Nimeona video ya Mose Radio nikakumbuka Interview yangu

Nimeona video ya Mose Radio nikakumbuka Interview yangu

kaua bila kukusudia

anaeza kujitetea alitukanwa akashndwa zuia hasira zake na ushahidi upo
sema ki tz tz jela haepuki sasa sijui huko kwao itakuaje
Ndo umnyanyue MTU kama mpo kwenye wwe.?
sio fair kabisa.
 
Jana nilisoma humu juu ya kifo cha mwanamuziki wa Uganda, Mose Radio, kilichosababishwa na kupigwa na baunsa wa klabu.

Leo nimeiona video ya tukio. Mose anaonekana anapigizana kelele na mtu ambaye haonekani (sijui kiganda nashindwa kuelewa anachomaanisha)

Mwana-jf mwenzetu amedai kisa ni ukorofi wa Mose mwenyewe.

View attachment 689132

Kuna mwaka nilienda kwenye usaili, tulikua mabaunsa wanne (sitawataja majina). Interview ilifanywa kwa pamoja, yaani wote wanne tuliulizwa maswali kwa pamoja.

Wote tulionekana hatujui kiingereza hivyo alikuepo mfasiri, mchina akasema kitu, mfasiri akatugeukia "Mfano klabu kumetokea vurugu, mtu anarusha chupa utamfanya nini?"

Baunsa wa kwanza akajibu "Nitambana mbavu kwa mikono na kwenda kumtupa nje"
Alivyotafsriwa nikaona mchina anatabasamu

Wa pili akajibu "Nitampiga ili ajue kua hapa fujo si mahala pake"
Alivyotafsriwa nikaona mchina kamkazia macho jamaa

Mimi nilikua wa tatu nikajibu "Nitamshika mkono na kumvuta nje, nitamsihi aache vurugu akigoma nitaita polisi"
Alivyotafsriwa akamuangalia wa nne

Jamaa wa nne akasema "Nitambeba na kumtoa nje ya klabu na kuhakikisha harudi ndani"

Mtekelezaji wa tukio la Mose pengine hata hakufanyiwa usaili, waliona mwili tu wakaridhika huyu atafaa. Uwezekano mwingine ni kua angefanyiwa usaili na kuulizwa swali nililoulizwa mwaka ule jibu lake lingekua la yule baunsa wa pili.

Yaani kwao suluhisho ni mwili zaidi kuliko akili. Kazi ya mlinzi ni kuona na kuripoti tukio, siyo kupiga watu humo klabu.

Yawezekana Mose ni mkorofi lakini huyu angeweza kumbeba na kumtoa nje kama ana silaha hapa ndiyo kuripoti kunapoingia, unapiga simu polisi na kusema kuna mteja ana silaha.

Mnaomiliki klabu na bar kama mpo humu fanyeni hata usaili wa uongo na kweli utakufanya ujue huyu mlinzi wangu ana akili gani, msiache kufanya.

Video ya tukio ni hii hapa (Kwa hisani ya jamii forums)
Ebana eeh...nouma sana. Ukorofi sio kabisa...watu wanasahau baunsa kukaa mlangoni kulinda watu wanakula bata...wanafanya kujitafutia riziki...so hata wao wangependa kula bata zito....sasa ukimkwaza unakuwa unatonesha mengi. Anyway, we should learn and behave accordingly...respect ni muhimu sana.
 
Ila mlinzi inabidi uwe na kujielewa kwakua unakua haujalewa, unaweza kuprocess situation kwa ufasaha kuliko mteja ambaye kashalewa na anafanya nusu na robo ya vitu kwa ajili ya kuwaimpress wenzie.
 
Sijui hao waliokuwa wana shabikia sasa wanajisikiaje? Alimnyanyua kama mtoto wake, inaumiza!
 
Ila mlinzi inabidi uwe na kujielewa kwakua unakua haujalewa, unaweza kuprocess situation kwa ufasaha kuliko mteja ambaye kashalewa na anafanya nusu na robo ya vitu kwa ajili ya kuwaimpress wenzie.
Sawa mkuu...but kumbuka watu tumetofautiana uchukuliaji wa mambo....+ ugomvi ni historia ya mshkaji.....so inakuwa kama...now this is too much "ngoja tumuoneshe".
 
baunsa alikuwa ana uwezo wa kumtoa tu nje ukizingatia jamaa alikuwa kanywa pombe na sio maji.
 
Sawa mkuu...but kumbuka watu tumetofautiana uchukuliaji wa mambo....+ ugomvi ni historia ya mshkaji.....so inakuwa kama...now this is too much "ngoja tumuoneshe".
Hilo nalo ni kweli pengine jamaa aliona hivyo. Ila ndiyo haiwezi kua utetezi wake kama akifikishwa mahakamani
 
Back
Top Bottom