Nimepanga kwenda kuishi Msituni/Porini sana

Hizo ni stress za kukutana na uliopiga nao kitabu mjini wapo levo nyingine. Sasa hiyo kitaalamu inaitwa kujicoumoflage kwa kukaa na nyani ambao hawatakuuliza β€œSasa hivi upo wapi” kila ukipishana nao
πŸ˜€πŸ˜πŸ˜‚πŸ€£
 
Mimi nami nina mpango wa kuhamia porini,kijijini.

Mnapajua Chato?Kila siku watu walikuwa hawaishi kupaponda kwasababu jiwe alisababisha wapaponde.

Basi bwana,kule kuna maeneo poa sana na soon ninahamia kule.Kwanza 90% ya Chato imezungukwa na Ziwa Victoria, na mimi nimejenga nyumba yangu kule kandokando ya ziwa Victoria.Kuna misitu mizuri,hewa safi na ardhi nzuri kwa kilimo.

Nyumba yangu haiko mbali sana na hifadhi nzuri za Rubondo na Burigi/Biharamulo kwa namna fulani. I love nature vibaya mno.

Mwendazake keshaenda sasa tuzungumzie positively fursa zilizoko huku.
 
Kila la kheri mkuu ..
 
Mzazi maisha ya wazungu Kuishi porini yasikudanganye nakwambia wale hata wakipatwa na tatizo chopa hii hapa .sasa wewe nenda ukaishi porini uone show ilivyo ya kibabe unaweza kujikuta unaingia himaya ya wachawi
Mapori yetu sio rafiki kabisa,nakushauri nenda ukaishi kijijini na sio porini
 
moja ya changamoto kubwa sana ya kujitenga na kuishi peke yako mbali na jamii ni usalama (vyote mali na wewe) nilitaka kutumia neno ukiingiliwa lakini ngoja nitumie ukivamiwa, hakuna msaada wa haraka. lazima ujipange sana kwenye hili na usilipuuze. Mguu wa kuku lazima uwe nao kiunoni 24/7.
 
Mwamba big up Mimi na wewe tupo sawa ki idea halafu Tena maeneo yale Yale aisee Njombe ni sehemu moja amaizing sana Kama unataka uishi maisha Kama hayo yaani unatengeneza bustani yako saaaaafi kabisaaa Kama paradiso flani hivi amaizing
Yaaaa I get you nigga, keep big up meeen You know!
(in Lemutuz voices)
πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜‚
 
Asisahau na solar power hata ya 200W inatosha sana.
 
Wako baadhi watakuona wa ajabu kuishi porini, hususani mkoa wa dar waliozoea kwenda sehemu za starehe, madisco, cinema, vilabu n.k.. hawa viumbe hata uwaambie nini hawatakuelewa.. ..hakuna life nzuri kama porini, especially napenda sana.. ..ukilala utasikia sauti za wanyamaπŸ¦ŒπŸ¦ŒπŸ¦“πŸƒπŸ‚πŸ„πŸπŸΈ, ukiamka asubuhi utasikia sauti za ndege wa aina tofautiπŸ¦ƒπŸ”πŸ“πŸ£πŸ€πŸ¦πŸ•ŠπŸ¦…πŸ¦†πŸ¦’πŸ¦‰πŸ¦œπŸ’.. ..raha sana πŸ˜ƒ



πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ‡¦πŸ‡·πŸ”₯πŸ”₯
 
Mwenzio huyo hapo alishawahi huko msituni....
 
Binafsi nafikiria kuhamia Rungwe, Lushoto au Mufindi ila sitokaa msituni napendelea kuishi eneo lililo pembezoni kidogo ya miji. Nilienda kufanya utafiti maeneo haya nimepapenda zaidi Brooke Bond - Mufindi na eneo jirani na Daraja la Mungu, KK - Rungwe. Ni maeneo yenye mandhari nzuri ya asilia.

Mfano mzuri ni kama Swiss farm cottage Lushoto.













 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…