Nimeona hapa ndo kuna shida kwa vijana wengi Tanzania

Hatari sana.

Kuna ndugu zangu fulani, kadhaa, na waliokuwa marafiki, kadhaa, nimewapoteza kwa sababu ya mikopo.

Yani unamkopesha mtu, halafu huo mkopo mdogo tu ndio unakuwa sababu anakomesha urafiki nawe, mwingine ndugu kabisa lakini kakopa, hataki kulipa, na anakukwepa kwa sababu ya mkopo. Kuna watu sijaongea nao sasa zaidi ya mwaka wa pili, kwa sababu ya mkopo mdogo tu.

Sasa hapo mtu anapata mtihani mgumu sana, mara nyingine naona bora niseme sina hela, ili mkopo usije kunikosesha ndugu, jamaa na marafiki.

Lakini mara nyingine, unaangalia mtu ana shida, unaona imani, unaamua ngoja nimpe tu, akinifanyia ubaya kutolipa ni ubaya wake yeye.
 
True
 
Mwachie Mungu atakulipa kwa wakati wake
 
Kuwa na roho safi ya kizungu kiduku lilo..... mungu atakuongezea msamehe kama unawsza msaidia msaidie kumbuka mtu mpaka afikirie jujidhalilisha kwako ina maana kaona una kitu special

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umefurahiii.

Watu wanaona usipoamini Mungu unakuwa mtu muovu.

Kumbe wengine tunakataa kuamini Mungu kwa sababu kuamini Mungu kunaweza kuruhusu kufanya maovu.
Mimi na wewe wote tupo kwenye boat 1...maono yetu kuhusu mungu yanafanana ...binafsi siamini pia katika uwepo wa mungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…