Nimeona video ya Mose Radio nikakumbuka Interview yangu

Nimeona video ya Mose Radio nikakumbuka Interview yangu

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Jana nilisoma humu juu ya kifo cha mwanamuziki wa Uganda, Mose Radio, kilichosababishwa na kupigwa na baunsa wa klabu.

Leo nimeiona video ya tukio. Mose anaonekana anapigizana kelele na mtu ambaye haonekani (sisikii vizuri nashindwa kuelewa anachomaanisha)

Mwana-jf mwenzetu amedai kisa ni ukorofi wa Mose mwenyewe.

Screenshot_2018-02-02-08-02-06.png


Kuna mwaka nilienda kwenye usaili, tulikua mabaunsa wanne (sitawataja majina). Interview ilifanywa kwa pamoja, yaani wote wanne tuliulizwa maswali kwa pamoja.

Wote tulionekana hatujui kiingereza hivyo alikuepo mfasiri, mchina akasema kitu, mfasiri akatugeukia "Mfano klabu kumetokea vurugu, mtu anarusha chupa utamfanya nini?"

Baunsa wa kwanza akajibu "Nitambana mbavu kwa mikono na kwenda kumtupa nje"
Alivyotafsriwa nikaona mchina anatabasamu

Wa pili akajibu "Nitampiga ili ajue kua hapa fujo si mahala pake"
Alivyotafsriwa nikaona mchina kamkazia macho jamaa

Mimi nilikua wa tatu nikajibu "Nitamshika mkono na kumvuta nje, nitamsihi aache vurugu akigoma nitaita polisi"
Alivyotafsriwa akamuangalia wa nne

Jamaa wa nne akasema "Nitambeba na kumtoa nje ya klabu na kuhakikisha harudi ndani"

Mtekelezaji wa tukio la Mose pengine hata hakufanyiwa usaili, waliona mwili tu wakaridhika huyu atafaa. Uwezekano mwingine ni kua angefanyiwa usaili na kuulizwa swali nililoulizwa mwaka ule jibu lake lingekua la yule baunsa wa pili.

Yaani kwao suluhisho ni mwili zaidi kuliko akili. Kazi ya mlinzi ni kuona na kuripoti tukio, siyo kupiga watu humo klabu.

Yawezekana Mose ni mkorofi lakini huyu angeweza kumbeba na kumtoa nje kama ana silaha hapa ndiyo kuripoti kunapoingia, unapiga simu polisi na kusema kuna mteja ana silaha.

Mnaomiliki klabu na bar kama mpo humu fanyeni hata usaili wa uongo na kweli utakufanya ujue huyu mlinzi wangu ana akili gani, msiache kufanya.

Video ya tukio ni hii hapa (Kwa hisani ya jamii forums)
 

Attachments

ASANTE
ngoja waje naimani watakuelewa ..ila hata mimi nilikuwa na mkubali mnoo marehemu but wakati wa kuishi duniani ulikuwa haumuhitaji tena. licha ya hao wenye bar kuja hapa na kujifnza namna ambavyo wanapaswa kumtreat mteja mkorofi ..lakini pia kuna chakujifnza toka kwetu as wateja ama binaadamu wakawaida kupitia shughuli zetu zakila siku
JAMANI MASIFA SIFA NA UGOMVI HAVINA MANTIKI KATIKA MAISHA YETU KWANZA UNAUTAJISBBISHIA KUWA MTU WAKUCHUKIWA NA WATU ..NA MWISHO WASIKU KUPIGWA KAMA HVYO NA KUJIPATIA MATATIZO NA MATATIZO YAKIJA HUWA HAWA YANAATHIRI MPKA WATU WAKO WNAKUZUNGUKA.
USIPENDE PENDE UGOMVI UKADHANI KUWA KILA BAUNSA AU KILA MTU ATAKUWA ANAELIMU YA NAMNA YA KUM TREAT MTU KAMA JINSI AMBAVYO ALIVYOWAKILISHA MTOA MADA
 
Duh ila ugomvi sio mzuri kwakweli na mda mwingine hata kuamulia ugomvi wa watu ni hatari unaweza utajikuta Upo dunia nyingine....
 
