Nimeona gorikipa Goalkeeper Yakoub Suleiman akienda simba imenipa mwaswali magumu sana

Nimeona gorikipa Goalkeeper Yakoub Suleiman akienda simba imenipa mwaswali magumu sana

Iko hivi.

Huyo kipa anaweza kusaini kwa milioni 100 leo na mshahara milioni 10 kwa mkataba wa miaka miwili maybe.

Chakujiuliza mkataba wake utapoisha atapewa kiwango hicho hicho au zaidi?
Unaweza kutoa mamilioni ya pesa kwa mchezaji anayesugua benchi?

Nini matokeo ya kiwango cha mchezaji anayesugua benchi?
Hii tunaita kuingilia uhuru wa mtu na ni kosa kisheria.

Itapendeza zaidi tukiwa busy na maisha yetu.
 
Sijui niseme tatizo ni uongozi unaosimamia huyu kijana,

Au niseme ni tamaa ya fedha,

Au sijui dogo kapenda kwenda kwenye timu kubwa,

Sijui timu yenyewe ya JKT ndio hawajielewi.

Kiufupi huyu kijana kafanya makosa makubwa sana,
Tena haya makosa yamejirudia ndani ya mwaka huu rejea mkasa wa (Clementi mzize na Sulemani mwalimu).

Tunahitaji kweli wachezaji wakubwa katika ligi yetu ila kwa hawa vijana wanaoufanya ni utoto.

Yakoub Suleiman hakupaswa kuichezea Simba timu ambayo yeye akienda anaenda kuwa kipa namba 2. Maana Camara anaufalme wake pale msimbazi.

Huyu kijana anapaswa kwenda kwenye timu ambayo inauhaba na magolikipa na aingie kwenye kikosi cha kwanza sio benchi.

Nimeona kulikuwa na ofa nyingi kutoka nje ya nchi japo hazikuwa za timu kubwa.

Je nini kipi kinawakumba vijana wetu mpaka wanashindwa kufanya maamuzi sahihi?

Moyo wangu ulisononeka sana wakati MZIZE anafanya maamuzi ya kubaki YANGA. Kabla moyo wangu haujapoa huyu mjinga nae anaenda Simba, sijakaa sawa Sulemani nae anarudi nyumbani, Fei nae kawazimia simu KAIZER.


Itoshe kusema kuwa wachezaji wa TANZANIA akili hawana.
UJui kama kuna maisha baada ya mpira wewe unadhani hizo sifa ndo zitampa chakula akishastaafu kabumbu
 
Back
Top Bottom