Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Miaka 31 kwa 44 siyo mbaya hata kidogo. Kwa sababu wote mpo kwenye utu uzima. Na miaka siyo tatizo sana, tatizo pia linakuja kwenye umbo. Unaweza kuwa na miaka midogo umbo la kizee ni mbaya. Au ukawa na miaka mingi ila umbo la kitoto/makamu. Kwa miaka yote hiyo je maumbo yenu yanaendana au? Kwa umri wenu wote je mnatarajia kuwa na familia ya watoto wangapi kwa muda wa kipindi gani? kuna vingi vya kuzingatia kabla ya kusema Tunapendana sana. Kupendana sana haitoshi...
Sasa tatizo kubwa ni lipi mdogo wangu?
Aaah wapi.....mimi nilipokuwa na miaka 27 wewe hata kusoma ulikuwa bado hujajua. Eli79 hii sio Id yako nyingine kweli?
Sawa. Ila tofauti hiyo kwa bongo ni ndogo?
At retirement, dogo atakuwa na umri gani na atakuwa wapi?
Ndoa ni zaidi ya ngono mkuu!
Mmh..rafiki, kweli? Niwe na ID mbili kwa natafuta nini jf! Hii moja inanitosha sana, dogo kapatia umri nini??
U love him because of the exposure and his smartness, kwa kiswahili tunasema umemtamani! Wacha aendelee kuwa boyfriend wako lakinj si kumfanya awe mumeo, unless u'll regret!🙄
Kwa hiyo unamshauri acheze bahati nasibu? Kwamba wakipata mtoto, hata jamaa akimuacha awe na Faraja ya kuwa na mtoto?
dada mpaka sa8 usiku mnaongea tuu live bila chenga wala umeme kukatikakatika??
ushauri....wewe kama mnapendana bebaneni tu muoane tena kwa shangwe zote! wambie unamiaka28! kwani wakwe watadai cheti cha kuzaliwa???
He made the first move, nimerespond to his move, pia ninaenjoy kuongea nae.
Hivi miaka 44 wanazaa bila shida?
nafikiri ana wasiwasi akikuoa atapata watoto?
ndo maana anataka mzae kwanza
na wewe ukuendelea kusubiri utazaa na mika 50?
nafikiri huna choice...zaa nae hata asipokuoa angalau utakua na mtoto
tena zaa nae watoto wawili kwa haraka haraka halafu muache mwenyewe aamue kukuoa au kutokuoa.....
ulimpa papuchi mara ngapi? dogo kanogewaUmri wangu ni miaka 44, sijaolewa na sina mtoto. Ninafanya kazi katika taasisi ya serikali, mwanzoni mwa mwaka huu nilipelekwa semina kwa wiki moja. Tukiwa kule kiti changu kilikuwa karibu na kiti cha kijana mmoja, mrefu, nadhifu, mcheshi. Tulifikia hoteli moja, baada ya siku tatu tulishabadishana number za simu maana tuliweza kuelekezana migahawa mizuri kwa chakula. Semina iliisha Ijumaa na tuligwa kwa tafrija baada ya hapo kila mtu aliekea alikotoka.
Mimi na kijana tuliendelea kuwasiliana kwenye whatsApp, imefikia katika hali kuwa, nikiamka asubuhi lazima tusalimiane, tunabadishana picha za lunch, usiku ndio kabisa tunachat masaa mawili-matatu. Ilitokea nikamuuliza hivi unahisi mimi ninamiaka mingapi? Akajibu 28, nilicheka, nikaamua kukaa kimya. Moyo wangu umempenda sana, sasa lakini niliamua kumueleza ukweli. Alistuka na kukaa kimya, nikajua basi ameshaondoka. Kesho yake alinipigia simu akaniuliza kama nilishawahi kuolewa, je ninamtoto. Akajibu umri kwake sio tatizo. Yeye anamiaka 31, anakazi nzuri sana.
Weekend iliyopita alikuja kunitembelea, alifika Jumamosi asubuhi, kwasababu bado tunafahamiana alichukua hoteli mjini, alikuja kwangu jioni, tulikaa tukaongea mpaka saa nane usiku, akaondoka kurudi hotelini kwake, kesho yake alirudi kwake. Dada yangu mkubwa ambae mtoto wake wa kwanza anamiaka 29 ameniambia nimuache kijana kwani ni sawa na mwanangu!! Kijana mwenyewe amekiri kuwa kwao wazazi wataleta zengwe, amenishauri tuzae kwanza kabla hajanipeleka kwao. Ushauri jamani.
Kuna ubaya gani?
Hope hutaongelea habari ya kutenda dhambi kwani hapa kuna mtu keshamtamani mtoto wa mwenzie!
Siwezi kusema ni tapeli au la, nilimuuliza sababu za yeye kutokuwa na girlfriend akanijibu vizuri tu kuwa kwa muda mrefu alikuwa nje ya nchi kikazi so long distant relationship haikuwork out.
You nailed it!!! Yeye ni mrefu, ni mtu wa mazoezi lakini akiacha anakuwa na nyama uzembe. Mimi ni 5.6ft tall. Ninatembea one hour morning and another hour evening. Kwakweli magauni yananipendeza sijisifu. Kingine ninampa heshima sana kama mwanaume, ninamsikiliza. e.g. Last week nilikuwa kwenyemkutano Ijumaa wadada niliokuwa nao walitaka tuunganishe weekend huku kwasababu ni kando ya bahari na upepo ni mzuri. Aliniambia nirudi kwangu kama mkutano umekwisha, nilipanda ndege Ijumaa na sasa niko kwangu.