Huruma siyo malezi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2020
- 1,433
- 3,210
Serikali mtavunja ndoa za watu badlikeni
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
hongeraMiaka 10 sasa
Kama hununui vitu in bulk aisee utamlaumu bure. Hakikisha unanunua chakula kingi,mafuta,sukari na vingine ambavyo havihitaji kutoa hela mfukoni. Na ikiwezekana awe anakuwekea orodha ya vitu unanunua kwa wiki hapo hata elfu 2 kwa siku inatoboa. Muulize pia anamadeni uyalipe huenda pindi mambo hayajakaa sawa alikua anakopa kusupport au kaingia kwenye michezo ile ya vikundi vya wamama daily wanatoana. Na pia mpe hela mara mojamoja afanyie mambo yake maana lazima kuna vitu alivikosa hasa nguo na vitu vingine vya wanawake na watoto kama unao....anahaki ya ku-upgrade kidogo na kama hujamuweka kwenye bajeti ata-upgrade kwa kuchakachua bajeti.
Mwisho muanzishie kibiashara hata kidogo atajichakachua humohumo
Mama D issue siyo ubahili shida bado hatujajenga tunaishi kwenye nyumba ya kupanga.
Laki 1 kwa wiki haitoshi? Twende pole pole, hiyo laki kwa wiki ni baada ya kuhakikisha kila kinachohitajika kipo au laki ndo kila kitu kipatikane hapo? Maji, unga, mchele, chumvi, mafuta ya kupikia, sukari, majani ya chai, mboga, mkaa, n.k?
Kaeni mjue gharama za vitu kwa mwezi, umeme, king'amuzi, matumizi yake binafsi, gesi, gunia la mkaa, nunua nyama, samaki, maharage, sukari, sabuni ya kufulia, kuoshea vyombo, kuogea, majani ya chai, unga wa ugali, nauli, n.k kisha mkabidhi fungu hilo, mkabidhi na sh 5,000 ya kila siku, baada ya hapi msijuane!
Akitaka pesa zaidi ya hapo, apeleke maombi Dawati la jinsia, utampea kule.
Sijajua unapoushi wewe lakini kama ni familia changa ya watu wawili mfano Morogoro : Mchicha fungu la haja Mia tano fungu mbili buku. Nyama nusu kilo 3500, vitunguu fungu la maana Mia tano, nyanya mia tano, mafuta lita elfu 4 lakini hununui kila siku, mchele kilo elfu moja Mia mbili mpaka Mia nne. Kiukweli elfu 10 ilitakiwa iwe inatosha kabisa. Ushauri wangu ni huu ukipata salary nunua vitu vya jumla vifuatavyo: mchele nenda mashine za kukoboa nunua 50kgs, unga nunua kufuko cha 25kgs, mafuta ya kupika lita tano, ngano ya Azam 5kgs, sukari, chumvi, nazi za pakiti, vitunguu, maharage, dagaa etc... Baada ya hapo mpe pesa kwa matumizi yake binafsi kulingana na kipato chako, na pia pesa ya matumizi madogo ya ndani kama nyama, nyanya etc... Mwisho kaa naye mkubaliane nini malengo yenu kwa huo mwaka na miaka mitano ijayo? Mfano kuanzia Mwaka huu tuanze kufanya serving kwa ajili ya kununua gari au kiwanja au kupata mtoto ili aone umuhimu wa serving na kubana matumizi. Asante.Mkuu gharama za maisha zimepanda.
1.mchicha ulikuwa fungu 1 TSH Mia 2 sasahivi Ni buku
2. Mafuta ya kula Lita ilikuwa Elfu 3 sasahivi Lita Tshs elfu 5
Bado Nyanya ,vitunguu na viungo vingine mkuu Hana matumizi mwbaya Bali gharama za maisha zimepanda sana
Na yeye ni mtumishi?Nashukuru sana mkuu shida nafanyia kazi mbali na yeye kwa hiyo kidogo ni Changamoto
Sasa wakiendekeza kutumia laki moja ndani ya siku tatu wataweza kweli kujijenga au kuanzisha biashara? Je kazi ikiisha kama ni ya mkataba au matatizo yoyote?Miaka2 sio sasa. Umeskia bei ya mafuta ña vyakula ilivyopanda?
Halafu wewe unaweza kuwa mwanaume bahili hadi kwa mkeo kweli!?
[emoji1666][emoji1666][emoji1666] Umemaliza kila kitu...Siyo kosa mkeo kujua unachopata, ila hichokinachopatikana kama hakina mwelekeo wa kuinvest au kuwa na long/short term planning........lazima iwe ivyo.....ila angekuwa anajua tunafanya jambo fulani angekuwa na disipilini
Sasa wakiendekeza kutumia laki moja ndani ya siku tatu wataweza kweli kujijenga au kuanzisha biashara? Je kazi ikiisha kama ni ya mkataba au matatizo yoyote?
Maisha ni uchaguzi, japo maisha yamepanda kiasi lakini usipijidhibiti utaishia matumizi ya kawaida tu, mkazie weka budget ya familia mkabidhi yeye na ziada, then wewe weka emergency tu, zingine peleka kwenye mambo ya msingi, mfano program za kiwanja kama huna,, kesho ni muhimu kuiangalia zaidi ya leoHabarini wapendwa, nimeona watu kadhaa wamekuwa waki share kadhia anuai katika jamvi hili na ushauri mzuri umekuwa ukitolewa ambao nadhani umekuwa msaada kwao.
Moja kwa moja kwenye point. Mimi na wife tunaishi kwenye ndoa, namshukuru Mungu so far tunaishi vizuri sana. Leo nimeona nishare hili na watu wenye experience wanisaidie kwa ushauri na hekima zao.
Ni miaka miwili sasa tangu nimeoana na mke wangu na wakati tunaoana sikuwa na kazi japo nilikuwa na kibiashara kidogo. Kwa karibu mwaka mmoja wife alikuwa na nidhamu sana ya matumizi ya pesa, yaani elfu tano ilikuwa inatosha kabisa matumizi ya ndani kwa siku.
Cha ajabu baada ya kuwa nimepata ajira na thanks be to God mshahara wangu ni mtamu, wife amezidisha matumizi sana. Yaani tofauti na mwanzoni, kwa sasa elfu kumi haitoboi kwa siku. Imefika wakati laki moja week haiishi, mwanzoni nilimshauri akakubaliana vema, lakini cha ajabu mabadiliko yalikuwa kidogo sana na niliporudia tena kumwambia kuhusu kupunguza matumizi ili tubane matumizi kwa ajili ya future yetu anakuwa mkali na anaona namunyanyasa baada ya kuwa nimepata ajira.
Naomba kwa haya machache, wenye ushauri na uzoefu wa ndoa munisaidie namna ya kufanya.
Asanteni sana
“Aquila non capit muscas”
Sio kila mbuz atakula kwa urefu wa kamba yake wengine hula kwa huruma ya mchungaj wake, wanawake wanajsahau mapema sana kama mlkua kwenye msoto ukipata Chanel anabadlka mpka unajiulza huyu kawaje na kama ulkua na pesa zkapata naul au kaz ikaisha utamwona visa vyake kila kukicha na mabeg yake mgongon kama ngoni migration Leo kwa Dada ake kesho kwao hatulii tena hata ukiongea hakuelew wala kukuskia kikubwa Mungu atupganie tu watoto wa kiume sisKila mbuzi hula kulingana na urefu wa kamba yake....kama anaujua hadi mshahara wako unategemea afanye nini? We mpe tu kama kujenga atajenga kwao