Nimeng'atwa na nyoka ndotoni

Nimeng'atwa na nyoka ndotoni

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Poleni na majukumu watu wa humu, niende moja kwa moja kwenye mada,

Tulikuwa watu zaidi ya watatu, tulikuwa kwenye eneo Kama mbuga hivi ambalo ni nyasi kwa wingi, Sasa ilikuwa ni Kama unachagua pa kukanyaga maana Kila baada ya hatua tatu ni nyoka wakubwa kwa wadogo,

Ikatokea nyoka mmoja mkubwa akanirukia na kuning'ata kisogoni, basi nukawa napiga kelele lakini mwenzangu akachuma majani ya mchunga chapu na kuanza kunipaka nilipong'atwa huku akiniambia ni dawa na nitapona tu nisijali,

Sasa wakati nasubiria kupona ndo nikashtuka kutoka usingizini,

Je hii ndoto Ina maana gani wakuu.
 
Kwa ulimwengu wa ndoto nyoka means uchawi.
Hapo Ina maanisha Pana nguvu ya uchawi ishaingizwa mwilini mwako.
Yaani ushatupiwa uchawi subiria matokeo.
Sasa kiimani zipo njia nyingi za kuuflash uchawi mwili.
Matokeo yeyeto nje ya mwili uanzia ndotoni,unaweza ukaliblock jambo mapema kabla halijatokea kimwili.
 
Binafsi nliota napambana na nyoka mkubwa,katika mapambano yale akaniweka mtu kati😂😂,akaning'ata mguu wangu wa kushoto halafu mguu wangu wa kulia akawa kauzungushia sehemu ya mkia wake. Wakati nahangaika kumtoa ndo kuamka kutoka usingizini na sikuwa nmemtoa kwenye miguu yangu.
Imenipa mawazo sana.
 
Ndoto ni ujumbe toka Kwa Mungu au shetani.
Na ndoto inatafsiri nyakati tatu pana tukio lililopita yaani lilishafanyika nyuma
Tukio linaloendelea sasa au tukio linalotegemea kutokea baadae.
Ukiweza kucheza na ndoto ni rahisi kucontrol maisha Yako.
 
Binafsi nliota napambana na nyoka mkubwa,katika mapambano yale akaniweka mtu kati😂😂,akaning'ata mguu wangu wa kushoto halafu mguu wangu wa kulia akawa kauzungushia sehemu ya mkia wake. Wakati nahangaika kumtoa ndo kuamka kutoka usingizini na sikuwa nmemtoa kwenye miguu yangu.
Imenipa mawazo sana.
Lini uliota na vipi matokeo ya hali yako baada ndoto pana mabadiliko yeyeto negative
 
Ndoto ni mawazi tu yanayokujia ukiwa usingini,watu tumeshaota tunakimbizwa na mbogo na hakuna baya lililotokea
Kuwa na amani mkuu na uendelee na maisha yako
 
Mkuu una mizimu ya uganga hapo umepewa ujumbe kuwa hiyo ni anti ~venom, cha kufanya tafuta wale panya weupe umkutanishe nja nyoka anga'twe then testia hiyo dawa au chukua panya na mifupa ya nyoka mchome nayo kisha mpe hiyo dawa usisahau kutuletea mrejesho, ila iuo mchunga huwa ni antibiotic kali sana kwa watu wanaougua tetekuwanga pia ni hormones kimtindo kwa wamama ambao hawatoi maziwa ya kutosha wanaponyonyesha watoto mwisho kabisa ni dawa ya magonjwa ya tumbo hasa hasa bowel inflamation kwa watoto kimtaamtaa mnaita chango ila sikuwahi kujua kama ni anti venom
 
Binafsi nliota napambana na nyoka mkubwa,katika mapambano yale akaniweka mtu kati😂😂,akaning'ata mguu wangu wa kushoto halafu mguu wangu wa kulia akawa kauzungushia sehemu ya mkia wake. Wakati nahangaika kumtoa ndo kuamka kutoka usingizini na sikuwa nmemtoa kwenye miguu yangu.
Imenipa mawazo sana.
Kungatwa na nyoka mguuni ni adui amepanga na amefanikiwa kuzuia hatua zako kiimani, kiuchumi, kiafya nk nk.

Imeandikwa Imebarikiwa miguu Yao wapelekao INJILI,

Kungatwa mguu maana ya kuwa usiweze kuhubiri kama ni mchungaji, kama ni biashara urudi nyuma nk nk.

Hakikisha unakemea na kuomba sana, pia hakikisha unalipa fungu la kumi Ili kuondoa Hila za shetani.

Usipuuzie nilichokwambia.

Ubarikiwe.
 
Poleni na majukumu watu wa humu, niende moja kwa moja kwenye mada,

Tulikuwa watu zaidi ya watatu, tulikuwa kwenye eneo Kama mbuga hivi ambalo ni nyasi kwa wingi, Sasa ilikuwa ni Kama unachagua pa kukanyaga maana Kila baada ya hatua tatu ni nyoka wakubwa kwa wadogo,

Ikatokea nyoka mmoja mkubwa akanirukia na kuning'ata kisogoni, basi nukawa napiga kelele lakini mwenzangu akachuma majani ya mchunga chapu na kuanza kunipaka nilipong'atwa huku akiniambia ni dawa na nitapona tu nisijali,

Sasa wakati nasubiria kupona ndo nikashtuka kutoka usingizini,

Je hii ndoto Ina maana gani wakuu.
Kuumwa nyoka kichwani:

1. Huna ulinzi kiroho, ndomana nyoka amefanikiwa kukuuma.

2. KICHWA ni eneo nyeti, ni engine ya MWILI, hivyo hatari Yako ni kubwa.

3. Shambulizi la KICHWA limelenga kukudhoofisha kiuongozi, maana KICHWA ni Mwanaume, kiongozi.

Umelengwa uvurugwe katika kuwaza, mipango, MIKAKATI kufikiri nk nk.

Umengatwa tayari, hivyo usizubae, tafuta ulinzi wa haraka wa Mungu Kwa kumtafuta kiongozi au mtu wa Mungu aliyeokoka mwenye nguvu za Mungu akusaidie.

4. Mbuga yenye majani, ni sehemu ya KAZI, shambani au kazini, hivyo umeambiwa, waliokushambulia ni katika eneo la kutafuta riziki.

5. Mtu anayekupaka majani ya mchunga ni adui anayekufariji Ili upoteze maxima, litatokea tatizo usipoomba, ambalo litakuwa kubwa, lakini watu wa karibu, marafiki wabaya, watakupa ushauri mbaya Ili upotee.

Badili Rafiki zako.

Ushauri: Tafuta mtumishi wa Mungu aliyeokoka, aliye na nguvu za Mungu, akusaidie kukunasua maana katika spiritual realm, umeshapigwa tayari, ukipuuza, muda Si mrefu, yatakutokea.

Mungu akubariki.

Aamen
 
Back
Top Bottom