Amani iwe nanyi watumishi wa MUNGU
Katika kufunga Kuna faida zake
Huenda ukaendelea kufunga na ukaendelea kubaki masikin sana usiye na tumaini wala rafiki wa kweli, wala msaada wala mfadhili
Usiye na cheo wala uchumi wa kueleweka
Lakini BWANA huendelea kukaa pemben yako daima , huendelea kukupenda na kukushika na kujua thamani yako siku hata siku
Hivyo tusife moyo wala usife moyo mtumish
Katika faida za kufunga mara kwa mara BWANA huniinulia maono ya kila namna mazuri kwa mabaya lakin yote ni maono
Mengine ya watu ninaojuana nao,mengine ya jamii furani mengine ya watu fulani
Kuna ndoto imekuwa ikinitesa sana siku nyingi nayo ni maono ambayo BWANA alinifunulia
Nilimuona papa Francisco wa Roma akiwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi, na hapo kwenye kiti chake palikuwa na ROHO wa paka ambaye alikuwa amekaa juu Papa Francis
Paka huyo alionekana kufanya utawala mkubwa katika kiti hicho na kuchukua nafasi kubwa kuliko hata papa mwenyewe, nilishangaa sana
Ni maono niliyoyaona Mimi mtumish nikiwa nimefunga katika ekarist takatifu
Ngoja tuendelee kumungoja BWANA tuone atafanyia nini zaidi
Ikumbukwe Mimi pia ni mkatoliki
Asante sana
SAYUNI BOY