Nimepata maumivu makali mno baada ya Ufaransa kushindwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la dunia 2022

Nimepata maumivu makali mno baada ya Ufaransa kushindwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la dunia 2022

Mmehuzunika france kukosa kombe au Messi kutwaa kombe?
 
Mmehuzunika france kukosa kombe au Messi kutwaa kombe?
Shida kubwa ni messi kutwaa kombe, now zile thread zao za mess vs ronaldo zitakua hazina mashiko tena
 
Nachukizwa na kushabikia timu sababu ya rangi, ndo mana nimefurahi France kupigwa
 
Yaani nashindwa nielezee vipi ili nieleweke.

Jana baada ya fainali ya kombe la dunia kumalizika nilipata maumivu makali sana ambayo sijawahi kuyapata kwenye masuala ya kimichezo yaani moyo ulikuwa unauma sana alafu nikawa sina raha kabisa. Nilijishangaa sana kutokana na hiyo hali, kwakwel niliumia sana na nikanyongonyea mithili ya mrenda.

Nilipenda sana Ufaransa atwae huo ubingwa lakini haikuwa hivyo, ilifika kipindi ukitizama kikosi cha Ufaransa chote ni Waafrika kasoro kipa wao tu, nilipenda sana hao wabaruya wachukue ubingwa. Pongezi sana kwa Mbappe

Mpaka sasa hivi bado nina maumivu makali sana, nimejaribu kutumia dawa za kutuliza maumivu lakini bado sijapata nafuu yoyote ile. Poor me
Pole sana ndo ukubwa huo
 
Maisha yangu yya mpira fainali 2 ziliniuma saana.

Arsenal vs Barcelona 2006
France 🇫🇷 vs 🇮🇹italy 2006
 
Back
Top Bottom