Nimenuniwa kisa nimejiita Bachela mbele yake!!!!

Hapa nimechekasana umeongea kweli..kwanza mleta mada ulimwambia gf wako kuwa unataka kumpa mtu lifti?? Halafu wewe na huyo jirani yako mnakoroga stori na kumwacha bibie kama sanamu la michelini....Yes, wewe ni bachelor ila hukuiweka vizuri kimaongezi...
 
Hata km ni mm ningekununia tu,tena ningeanza kujifikiria upya kuhusu ww!kwan km ungepotezea hilo swali ingekuwaje?alafu inaonekana ni mgumu sn kukubali makosa yako na kutubu!imajin watu wanavyokushauri na kukuonesha ulipokosea still huelewi!uwe unafikiria cha kusema kabla ya kusema cku zote kila neno kwenye mapnz linakua na uzito wake,hapo ulionyesha dharau na kushusha thaman ya mwenzio!
 
Mkuu,
Sikumaanisha sina mtu, na kwanza mgeni alivyoingia tu nlianza utambulisho mfupi kwa kila mmoja wao!!!

Wewe jifanye kubisha tu, kauli ulioitumia haistahili kabisa hasa kwa mazingira mlokuwepo! Sasa endelea kubisha ili uwe unarudia makosa yale yale tu!!
 
Hapana Lizzy,

Hao tunawashauri wakiona mambo hayaendi, watafute midume isiyojielewa waikamate masikio...

Mwisho wa siku kila mtu ajitahidi kutafuta furaha, raha na amani!!

Babu DC!!

Hahahahah. . . babu si bora nikachunge ng'ombe nijue kabisa nawapelekesha kwasababu wao sio wanadamu?
 
Miss ya saaana mwanakwetu, mambo niaje?? Dah.....naona jamaa anajaribu kufananisha kesi za mapenzi na zile za wizi wa kuku mahakamani!! LOL
 
Miss ya saaana mwanakwetu, mambo niaje?? Dah.....naona jamaa anajaribu kufananisha kesi za mapenzi na zile za wizi wa kuku mahakamani!! LOL

Missing u 2 wakwetu,huyu jamaa anaomba ushauri akiwa tayari na maamuzi!alafu ni aina ya wale wanaoona ni jinai kukubali kosa na kutubu ili kuweka mambo sawa!hapo hajielewa hata alipokosea co kila kitu kinakua kawaida kila wakati!
 
Nakuonea wivu kisenzi ! Wewe lazima uta'parfom vizuri ! Una gari, na Dem permanent ! Kwa nini buku lisishuke !

Buku lenyewe kama ndio linaambatana na manuniano kama haya ntafaulu vipi??
Hapa nimeganda nje kwake kama jana na hataki kutoka.
Sasa mmenishauri nimuombe msamaha, sasa nitamuombaje mtu ambae hajibu msg, hapokea simu wala hataki kuniona??
Leo ni public holiday, nimemu-sms tukutane mahali ili tuyamalize nikaganda weee mpaka muda huu ndo nimeamua kuja kwake!!
Nakubali kosa kua nlikosea, ingawa sio kosa kubwa sana kivile, but nitaelezaje kukiri kwangu kosa!!!!
 
Msamehe bure,

Alijisahau kwamba ana GF wake akaanza kum-impress jirani!!!!

Ni technical miscalculations....atajua jinsi ya kuhandle mambo kadri anavyokua na kujifunza mengi!!

Hii practical session lazima itamsaidia sana kujua la kufanya next time!!

Babu DC
 
Naamini bwana Shark ataelewa kwa nini watu wengi tukiwa na wake zetu tunakuwa wapole sana hata kama wakati mwingine tunajulikana kama mafyatu!!

Neno moja tu, cost yake wakati mwingine hailipiki...Dawa yake ni kukaa kimya tu!!

Babu DC!!
 
Hahahahah. . . babu si bora nikachunge ng'ombe nijue kabisa nawapelekesha kwasababu wao sio wanadamu?

Huyo ni wewe Lizzy, wenzio wanatumia mbinu zozote halali na haramu kubadilisha status....Kuna dada mmoja amembaka mate wetu na harusi ilikuwa December 2011!!

Haya mambo ni ya kawaida tu!!

Hahahahahahaha.
Asante kwa kunichekesha babu, kweli ishi uone mambo na majambo.
 
