Huyu muuza duka nimejuana nae miezi 3 iliyopita na toka hapo nakopaga ila nampa pesa yake jioni nikifeli saana kesho asubuhi nampati.
Sasa Jana asubuhi nimepitia hapo asubuhi baada ya kutoka kwenye ofisi yangu nikamwambia anipe mkate wa buku hela nampitishia jioni, akagoma kunipatia akidai faida yake ni ndogo sana nikakubali matokeo nikaondoka ila jioni nimepita nikamuungisha mkate na unga, lipa wema kwa ubaya.
Ila maisha bwana! Nakumbuka wakati fulani miaka 10 nyuma niliwahi kuacha 200 nyumbani halafu sina ramani yoyote, ila haikufika saa nne nilipata hela ya kutosha.
Ila maisha bwana!
Nakumbuka wakati fulani miaka 10 nyuma niliwahi kuacha 200 nyumbani halafu sina ramani yoyote, ila haikufika saa nne nilipata hela ya kutosha.
Kuna watu hapa mjini ukiwaambia unaweza kosa buku ya mkate wanakucheka.
Usimlaumu sana ukizingatia kila siku alikuwa anakukopesha. Ukute na yeye siku hiyo biashara haikuwa sawa na yeye alikuwa anatafuta buku tu familia yake ikale.