Kwahiyo Huyo baunsa Ana kesi ya kujibu?
kaua bila kukusudia

anaeza kujitetea alitukanwa akashndwa zuia hasira zake na ushahidi upo
sema ki tz tz jela haepuki sasa sijui huko kwao itakuaje
 
MAJINA YA KIBANTU TOKA KABILA LA WANYAKYUSA NA MAANA ZAKE.

1.LUSAKO. - BAHATI
2.LUSAJO. -BARAKA
3.LUGHANO. - UPENDO
4.LUTENGANO.- AMANI
5.LUSEKELO. - FURAHA
6.LUSUBILO. -TUMAINI
7.TUPOKIGWE-TUMEOKOLEWA
8.TUPOKE - TUOKOE
9.MPELI - MUUMBA
10.NTULI - MSAIDIZI
11.NTOLI - MSHINDI
12.MPOKI - MUOKOZI
13.KISSA - HURUMA
14.ULIMBOKA - NIOKOE
15.ANDINDILILE-AMENILINDA
16.ASUMILE - ALIOMBA
17.ANGANILE-AMENIPENDA
18.ATUGANILE - ALITUPENDA
19.ATUFIGWEGE -ASIFIWE
20.ANYISISILE - AMENIJIA
21.AFWILILE. - ALINIFIA
22.AHOBOKIILE - ALINISAMEHE
23.ASAJILE. - AMENIBARIKI
24.ANYOSISYE. AMENIBATIZA
25.ANYELWISYE. MENITAKASA 26.NDIMBUMI.
Nipo UZIMANI
27.NDIMBWELU-NIPO KWENYE NURU
28.ATUPELE - ALITUPA
29.TUMPALE. -TUMSIFU
30.NTUFYE. - MSIFU
31.GWAKISA- MWENYE HURUMA
32.GWAMAKA-MWENYENGUVU
33.GWANDUMI-MALAIKA
34.TUSEKILE-TUMEFURAHI
35.SEKELA -FURAHI
36.IPYANA. - HEKIMA
37.ATUPAKISYE.- ALITUJALI
38.USWEGE. - UNISAMEHE
39.ANDONGWISYE-AMENIONGOZA
40.AMBWENE. - AMENIONA
41.GWALUGANO. MWENYE UPNDO
42.MJE MASO
MUWE MACHO
43.NEGWAKO. - NI WAKO
44.ANDWELE - AMENILETA
45.ANDOBWISYE. AMENIVUSHA
46.TUSAJIGWE. TUMEBARIKIWA
47.LUTUFYO - SIFA
48.AMBILIKIILE. AMENISIKILIZA
49.AMBINDWILE. AMENIBADILI
50.AMBELE. - AMENIPA
51.AMANYISYE. AMENIFUNDISHA
52.AMULIKE. AMENIANGAZA
53.LUMULI - NURU
54.LUBATIKO UTALATIBU
55.SUBILAGA - TUMAINIA
56.ANGETILE. AMENITAZAMA
57.ANDONDILE AMENITAFUTA
58.ANGANILe -ANANIPENDA
59.ANGOLWISYE. AMENINYOSHA
60.ANDOGWISYE-AMENIONGOZA
61.NSAJIGWA - MBARIKIWA
62.NKUNDWE. - MPENDWA.

HAYA NI BAADHI YA MAJINA YA KINYAKYUSA NA MAANA YAKE, YA MAJINA HAYA YAMEBEBA SIFA NA UTUKUFU WA MUNGU,
PENDA MAJINA YA ASILI YAKO .hapa ni kyela
 
MAJINA YA KIBANTU TOKA KABILA LA WANYAKYUSA NA MAANA ZAKE.

