Dawa ya Mbu jau sana Mimi mwenyewe nilishanusurika kukata upepo.
Nakumbuka wakati nipo Chuo kuna siku nimerudi home nimechoka ile mbaya. Kulala na Neti siwezi kabisa, nikachoma ile dawa ya Mbu ya coil.
Nikalala kws sababu nilikuwa nimechoka sana nikawa nimelala huku nimejiachia sana mto wa kulalia ukadondoka chini karibu na ile dawa ya Mbu, ile pillow ikaanza kuungua na mimi nipo usingizini huku nakohoa bila kujitambua.
Watu wamekuja kuvunja mlango wakanitoa nje niko hoi nimeshakohoa non stop na macho yamevimba, mbavu na kifua vinauma sana.