Kingine mtoa mada,
Mwanaume hutakiwi kabisa kukaa kuipigia hesabu Ela ya MKE wako.
Kwa Bahat mbaya mm sijaoa MKE mfanyakazi,
ila laiti ningekua na mke mfanyakaz basi ingenisaidia kupunguza mzigo wa request za pesa zinazotoka kwenda ukweni. (Aisee Napasuka balaa uko ukweni)
Vitu vingine vidg vidg najua Ela ya wife ingesolve Moja kwa Moja uko ukweni, pamoja na mahitaji yake binafs madogo madogo.
Sisi Wanaume tuliooa mama wa nyumbani huwa always tunapasuka sio chini ya Mara tatu.
-ukweni,
-kwetu tulikozaliwa,
-kwenye familia yangu.
-hapo ujaongeza na kwenye michepuko,bar n.k
Ila hatulalamiki Wala kuuliza Ela ya wife imefanya nini, Tunapambana tu kiume kutekeleza wajibu wetu.
Kwaiyo mkuu,
Hebu acha kabisa kuipigia hesabu Ela ya mkeo, hujaoa ili kutafuta unafuu wa maisha. UTASABABISHA MIGOGORO
Usitake kugeuza ndoa Kama daraja la kupunguzia makali ya maisha, Tekeleza wajibu wako. Ikishindikana mshirikishe mwenzio mwende pamoja.
Hatma ya familia yako iko katika uchumi wako
Kama Mwanaume Tekeleza wajibu wako ipasavyo,
Achana na tabia ya kumbebesha mdada wa watu majukum ya kiume.
Mwisho wa siku atapungukiwa na nguvu za kike kesho uje Tena hapa kulaumu unanyimwa penzi au mkeo Ni mvivu kitandani, maana unamchosha Sana kiukweli
Sent using
Jamii Forums mobile app