1.LUSAKO. - BAHATI
2.LUSAJO. -BARAKA
3.LUGHANO. - UPENDO
4.LUTENGANO.- AMANI
5.LUSEKELO. - FURAHA
6.LUSUBILO. -TUMAINI
7.TUPOKIGWE-TUMEOKOLEWA
8.TUPOKE - TUOKOE
9.MPELI - MUUMBA
10.NTULI - MSAIDIZI
11.NTOLI - MSHINDI
12.MPOKI - MUOKOZI
13.KISSA - HURUMA
14.ULIMBOKA - NIOKOE
15.ANDINDILILE-AMENILINDA
16.ASUMILE - ALIOMBA
17.ANGANILE-AMENIPENDA
18.ATUGANILE - ALITUPENDA
19.ATUFIGWEGE -ASIFIWE
20.ANYISISILE - AMENIJIA
21.AFWILILE. - ALINIFIA
22.AHOBOKIILE - ALINISAMEHE
23.ASAJILE. - AMENIBARIKI
24.ANYOSISYE. AMENIBATIZA
25.ANYELWISYE. MENITAKASA 26.NDIMBUMI.
Nipo UZIMANI
27.NDIMBWELU-NIPO KWENYE NURU
28.ATUPELE - ALITUPA
29.TUMPALE. -TUMSIFU
30.NTUFYE. - MSIFU
31.GWAKISA- MWENYE HURUMA
32.GWAMAKA-MWENYENGUVU
33.GWANDUMI-MALAIKA
34.TUSEKILE-TUMEFURAHI
35.SEKELA -FURAHI
36.IPYANA. - HEKIMA
37.ATUPAKISYE.- ALITUJALI
38.USWEGE. - UNISAMEHE
39.ANDONGWISYE-AMENIONGOZA
40.AMBWENE. - AMENIONA
41.GWALUGANO. MWENYE UPNDO
42.MJE MASO
MUWE MACHO
43.NEGWAKO. - NI WAKO
44.ANDWELE - AMENILETA
45.ANDOBWISYE. AMENIVUSHA
46.TUSAJIGWE. TUMEBARIKIWA
47.LUTUFYO - SIFA
48.AMBILIKIILE. AMENISIKILIZA
49.AMBINDWILE. AMENIBADILI
50.AMBELE. - AMENIPA
51.AMANYISYE. AMENIFUNDISHA
52.AMULIKE. AMENIANGAZA
53.LUMULI - NURU
54.LUBATIKO UTALATIBU
55.SUBILAGA - TUMAINIA
56.ANGETILE. AMENITAZAMA
57.ANDONDILE AMENITAFUTA
58.ANGANILe -ANANIPENDA
59.ANGOLWISYE. AMENINYOSHA
60.ANDOGWISYE-AMENIONGOZA
61.NSAJIGWA - MBARIKIWA
62.NKUNDWE. - MPENDWA.

HAYA NI BAADHI YA MAJINA YA KINYAKYUSA NA MAANA YAKE, YA MAJINA HAYA YAMEBEBA SIFA NA UTUKUFU WA MUNGU,
PENDA MAJINA YA ASILI YAKO .hapa ni kyela
Sasa Ww Bujibuji haya majina yako ya kienyeji yana uhusiano gani na hii thread?
 
kaua bila kukusudia

anaeza kujitetea alitukanwa akashndwa zuia hasira zake na ushahidi upo
sema ki tz tz jela haepuki sasa sijui huko kwao itakuaje
Kutukanwa ni sababu ndogo sana, labda ajitetea kuwa jamaa alikuwa threat mke ndani, na bila kumdhibiti angeweza kuleta Madhara kwa wateja ikiwemo kuwaumiza!
 
Kutukanwa ni sababu ndogo sana, labda ajitetea kuwa jamaa alikuwa threat mke ndani, na bila kumdhibiti angeweza kuleta Madhara kwa wateja ikiwemo kuwaumiza!
kutukanwa ni sababu ndogo mitaani kwasababu matusi ni kawaida kwetu lkn sio mahakaman
mahakamani mtu anashnda kesi za mamilioni kwa sababu ya kipuuz tu
kama ushawahi kuhudhuria mahakaman utaelewa namaanisha nn
 
Kwahiyo Huyo baunsa Ana kesi ya kujibu?
Hata mi naona hivyo, na nilifikiri ilibidi awe chini ya uangalizi na kuachiwa kwake kutegemee hali ya mhanga wake. Ila nasikia hajakamatwa na hajulikani alipo.
 
kaua bila kukusudia

anaeza kujitetea alitukanwa akashndwa zuia hasira zake na ushahidi upo
sema ki tz tz jela haepuki sasa sijui huko kwao itakuaje
Ila aliendelea na kumpiga mateke, nafikiri kinga yake ya kutokukusudia inaishia pale alipombamiza chini kwakua Mhanga hakua threat tena si kivitendo au kuongea.
 
Back
Top Bottom