Nimenyimwa kukopeshwa mkate wa buku nikanywe chai na familia yangu

Nimenyimwa kukopeshwa mkate wa buku nikanywe chai na familia yangu

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Huyu muuza duka nimejuana nae miezi 3 iliyopita na toka hapo nakopaga ila nampa pesa yake jioni nikifeli saana kesho asubuhi nampati.

Sasa Jana asubuhi nimepitia hapo asubuhi baada ya kutoka kwenye ofisi yangu nikamwambia anipe mkate wa buku hela nampitishia jioni, akagoma kunipatia akidai faida yake ni ndogo sana nikakubali matokeo nikaondoka ila jioni nimepita nikamuungisha mkate na unga, lipa wema kwa ubaya.
 
Ila maisha bwana!
Nakumbuka wakati fulani miaka 10 nyuma niliwahi kuacha 200 nyumbani halafu sina ramani yoyote, ila haikufika saa nne nilipata hela ya kutosha.

Mtoa riziki huwa hakusahau moja kwa moja.
ni mapito tukiamini yajayo yanafurahisha
 
Mambo ya mangi au Muha dukani ndo yanaongeza umuhimu wa kua na mama watoto mweupee peee
Nioneshe muha anaegoma kumkopa mwanamke mweupe
 
Kweli hakuna faraja katika umaskini.

Kuna watu hapa mjini ukiwaambia unaweza kosa buku ya mkate wanakucheka.

Usimlaumu sana ukizingatia kila siku alikuwa anakukopesha. Ukute na yeye siku hiyo biashara haikuwa sawa na yeye alikuwa anatafuta buku tu familia yake ikale.
 
Back
Top Bottom