iwe na kikomo. Vinginevyo yanakuwa matumaini hewa.
 
Back
Top Bottom