Poleni na majukumu watu wa humu, niende moja kwa moja kwenye mada,
Tulikuwa watu zaidi ya watatu, tulikuwa kwenye eneo Kama mbuga hivi ambalo ni nyasi kwa wingi, Sasa ilikuwa ni Kama unachagua pa kukanyaga maana Kila baada ya hatua tatu ni nyoka wakubwa kwa wadogo,
Ikatokea nyoka mmoja mkubwa akanirukia na kuning'ata kisogoni, basi nukawa napiga kelele lakini mwenzangu akachuma majani ya mchunga chapu na kuanza kunipaka nilipong'atwa huku akiniambia ni dawa na nitapona tu nisijali,
Sasa wakati nasubiria kupona ndo nikashtuka kutoka usingizini,
Je hii ndoto Ina maana gani wakuu.
Kuumwa nyoka kichwani:
1. Huna ulinzi kiroho, ndomana nyoka amefanikiwa kukuuma.
2. KICHWA ni eneo nyeti, ni engine ya MWILI, hivyo hatari Yako ni kubwa.
3. Shambulizi la KICHWA limelenga kukudhoofisha kiuongozi, maana KICHWA ni Mwanaume, kiongozi.
Umelengwa uvurugwe katika kuwaza, mipango, MIKAKATI kufikiri nk nk.
Umengatwa tayari, hivyo usizubae, tafuta ulinzi wa haraka wa Mungu Kwa kumtafuta kiongozi au mtu wa Mungu aliyeokoka mwenye nguvu za Mungu akusaidie.
4. Mbuga yenye majani, ni sehemu ya KAZI, shambani au kazini, hivyo umeambiwa, waliokushambulia ni katika eneo la kutafuta riziki.
5. Mtu anayekupaka majani ya mchunga ni adui anayekufariji Ili upoteze maxima, litatokea tatizo usipoomba, ambalo litakuwa kubwa, lakini watu wa karibu, marafiki wabaya, watakupa ushauri mbaya Ili upotee.
Badili Rafiki zako.
Ushauri: Tafuta mtumishi wa Mungu aliyeokoka, aliye na nguvu za Mungu, akusaidie kukunasua maana katika spiritual realm, umeshapigwa tayari, ukipuuza, muda Si mrefu, yatakutokea.
Mungu akubariki.
Aamen