LA7
JF-Expert Member
- Aug 26, 2019
- 655
- 2,369
Poleni na majukumu watu wa humu, niende moja kwa moja kwenye mada,
Tulikuwa watu zaidi ya watatu, tulikuwa kwenye eneo Kama mbuga hivi ambalo ni nyasi kwa wingi, Sasa ilikuwa ni Kama unachagua pa kukanyaga maana Kila baada ya hatua tatu ni nyoka wakubwa kwa wadogo,
Ikatokea nyoka mmoja mkubwa akanirukia na kuning'ata kisogoni, basi nukawa napiga kelele lakini mwenzangu akachuma majani ya mchunga chapu na kuanza kunipaka nilipong'atwa huku akiniambia ni dawa na nitapona tu nisijali,
Sasa wakati nasubiria kupona ndo nikashtuka kutoka usingizini,
Je hii ndoto Ina maana gani wakuu.