Nimeokoa mamilioni ya pesa kwa kusoma Kitabu hiki cha ajabu!

Nimeokoa mamilioni ya pesa kwa kusoma Kitabu hiki cha ajabu!

😂 Inasikitisha sana
Wewe kila uzi unasikitika tu?!
Flp 4:4-7
"Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini. Upole wenu na ujulikane na watu wote. Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu."
 
Yoshua 1:8
"Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana."
Praise the LORD oh my soul.... Psalm 103
 
Zaburi 1:2-3
"Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, na sheria yake huitafakari mchana na usiku. Naye atakuwa kama mti uliopandwa kandokando ya vijito vya maji, uzaao matunda yake kwa majira yake, wala jani lake halinyauki; na kila alitendalo litafanikiwa."
BWANA ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu! Psalm_23
 
BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, ni mwogope nani? Psalm_27
Zaburi 27_1.png
 
Kitabu hiki kina hazina zilizofichika kwa wengi. Waswahili wanasema kizuri, kula na mwenzio. Leo napenda kukushirikisha baadhi ya faida nilizozipata baada ya kuanza kusoma Kitabu hiki na ku-apply yaliyoandikwa katika Kitabu hiki cha ajabu.

Kitabu hiki ni Biblia. Kwanza kabisa, nimeokoa mamilioni ya pesa. Mimi katika maisha yangu nimekuwa nikiugua magonjwa ya aina nyingi sana katika sehemu mbalimbali za mwili wangu. Sasa kila ninapopatwa na ugonjwa wowote, jambo la kwanza ninalolifanya ni kuukemea/kuuamuru ugonjwa utoke kwa Jina la Yesu. Njia hii imeniwezesha kupona makumi kama sio mamia ya magonjwa, tangu nilipoamua kumwamini na kumfuata Yesu. Magonjwa niliyougua yangenifanya nilipe pesa nyingi sana kwa ajili ya vipimo hospitalini na madawa.

Nimeweza kuishi bila kuathiriwa na magonjwa ya zinaa. Nimepata mbinu na maarifa mengi ya kufanikiwa katika kazi na biashara. Nimelindwa na kuokolewa na ajali nyingi sana barabarani na angani zilizokuwa dhahiri kabisa kutokea. Nimepata mahitaji yangu mengi sana just after praying to God. Kuna wakati nilikopa mamilioni ya pesa benki na ilipofika siku moja kabla ya deadline ya kulipa installment ya mwisho, sikuwa na pesa kabisa za kulipa. Nilimuomba Mungu, akatenda muujiza, akamuotesha ndoto mtu mmoja. Huyo mtu akanisaidia kulipa installment ya mwisho! Bila hivyo nyumba yangu niliyokuwa nimeiweka kama mortgage ingechukuliwa na kupigwa mnada na benki. Huyo ndugu alisema kabisa kama sio ile ndoto asingenilipia. Mara nyingi wachawi wamejaribu kunikaba usiku au kutupa wanyama wa ajabu ajabu nje ya nyumba lakini uchawi wao naupiga knock out.

Hizo ni faida za kibinafsi, lakini zipo pia za kijamii, yaani zilizowagusa watu wengine. Kuna mama mmoja alikuwa kila akijifungua anapata mtoto wa kike, na alitamani sana kupata na mtoto wa kiume. Nilimuombea akapata mtoto wa kiume. Kuna mama mmoja alipagawa na mapepo kwa kiwango cha kutaka kumrusha na kumtupa mtoto wake mchanga. Nilimuombea, mapepo yakamtoka. Yuko huru hadi leo.

Hizo ni baadhi tu ya baraka ambazo nimepata tangu nilipoanza kusoma na kuyafanyia kazi yaliyoandikwa katika Biblia.

Nyie mnaosusa kula pilau ya kiroho, inayopatikana katika Biblia, suseni tu, sie twala.

Maneno yako Mungu ni matamu sana kwangu; naam, ni matamu kuliko asali! (Zaburi 119:103)
Amen mtumishi wa Mungu. Bwana awe nawe siku zote za maisha yako.
 
Unanena kwa lugha au? what is teh teh....
Nimecheka kwa sababu unataka kuoa AI?😀
Kazana kupiga magoti BWANA akupe mke mwenye busara, anayefanana na wewe.
Mit 19:14
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
 
Seran & leo dada KAZI YENU NI NJEMA SANA
Mbarikiwe mjini na mashambani.
Ubarikiwe uzao wa matumbo yenu, na mazao ya nchi yenu na mifugo yenu.
Makapu yenu na vyombo vyenu vya kukandia vibarikiwe.
Mbarikiwe muingiapo na mtokapo.
Bwana asababishe adui wainukao dhidi yenu kushindwa mbele yenu. .
Bwana aagize baraka juu ya ghala zenu na juu ya kila kitu mtakachogusa kwa mikono yenu. Amen.

[Zaburi 28:1]
 
Seran & leo dada KAZI YENU NI NJEMA SANA
Mbarikiwe mjini na mashambani.
Ubarikiwe uzao wa matumbo yenu, na mazao ya nchi yenu na mifugo yenu.
Makapu yenu na vyombo vyenu vya kukandia vibarikiwe.
Mbarikiwe muingiapo na mtokapo.
Bwana asababishe adui wainukao dhidi yenu kushindwa mbele yenu. .
Bwana aagize baraka juu ya ghala zenu na juu ya kila kitu mtakachogusa kwa mikono yenu. Amen.

[Zaburi 28:1]
Amen sis 🙏🏽
 
Nimecheka kwa sababu unataka kuoa AI?😀
Kazana kupiga magoti BWANA akupe mke mwenye busara, anayefanana na wewe.
Mit 19:14
Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; Bali mke mwenye busara, mtu hupewa na BWANA.
Hakika......umenena vyema mtumish......
 
Back
Top Bottom