Shark,

Kama kweli wewe ni mwanafunzi basi unahitaji kwenda shule zaidi...Inaonekana bado kabisa shule haijapanda!!

Kwani katika maisha unakuwa na mbinu moja??? Kama hataki kuongea na wewe, ina maana haongei na watu wengine?? Hebu fikiria basi beyond your nose!!

Halafu wewe umetuma sms na yeye hakakujibu, unawezaje kwenda kumsubiri kana kwamba mmepeana appointment??

Kwa mwendo huo, take precautions kwani ukikutana na mwanamke mjanja mjanja atakupelekesha kama gari bovu....

Babu DC!!
 
huyo jiran ana mawili eiza anakutaka au mgombanishi, mwanamke mwenye adabu hawez kuanza kukuulizia usafi wa gari wakati haimuhuu, jishushe endelea kumbembeleza jarbu kuongea na watu wake wa karbu pia ili muonane
 
Naamini bwana Shark ataelewa kwa nini watu wengi tukiwa na wake zetu tunakuwa wapole sana hata kama wakati mwingine tunajulikana kama mafyatu!!

Neno moja tu, cost yake wakati mwingine hailipiki...Dawa yake ni kukaa kimya tu!!

Babu DC!!

Babu DC,hope kwa ubishi na ugumu wa kuelewa alionao huyu jamaa nachelea kusema bado ni mvulana,akiwa mwanaume ataacha na atakua keshaelewa namna ya kuchambua maneno ya kuongea akiwa na mpnz wake.
 
Babu DC,hope kwa ubishi na ugumu wa kuelewa alionao huyu jamaa nachelea kusema bado ni mvulana,akiwa mwanaume ataacha na atakua keshaelewa namna ya kuchambua maneno ya kuongea akiwa na mpnz wake.

Kweli kabisa,

Baada ya kupita stage ya kuwa mvulana, naamini atafahamu the power of a woman na kwa hiyo atakuwa tayari keshabadilika na kuwa mwanamume!!

It takes time to train.....Tumsaidie ajue jinsi ya kukwepa kufanya makosa madogo madogo lakini yenye madhara makubwa linapokuja suala la kudeal na wanawake!!

Babu DC!!
 
Babu DC,hope kwa ubishi na ugumu wa kuelewa alionao huyu jamaa nachelea kusema bado ni mvulana,akiwa mwanaume ataacha na atakua keshaelewa namna ya kuchambua maneno ya kuongea akiwa na mpnz wake.
Mkuu, Sijui kikomo cha uvulana ni miaka mingapi, nina umri miaka 30 na nusu, na shule nayosoma ni MBA-Mzumbe baada ya miaka 5 baada ya ku-graduate BA.
 
Mkuu, Sijui kikomo cha uvulana ni miaka mingapi, nina umri miaka 30 na nusu, na shule nayosoma ni MBA-Mzumbe baada ya miaka 5 baada ya ku-graduate BA.

Shark,

Jinsi ambavyo umejibu posts za wadau, imewapa wasi wasi wengi wetu kama kweli unazoefu na hawa wadau wenzetu. Ndiyo maana si lazima uwe na miaka 18 ili uitwe mvulana. Kuna watu wanakaribia 40yrs ila kwa tabia zao, unaweza kudhani ni teens!!

Kwa hiyo pamoja na umri wako kuwa si mdogo, inawezekana ama uzoefu wako na wanawake si mkubwa au kuna kitu bado unahitaji kujifunza ili uweze kukwepa kuangukia katika hali kama hii iliyokukuta!!

Babu DC!!
 
Ana kila sababu ya kukununia, hapo ukijaribu kuangalia kwa makini utagundua tatizo sio neno Bachelor ila tatizo ni tafsiri nzima ya maneno yako ambayo kwa namna moja ama nyingine yamemdhalilisha huyo unayemuita mchumba wako, ikiwa na maana hata huyo uliyenae hakuna anachokifanya katika kuhakikisha wewe unaweka mambo yako katika utaratibu wa kueleweka, jambo ambalo si kweli. Wewe kwenye majibu yako umeonyesha ubinafsi wa hali juu sana, ulikurupuka kujibu kwani ulikuwa na option nyingi za kujitetea sio kukimbilia kutoa jibu la namna hiyo. MWOMBE RADHI TAFADHALI:
 
sasa kama umenuniwa ndo iwe aje tena, na wewe mnunie mpaa siku amewacha ma wewe unawacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…