Nimenusurika Kupigwa Risasi na Polisi usiku huu

Acha porojo kijana
 
Naunga mkono hoja....
 
This time nikula na kuosha vyombo
 
This time nikula na kuosha vyombo
Aiwaaa.
Wewe km mimi.
Tena hii hali imesababisha mpk nijue home work za watoto zikoje . Na majina ya majirani zangu wengi tu ambao zamani ilikuwa salamu tu.

Kumbe kila shari kuna kheri ndani yake
 
Ila mkuu kwa Sasa nawaasa.na wanaume wengine usitembee na familia ...iache nyumban kabisa ..kama unatoka toka mwenyewe....na pia hakuna sababu ya kutembea usiku..mahitaji watu wamefanya muda wa mchana...ama jioni...
Huyo Mtoto na Mke ndio pona yake, fikiri angekuwa na njemba mbili ingekuwaje?
 
Propaganda mshaanza ili kutia hofu watu…cjui nyie mboga mboga mkoje.
Hujawahi kuingia mikononi mwa polisi wewe. Polisi wengi ni wa HOVYO.
Miaka kama kama 3 iliyopita niliwahi kupigiwa simu na mzee mmoja kutoka kijijini, mzee huyo tunafahamiana. Aliniambia niende kituo cha polisi Chang'ombe kwani kijana wake kakamatwa, polisi ndo waliompigia simu. Nilianza safari ya kuelekea kituoni pale, kufika nikaeleza shida yangu, wakaniuliza jina la kijana, nikataja. Walipekuwa kwenye madaftari yao pasipo kuliona kina lake. Nikajibiwa kubwa huyo mtu hayupo kituoni kwao.
Niliandika na kupelekwa sehemu alikokuwa akiishi, majirani zake wakaniambia kubwa alikamatwa jana yake jioni na polisi. Nikarudi kituoni nikawaeleza kuwa aliletwa hapa kwa kujibu wa majirani zake, askari mmoja wa kike akachukua daftari na kukagua, akikosa jina. Wakti huo kaka yake huyo kijana anayeishi Iringa alifika kuja kufuatilia issue ya mdogo wake, alifika na kuzungumza na askari mmoja kisha akanifuata na kunitaka nimwqzime sh. 50,000/- nikampa, baada ya dk kama 7 hivi akitolewa nje kutoka hapohapo kituoni!. Nilipomuuliza kaka mtu imekuwaje? akasema ametoa sh. Laki 2, ile hamsini nilomkopesha ulikuwa imepungua kwani yeye alikuwa na 150,000/- mfukoni.
Mimi walinikatalia katakata kubwa huyo mtu hayupo na sijuwi walijuaje kuwa sikuwa na mpango wa kuwapa hela.
 
Kuna madereva wengine sijui udereva wamejifunzia wapi inawezekana na wewe ni mmojawapo.

Mtu usiku kapaki gari pembezoni mwa barabara unapishana naye unakuta jitu limewaaha taa (Low Bean l/High Beam) badala ya kuwasha taa za parking, yaani inakuwa ni kero.

Sasa kama mimi dereva mwenzio nakereka wakati niko barabarabu sasa hao askari unategemea wasikereke?
 
Hivyo vyuma mnavyotishia watu, soon or later kila mtu atakuwa nacho, kuna wenye akili kuliko nyie, watu wameshaona fursa, police na CCM wameamua kuharibu nchi mtapata mlichokuwa mnatafuta
 
Ndio sababu ya kumpigisha mtu magoti na kutoa bunduki au? hizi akili za mavi mnatoaga wapi
 
Hivyo vyuma mnavyotishia watu, soon or later kila mtu atakuwa nacho, kuna wenye akili kuliko nyie, watu wameshaona fursa, police na CCM wameamua kuharibu nchi mtapata mlichokuwa mnatafuta
Sasa hizi kelele zoote za nini.?
We si umeamua kwenda kinyume na amri ya serikali? Basi njoo mitaani.

Unapiga kelele humu kwa sababu huna jeuri ya kuandamana... full stop
 
Acha uoga dogo. Ingetakiwa uwe shujaa wa kwanza kwa siku ya leo. Ulitakiwa upite nao mara baada ya kuingia kwenye gari.

Ungewagonga tu.
 
Hii story naweza kuikubali bila shaka.
Hakuna mtu mwenye akili timamu asiekubali kuwa polisi na sehemu nyingi serikalini wanakula rushwa.

Lkn juu ya hivyo sisapoti kabisa watu kuandamana.
Vijana tunawahitaji kujenga hili taifa. Hatutaki kuona vijana wetu wanakufa kwa kosa la kuvunja sheria . Hata km sheria hizo ni kandamizi.
Uhai wa mtu huwezi kulinganishwa thamani yake ni chochote duniani.
 
Naona chawa wa Mama Asubuhi umeungia mzigoni. Leo umeahidiwa kulipwa Tsh ngapi maana umeamka Asubuhi sana kuanza kazi. 😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…