Mwanafalsafa
Platinum Member
- Jun 24, 2007
- 673
- 865
Alikuteka wewe?Ufanikiwe kumsifia mtekaji?!
Au kuna mtu ulimuona akimteka?
Fuatilia habari ya bomba la mafuta ya Uganda linavyopigwa vita na mabeberu, ilhali ubeberuni mabomba mapya ya mafuta yanajengwa. Ila huku Afrika ndo likijengwa bomba la mafuta inaonekana ni uchafuzi wa mazingira. Sasa anasimama mtu kisa tu yeye ameshajiita ni mpinzani anapayukapayuka kukosoa au kudhihika au kukanusha kuwa hakuna vita ya uchumi duniani. Binafsi ningekuwa Rais wapumbavu kama hao wanaopayukapayuka kuyumbisha tu wananchi na kuwapindikizia chuki zisizo na msingi kuhusu serikali yao ningewanyamazisha kwa kweli.
Mmepewa uhuru wa kuongea, kautumieni vizuri. Kamsifieni Magufuli ili nchi irudi katika mstari. Mstari wa ukali, na mstari wa watumishi wa umma na viongozi wa kisiasa kubanwa waache ujinga ujinga, wizi na uzembe. Maana tunakoelekea sasa hivi hapaeleweki.