Nimeona Jiko kwa Wanyamwezi.

Nimeona Jiko kwa Wanyamwezi.

kakuruvi

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2009
Posts
770
Reaction score
258
Wadau kwa heshima na taadhima nawapa salamu!

Katika pitapita zangu nimeona Jiko linalonifaa kwa Wanyamwezi, tafadhali anayefahamu taratibu za kupata Jiko kwa Wanyamwezi anipe ujuzi ili nijitokeze kwao.

Natanguliza shukrani zangu za dhati!!!
 
We msome mwenyewe hakuna maelezo kamili ya kabila la mtu
 
muulize mwenyewe, au unataka kumsuprise mkuu!!!
 
Mnyamwezi yupi hasa?
1.mnyamwezi wa kuishi mamtoni
2.mnyamwezi kama kabila tz



vyovyote vile uamuzi unao wewe
 
WanaJf hakuna aliyepata jiko huko Tabora jamani? bado sijasaidiwa, please naendelea kutoa wito!
 
Taratibu muulize muhusika.

Ushauri acha ukabila

Mlimazunzu sijakupata, kwani kuna msichana asiye na kabila, ili ujue taratibu si lazima uulize taratibu za kabila lao? aidha kwa kabila hilo au wenye uhusiano na kabila hilo. sina ukabila Mwana ni kutaka kujua tu!
 
Tuma mshenga apeleke barua ya posa,wao watakujibu na kama itakuwa imekubaliwa utapewa mchanganuo wa vitu vinavyohitajika. Unaweza ukapeleka vitu ulivyoagizwa au pesa yenye thamani ya hivyo vitu. Wengi wao ni wakarimu sana.
 
Tuma mshenga apeleke barua ya posa,wao watakujibu na kama itakuwa imekubaliwa utapewa mchanganuo wa vitu vinavyohitajika. Unaweza ukapeleka vitu ulivyoagizwa au pesa yenye thamani ya hivyo vitu. Wengi wao ni wakarimu sana.

Ennie, hili nalifanyia kazi leo leo!
 
Wanyamwezi wanajua mapenzi sana nasikia, halafu wakarimu, halafu wanapenda mti na matunda yake

Halafu wanapenda mboga za majani, wanakuchanganyia na niaje kidogo kwenye mboga, unakua hubanduki home ha haaa ukitoka job hom au unaacha kabisa.
 
Back
Top Bottom