#COVID19 Nimepata Chanjo ya Corona nchini Marekani, puuzeni uzushi

Wewe hujui chochote Tz maana upo Marekani na hajawahi ingia maabara yoyote ya Tz ili kujua kuna Corona gani.Wewe usutufananishe Waafrika na Wamarekani maana wao mfumo wao wa maisha haufanani na wetu.huko mnakula Bisi mnalala huku wali maharage, kwetu jua kali kwenu mnalichungulia .Acha upuuzi Mtu mweusi hana undugu na mzungu.
 

Hebu angalia bega lako kama huna chanjo😂. Usidanganye na rangi yako kijana Afya sio rangi . Tofauti ya aina ya damu kiafya ni kitu kikubwa kuliko hata rangi kama una type A haijali rangi! Hivi hizi shule za kata zinatutolea vijana wa type gani siku hizi!
 
Si mbaya kujulishana WAPENDWA. Kwa aliepitia hii chanjo anajisikiaje?

Na ikoje, unachomwa sindano ama?

Wengine tukisikia tutashawishika kusisitiza ifanyiwe haraka kuja nchini mwetu.
 
Unachomwa sindano, binafsi kwa masaa kama nane baada ya kuchomwa mkono uliuma na kuwa mzito. Baada ya hapo sikuhisi chochote. Nimemaliza sindano zote mbili tangu mwezi wa March mwaka huu.
Congratulations dia aina gani hioo inabidi ukatoe na sadaka kanisan MAANA ninavyoziwaza loh
 
Can I get Covid after being fully vaccinated?
The U.S. Centers for Disease Control and Prevention also continues to recommend vaccinated people with symptoms get tested for COVID. Cases of fully vaccinated individuals contracting coronavirus are rare, but possible
 
Si mbaya kujulishana WAPENDWA. Kwa aliepitia hii chanjo anajisikiaje?

Na ikoje, unachomwa sindano ama?

Wengine tukisikia tutashawishika kusisitiza ifanyiwe haraka kuja nchini mwetu.
Akili kubwa 👍
Nilidungwa ya kwanza 03/2021 na ya pili 04/2021.

Ukishadungwa unawekwa checkpoint ukae kwa dakika 15 kuangalia kama una adverse reaction.

Ukipita hizo dakika 15, unapotea zako.

Next day maumivu yana kuja kwenye mkono uliodungwa, kwa mimi hii ni kawaida sababu nikisafiri lazima nikamilishe yellow card(kadi ya chanjo) kwenda dunia ya tatu,

kwahiyo haya maumivu ni kitu cha kawaida kwa yeyeto aliewahi kupitia chanjo hizi. Pitia mtu anaitwa David Attenborough, huyu inasemekana anarekodi ya dunia yakuchanjwa🤣(joking).

Binafsi sijaona mabadiliko yeyeto ya kiafya baada ya chanjo lakini mke wangu anasema;
"Pfizer did it again" kama Via......a
 
Kwasasa binaadamu hatuna tofauti na kuku wa kizungu (Broiler), kila kukicha ni kudungana machanjo kwenda mbele. Yani "Mguu upande, Mguu sawa, Kaburini elekea", muda wowote.

Maradhi kila kukicha yanazuka mapya, mpaka utamu wa maisha umekwisha. Tofauti na maisha ya enzi za mababu zetu ambao hata ukimwi kulikua hakuna.

Siku hizi ukimwi ukikukosa, kuna Hepatitis, na yenyewe ikikukosa basi kuna homa ya manjano, ukikoswa na homa ya manjano kuna Covid inakuwinda kwa spidi ya 4G.

Tunaishi kama nyani porini, kila kukicha ni kukwepa mishale kwenda mbele. Yani tafrani tupu walahi.
 
Mimi nilichomwa vaccine ya MODERNA ; hakuna matatizo kabisa . In fact vaccine ya SHINGLES inauma zaidi kuliko ile ya COVID!!!
 
Akili kubwa 👍
Nilidungwa ya kwanza 03/2021 na ya pili 04/2021
Ukishadungwa unawekwa checkpoint ukae kwa dakika 15 kuangalia kama una adverse reaction...
Mkuu nimeelewa sahihi? Kuwa ukisafiri lazima upate chanjo ya manjano, una maana kila ukisafiri unaenda kuchomwa chanjo ya "manjano"?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…