Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nahisi alikuwa upanga eastMaprosoo, jina kama linanijia hivi. Upanga kipindi sana, mpaka majina ya watu naanza kusahau.
Kuna mtu ananipaga pesa nyingi tu millions kadhaa.
Juzi nilikwama laki 4 nadaiwa.
Aiseeee ikabidi nimuingie anikopeshe.
Akanikopesha.
Lakini najua hiyo hela kwake hawezi nidai na ni hela upande wake ni ya kuspend ijumaa usiku, napengine haitoshi.
Lakini ni lazima nimlipe maana kanikopesha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Jolly pale California Dreamer Fanani aliwapuna mpaka wakampiga ban asije pale.Nahisi alikuwa upanga east
Jamaa alikuwa kiboko, Enzi za jolly akija akiwa mezani hana hata 100 lkn huo mkwala wake dah
Mwisho wa siku meza yote anaicontroll yeye
Ova
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu subiria dada wa kazi amalizie kutoa vyombo,ume muarakisha sana
Uchawi vipi mkuu??..upo au haupo??Umefurahiii.
Watu wanaona usipoamini Mungu unakuwa mtu muovu.
Kumbe wengine tunakataa kuamini Mungu kwa sababu kuamini Mungu kunaweza kuruhusu kufanya maovu.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Tatizo wachezeshaji kamali ukiwala sna lazima wakupige banJolly pale California Dreamer Fanani aliwapuna mpaka wakampiga ban asije pale.
Kuna mchezo fulani alikuwa amewashtukia kwenye kamali zao, kila akicheza anashinda yeye tu.
Wahindi wakampiga ban hatakiwi kutia mguu.
Uchawi ni nini?Uchawi vipi mkuu??..upo au haupo??
Nimeshindwa kujibu swali lakoUchawi ni nini?
Maana mtu anaweza kuweka Cyanide kwenye chakula, akaua, kwa sababu ya kemia, halafu akasema yeye mchawi kaua mtu kwa kumloga.
Sasa kabla ya kuniuliza kama uchawi upo, uchawi ni nini?
Na unajuaje huu ni uchawi na si trick tu ambayo sijaijua vizuri bado ambayo si uchawi?
Mtu akitoa kafara ni lazima afanikiwe?Nimeshindwa kujibu swali lako
Kafara je zipo??..yaani mtu kutoa kafara na kufanikiwa kwenye michongo yake..
Tumepata kusikia stori nyingi tu zikitamka neno kafara
Sina hakika
Kuna coincidence, lakini pia kuna saikolojia ya "placebo effect".Sina hakika
Vipi wanaofanikiwa kweli baada ya kufanya hivyo..it's just coincedence??
Mkuu ile link uliyoweka ya kuandika paper na research. Kuna vitu nilipitia kisha nikaja kusimulia kwa jamaa zangu wengi waliona teknolojia hizo kama uchawi kumbe nchi zilizoendelea wamefanya tafiti hizo.Kuna coincidence, lakini pia kuna saikolojia ya "placebo effect".
Watafiti wa afya wakifanya majaribio ya dawa mpya, mara nyingi huwa na kitu kinaitwa "control group". Yani inakuwa kama dawa mpya imepatikana, na wanataka kuifanyia test, kwa mfano kuna watu 1,000 walio na ugonjwa, kati ya hao 1,000, 800 wanaweza kupewa dawa, na 200 wengine wasipewe dawa, wanapewa vidonge tu, vimekaa kama dawa, havina tofauti na dawa ukiviangalia kwa macho.Hao 200 wanakuwa "control group". Hii control group inakuwa benchmark ya kupima tofauti kati ya mtu anayepewa dawa na asiyepewa dawa.
Halafu hao 1000 wote hawaambiwi nani kapewa dawa na nani hajapewa dawa.
Sasa inaonekana mara nyingi sana, katika wale 200 ambao hawajapewa dawa, lakini hawajaambiwa kwamba hawajapewa dawa, kuna wengine wanapona kwa saikolojia ya kuamini kwamba wamepewa dawa.
Hii inaitwa "placebo effect". Placebo - Wikipedia
Sasa, inawezekana kabisa, mtu akawa kikawaida hana nguvu za kupigana, hana juhudi za kutafuta pesa, hana juhudi za kusoma, lakini akifanya kitu kama kafara, akiomba Mungu, akiloga kwa wachawi, etc, vitu ambavyo physically havina effect yoyote kwake, ila kisaikolojia vinampa imani kwamba ana nguvu fulani zaidi yake yeye mwenyewe inamsaidia, na inawezekana kabisa kwamba imani hiyo ikamuhamasisha mpaka kile kitu alicholenga kikatokea.
Kwa hiyo, hapo unaweza kuona kwamba kafara inaweza kufanya kazi kisaikolojia kumpa mtu boost fulani au placebo effect fulani.
Lakini si kwamba ile kafara imesababisha vitu viwezekane kivingine vyovyote.
I've read my Claude Levi-Strauss, siwezi kukataa moja kwa moja tu kwamba kafara, laana, uchawi etc havifanyi kazi.
Tatizo ni muktadha.
Kuna muktadha wa kisaikolojia unahusika sana.
Unaweza kukuta timu ya mpira imevunja nazi uwanjani, wapinzani wameona nazi, wameogopa wakidhani uchawi.
Woga huo unasababisha wasicheze kwa kujiamini, wakiona wanashindwa kidogo tu, wanadhani uchawi unafanya kazi.
Mwishowe wanafungwa kwa woga, wanadhani wamefungwa kwa uchawi.
Anhaaaa!
Unao wangapi wanaokupaga hela?
[emoji1][emoji1787]