I love this quotation. Thank youZaburi 1:2-3
"Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa."
Wewe mpuuzi siku nyingine ukitaka kuchukua mkopo muombe Mungu akupe akili za kufanya maamuzi sahihi kwenye kazi uliyoombea mkopo ili marejesho yasikushinde. Mkopo haurudishwi kwa maombi.Kuna wakati nilikopa mamilioni ya pesa benki na ilipofika siku moja kabla ya deadline ya kulipa installment ya mwisho, sikuwa na pesa kabisa za kulipa. Nilimuomba Mungu, akatenda muujiza, akamuotesha ndoto mtu mmoja. Huyo mtu akanisaidia kulipa installment ya mwisho! Bila hivyo nyumba yangu niliyokuwa nimeiweka kama mortgage ingechukuliwa na kupigwa mnada na benki. Huyo ndugu alisema kabisa kama sio ile ndoto asingenilipia.
Rafiki, huo ushauri ungewapa wanaokopa halafu wanashindwa kurudisha mkopo hadi mali zao zinachukuliwa. Wapo wengi sana. Mimi nimekopa mamilioni mara tatu mfululizo na sijashindwa kurudisha mkopo. Hiyo case ilikuwa special na Mungu amenifundisha kitu kikubwa hapo.Wewe mpuuzi siku nyingine ukitaka kuchukua mkopo muombe Mungu akupe akili za kufanya maamuzi sahihi kwenye kazi uliyoombea mkopo ili marejesho yasikushinde. Mkopo haurudishwi kwa maombi.
Halafu unachekesha rafiki; unaamini Mungu anaweza kukuongoza kufanya maamuzi sahihi kwenye kazi, lakini unakosa imani kwamba Mungu anaweza kukupa pesa ya kurudisha mkopo?! Mungu unamuwekea mipaka ya kile anachoweza kufanya?! Kuna mahali imeandikwa kwamba Mungu hawezi kukupa pesa za kurudisha mkopo? Nini maana ya ombeni lolote mtapewa?Wewe mpuuzi siku nyingine ukitaka kuchukua mkopo muombe Mungu akupe akili za kufanya maamuzi sahihi kwenye kazi uliyoombea mkopo ili marejesho yasikushinde. Mkopo haurudishwi kwa maombi.
Oh God, Increase our faith!Kitabu hiki kina hazina zilizofichika kwa wengi. Waswahili wanasema kizuri, kula na mwenzio. Leo napenda kukushirikisha baadhi ya faida nilizozipata baada ya kuanza kusoma Kitabu hiki na ku-apply yaliyoandikwa katika Kitabu hiki cha ajabu.
Kitabu hiki ni Biblia. Kwanza kabisa, nimeokoa mamilioni ya pesa. Mimi katika maisha yangu nimekuwa nikiugua magonjwa ya aina nyingi sana katika sehemu mbalimbali za mwili wangu. Sasa kila ninapopatwa na ugonjwa wowote, jambo la kwanza ninalolifanya ni kuukemea/kuuamuru ugonjwa utoke kwa Jina la Yesu. Njia hii imeniwezesha kupona makumi kama sio mamia ya magonjwa, tangu nilipoamua kumwamini na kumfuata Yesu. Magonjwa niliyougua yangenifanya nilipe pesa nyingi sana kwa ajili ya vipimo hospitalini na madawa.
Nimeweza kuishi bila kuathiriwa na magonjwa ya zinaa. Nimepata mbinu na maarifa mengi ya kufanikiwa katika kazi na biashara. Nimelindwa na kuokolewa na ajali nyingi sana barabarani na angani zilizokuwa dhahiri kabisa kutokea. Nimepata mahitaji yangu mengi sana just after praying to God. Kuna wakati nilikopa mamilioni ya pesa benki na ilipofika siku moja kabla ya deadline ya kulipa installment ya mwisho, sikuwa na pesa kabisa za kulipa. Nilimuomba Mungu, akatenda muujiza, akamuotesha ndoto mtu mmoja. Huyo mtu akanisaidia kulipa installment ya mwisho! Bila hivyo nyumba yangu niliyokuwa nimeiweka kama mortgage ingechukuliwa na kupigwa mnada na benki. Huyo ndugu alisema kabisa kama sio ile ndoto asingenilipia. Mara nyingi wachawi wamejaribu kunikaba usiku au kutupa wanyama wa ajabu ajabu nje ya nyumba lakini uchawi wao naupiga knock out.
Hizo ni faida za kibinafsi, lakini zipo pia za kijamii, yaani zilizowagusa watu wengine. Kuna mama mmoja alikuwa kila akijifungua anapata mtoto wa kike, na alitamani sana kupata na mtoto wa kiume. Nilimuombea akapata mtoto wa kiume. Kuna mama mmoja alipagawa na mapepo kwa kiwango cha kutaka kumrusha na kumtupa mtoto wake mchanga. Nilimuombea, mapepo yakamtoka. Yuko huru hadi leo.
Hizo ni baadhi tu ya baraka ambazo nimepata tangu nilipoanza kusoma na kuyafanyia kazi yaliyoandikwa katika Biblia.
Nyie mnaosusa kula pilau ya kiroho, inayopatikana katika Biblia, suseni tu, sie twala.
Maneno yako Mungu ni matamu sana kwangu; naam, ni matamu kuliko asali! (Zaburi 119:103)
I certainly shall; if Scripture has already illuminated so much of my understanding, I have every reason to pursue its depths further. Intellectual humility demands that we investigate what we dismiss before presuming ourselves qualified to ridicule it.Endelea kukisoma ili na ujinga ukutoke
Umekosea njia Bwashee, hili sio jukwaa la siasa. Hata hivyo nashukuru umeonja chakula cha uzima.Bwashee una kadi ya CHADEMA
Of course I do! Why wouldn't I?mtumishi, je unatoa fungu la 10?
vipi nikikopa benk milioni 100 alafu nikatoa mil. 10 fungu la kumi, je nitakuwa sahihi?Of course I do! Why wouldn't I?
Yesu anasema katika Yohana 14:15: "Mkinipenda mtazishika amri zangu..."
Na mojawapo ya amri/maagizo ya Mungu ni utoaji wa zaka
Mal 3:10
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Hiyo sasa itakuwa zaka ya mkopoπ. Mkopo sio mapato, ni deni. Ila ukiitoa kama sadaka ya hiari ni sawa.vipi nikikopa benk milioni 100 alafu nikatoa mil. 10 fungu la kumi, je nitakuwa sahihi?
Haya ni madini adimu. Pigia Yesu makofiIn fact bibilia ni kitabu cha vitabu vyote vitakatifu. Ni formula au kanuni ya mafanikio ya kiroho na kimwili kwa yeyote yule alietayari.
"Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni wala si kwa lazima, maana Mungu humpenda yeye atoae kwa moyo wa ukarimu"
2 Wakorintho 9:7
π