Nimepata ajira wife ameongeza matumizi ya pesa zaidi ya mara mbili

Nimepata ajira wife ameongeza matumizi ya pesa zaidi ya mara mbili

Mkuu gharama za maisha zimepanda.

1. Mchicha ulikuwa fungu 1 TSH Mia 2 sasahivi Ni buku

2. Mafuta ya kula Lita ilikuwa Elfu 3 sasahivi Lita Tshs elfu 5

Bado Nyanya ,vitunguu na viungo vingine mkuu Hana matumizi mabaya Bali gharama za maisha zimepanda sana
 
Kama hununui vitu in bulk aisee utamlaumu bure. Hakikisha unanunua chakula kingi,mafuta,sukari na vingine ambavyo havihitaji kutoa hela mfukoni. Na ikiwezekana awe anakuwekea orodha ya vitu unanunua kwa wiki hapo hata elfu 2 kwa siku inatoboa. Muulize pia anamadeni uyalipe huenda pindi mambo hayajakaa sawa alikua anakopa kusupport au kaingia kwenye michezo ile ya vikundi vya wamama daily wanatoana.

Na pia mpe hela mara mojamoja afanyie mambo yake maana lazima kuna vitu alivikosa hasa nguo na vitu vingine vya wanawake na watoto kama unao....anahaki ya ku-upgrade kidogo na kama hujamuweka kwenye bajeti ata-upgrade kwa kuchakachua bajeti.

Mwisho muanzishie kibiashara hata kidogo atajichakachua humohumo
 
Back
Top Bottom