Castr
JF-Expert Member
- Apr 5, 2014
- 35,012
- 70,201
Jana nilisoma humu juu ya kifo cha mwanamuziki wa Uganda, Mose Radio, kilichosababishwa na kupigwa na baunsa wa klabu.
Leo nimeiona video ya tukio. Mose anaonekana anapigizana kelele na mtu ambaye haonekani (sisikii vizuri nashindwa kuelewa anachomaanisha)
Mwana-jf mwenzetu amedai kisa ni ukorofi wa Mose mwenyewe.
Kuna mwaka nilienda kwenye usaili, tulikua mabaunsa wanne (sitawataja majina). Interview ilifanywa kwa pamoja, yaani wote wanne tuliulizwa maswali kwa pamoja.
Wote tulionekana hatujui kiingereza hivyo alikuepo mfasiri, mchina akasema kitu, mfasiri akatugeukia "Mfano klabu kumetokea vurugu, mtu anarusha chupa utamfanya nini?"
Baunsa wa kwanza akajibu "Nitambana mbavu kwa mikono na kwenda kumtupa nje"
Alivyotafsriwa nikaona mchina anatabasamu
Wa pili akajibu "Nitampiga ili ajue kua hapa fujo si mahala pake"
Alivyotafsriwa nikaona mchina kamkazia macho jamaa
Mimi nilikua wa tatu nikajibu "Nitamshika mkono na kumvuta nje, nitamsihi aache vurugu akigoma nitaita polisi"
Alivyotafsriwa akamuangalia wa nne
Jamaa wa nne akasema "Nitambeba na kumtoa nje ya klabu na kuhakikisha harudi ndani"
Mtekelezaji wa tukio la Mose pengine hata hakufanyiwa usaili, waliona mwili tu wakaridhika huyu atafaa. Uwezekano mwingine ni kua angefanyiwa usaili na kuulizwa swali nililoulizwa mwaka ule jibu lake lingekua la yule baunsa wa pili.
Yaani kwao suluhisho ni mwili zaidi kuliko akili. Kazi ya mlinzi ni kuona na kuripoti tukio, siyo kupiga watu humo klabu.
Yawezekana Mose ni mkorofi lakini huyu angeweza kumbeba na kumtoa nje kama ana silaha hapa ndiyo kuripoti kunapoingia, unapiga simu polisi na kusema kuna mteja ana silaha.
Mnaomiliki klabu na bar kama mpo humu fanyeni hata usaili wa uongo na kweli utakufanya ujue huyu mlinzi wangu ana akili gani, msiache kufanya.
Video ya tukio ni hii hapa (Kwa hisani ya jamii forums)