Nimenusurika kuuliwa na radi

bora we imekukosakosa shukuru MUNGU aya lete sadaka kwa mwamposa
 
Kuna moja ilinimulika mchana huko kigoma hadi nikahisi nilikuwa nafanyiwa upareshen ya macho nikatoka mbio nikakimbilia kwenye mtaro wa maji wakati nilikuwa nimejificha kwenye kibaraza cha nyumba za barabarani
Ahahaaaa

Siku nyingine ukiona radi usikimbilie kwenye maji maana kwenye maji ndo Kuna njia zake

Pole sana mtumish

Sasa ungetuwipa oreshink ingekuwaje sasa
 
Radi Iko kama jogoo au ni kama kondoo?
 
Mmh radi ipige mita 2 toka ulipokaa halafu isikudhuru?
 
Pole sana, niliwahi koswakoswa na radi nikiwa nyumbani nimejikinga mvua sebureni baada ya kutoka shambani. Ilipiga kwa kishindo kikubwa kiasi ambacho nilihisi kuangukiwa na ukuta wa nyumba, nilipiga yowe kubwa ambalo sijui lilitoka wapi.

Sikuwa nimewasha electronic device yoyote ila nilikuwa karibu na socket ya umeme. Kile kilichonitokea hakielezeki kwa maneno ila ni rahisi kwa aliyewahi kukutwa na hali hiyo kuelewa. Nashukuru sikudhurika.
 
Inakuwaje radi inakuja ndani
Ama ni nyumba hazina waya zile sijui za nini
earth ama kitu gani
Wataalamu tunaomba elimu pls
 
Radi ni millions of voltage huwa hanusuriki mtu,
 
Sasa mim huwa naamin radi huwa haingii ndani

Huku kwetu iliwah pasua watu,walikuwa wamejibanza kibarazan sasa mmoja wao akawa anaongea na sm,sahv ukitoa tu sm wakat mvua inanyesha watu wanaweza kukupiga mabanz

Kuna mwalim wa technical aliwah kutuambia eti vifaa vya electronic haviwez kukusababishia kupigwa radi,lakin ajabu huku kuna watu wanapigwa unakuta yeye kafa na kifaa alichokuwa nacho simu au redio imepasuka na kuungua
 
Hiyo ilishawahi kunikuta zile nyumba za kizamani ambazo mawaya ya umeme yalikuwa nje.Kilipiga kitu mpaka nyaya zikawa zinatoa mvuke.Watu ikabidi kuvurumka ndani tena kwenda nje😁😁😁
Nyieee kuweni serious basiπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Reactions: EEX
Ulikua na viatu au kandambili miguuni?
 
Lightning bolt huwa na kawaida inapo make contact kwenye ground, inarusha au kusambaza charges katika mazingira yanayoizunguka.. hivyo kama wewe sio contact, basi utaishia kupata electrical burns and sometimes hearing/vision problems kutokana na sound and light it makes (It depends na distance ulosimama from the contact)

Otherwise, ukiwa wewe ndio contact, basi utakua umesaidia kukamilisha circuit maana umeme utapita through you towards the ground, hivyo sababu kubwa ya kifo huwa ni cardiac arrest due to arrhythmias, kumbuka moyo nao una conducting system yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…