Nimepata kazi ambayo inaniruhusu kuhamia USA nikitaka, lakini mshahara ni ule ule popote nitakapoamua kufanyia kazi

Kwanza hongera Kwa kuwa na OPTIONS ambazo wengi tunaona kama ni BAHATI NASIBU!
Baki hapa mkuu, hiyo hela kule ni ndogo mno mno mno..
Hapa utafanya mambo makubwa na ya maana kuliko kule..
Mwisho wa siku wewe ndio muamuzi..
All the best 🙏👏👏👏👏👏
 
Typing........[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu kama una watoto na unataka kufanya kitu kwa ajili yao nenda nao USA.
But kama hauna watoto baki Tz twanga maisha.
Kwa nini nasema hivyo;
Kama watoto wako wapo vizuri kichwan, wakiwa USA wanaweza soma bure maisha yao yote ya elimu bila wewe kutoa hata $1.
So kama unakwenda USA nenda kwa lengo la kuwapeleka watoto wako. Ili wasije kuwa chawa wa mtu.
But kama hauna watoto fanya maendeleo hapa hapa TZ.
 
Sio hilo mkuu, ila linafanana na hilo kwa maana ni upande wa afya, lakini wenyewe wana miradi ya mama na mtoto sana sana.
Okay mimi nakushauri uende kama una mpango wa kuishi Marekani hiyo bonge ya opportunity na huwezi pata tena! Utapata permanent residency kirahisi na hata uraia ukipenda. Kumbuka kazi hizi za mashirika zaweza kuisha muda wowote basi kama ukienda Marekani na baada ya muda kazi/mkataba ukaisha utabaki na permanent residency ambayo hiyo tu watu wanahemea kwa maisha yao yote bila mafanikio.
 
Akazae watoto huko huko na kufanya hayo yote.
 
Umepigwa au unakaribia kupigwa! Hakuna cha ajira wala mjomba wake ajira! Shtuka!
 

Bongo na America kuna tofauti gani mkuu? Kunya hata kule unakunya, unachokula hapa na kule ni hicho hicho, hali ya hewa ya huku ni nzuri kuliko kule, kule waafrika wanauawa kinyama dhidi ya magaidi!

Ni heri ukaishi North Afrika au Gulf countries
 
Narudia tena hakuna Shirika utafanya kazi Vietnam ulipwe mshahara wa Tanzania hata kama mkataba mtafanya mkiwa Tanzania nasema hakuna pili swala la kufanya kazi sehemu yeyote inawezekana ila sio kwa vipengele hivyo...
 
Hapana mkuu, hawa ni genuine kabisa 100%, hakuna utapeli.
Haya. Yatakayojiri usisite kutupa mrejesho maana wameshateka akili yako.

Red flags: Hakuna mwajiri (kampuni) ambayo inatoa mshahara bila kujali mazingira. gharama za maisha za Tanzania siyo sawa na Marekani. Pili Tangazo la kazi lazima liseme kituo cha kazi kitakuwa wapi.

WHEN THE DEAL IS TOO GOOD, THINK TWICE.
 
Naona naysayers wamekua wengi sana.
Anyways, ni sawa pia kwa sababu ni sahihi watu kuwa na wasiwasi, wanasema wasiwasi ndio akili.
Hii nafasi ilikua ni global, yaani ililua mtu kutoka sehemu yoyote ile ya dunia anaweza ku apply, hivyo kwenye interviews nilishindana na watu kutoka nchi mbalimbali. I did like 5 rounds of interviews. Kwenye tangazo la kazi, location ilionyesha kuwa preferred locations ni zile nchi za Africa ambazo mradi husika unatekelezwa.
Baada ya kupita rounds zote interviews kwenye dicussions kabla ya kusaini mkataba ndio zimekuja hizo options; Wao kama wao hawana shida nikifanyia kazi hata huku huku Tz, lakini in case nikitaka kuhamia USA, ndo hiyo nafasi ipo na wata sponsor H-1B VISA kuwezesha hilo, lakini benefits zinabaki zile zile tu. Hakuna ongezeko kwa sababu ishu ya kuhamia USA ni uchaguzi wangu sio requirement ya kazi yao, I can work from here and still deliver perfectly bila shida.
Pia, kitu kingine ni kwamba, naweza pia nikabaki hapa bongo lakini nisiwe employer wao, ila nikafanya nao kazi nikiwa kama consultant, na nikawa napata the same benefits, ila hapo nakua tu consultant.
 
Hakuna kitu kibaya kama dilema katika kufanya uamuzi / indecision. Usd 7k kwa kule ni pesa ndogo kama wadau wanavyosema kuna bills kibao za lazima
Unaenda kuishi maisha tofauti ya upweke wewe na familia yako. Yani kule ukienda ni kazi kazi kazi juu ya kazi
Mke nae atafutiwe kazi ili muweze kupay bills na kusave

Ila kibongo bongo iyo pesa utaienjoy sana na utawekeza na kunufaika zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…