Nimepata mbinu mpya ya kupunguza gharama ya tozo za miamala

Kutuma pesa CRDB to CRDB ni bure. Ila kutoa kwenye ATM ni 800 kama sikosei, na kutoa 1m inabidi utoe 400K + 400K + 200K. Mara 3 inakuwa 2400 kwisha habari.
Na lengo la tozo ni kurudisha afya ya mabenk.maana yalikua yanakufa..kaz zao zilihamia kwenye miamala ya simu...wanasahau kuwa technolojia inakua ila wao hawatak badirika...
 
Mkuu ujue mimi huwa sikuelewi sana wakati mwingine unakuwa mkosoaji na wakati mwingine unakuwa upo upande wao....kimsingi hapo ni kama sijakwepa kodi coz hiyo huduma ipo kihalali na inatumika
 
Mkuu ujue mimi huwa sikuelewi sana wakati mwingine unakuwa mkosoaji na wakati mwingine unakuwa upo upande wao....kimsingi hapo ni kama sijakwepa kodi coz hiyo huduma ipo kihalali na inatumika
Na Siku zote huwa sipendi Kueleweka.
 
Hayo makato sio kodi ni tozo ya uzarendo ndio maana ni kubwa kuliko pesa inayostahili kulipia kodi
 
Na lengo la tozo ni kurudisha afya ya mabenk.maana yalikua yanakufa..kaz zao zilihamia kwenye miamala ya simu...wanasahau kuwa technolojia inakua ila wao hawatak badirika...
Sidhani kama biashara yao ilikuwa ngumu sana kihivyo ni huyu dr wa uchumi ndio kichwa maji
 
Kuna
1.Kukwepa kodi (ni kosa kisheria)
2.Kuepuka kodi ni halali kabisa.
Kinachozungumziwa hapa ni kuepuka tozo. Ni sawa na nimwambie mtu usinitumie kwa simu hio 4m kwasababu nitakatwa 18,000 bali mpe bodaboda aniletee au nitumie moja kwa moja kwenye akaunti yangu. Hapa nimeepuka tozo na niko sawa kwa mujibu wa sheria hakuna jinai.
 
Serikali yenu sikivu inakwenda kupiga marufuku matumizi ya hiyo Lipa Namba huku wakiwahimiza wadanganyika kuachana na matumizi ya cash
 
Uzuri kwa hao wazungu hamna mtu ambaye anadokoa pesa ya serikali na kujineemesha kizembe bila kuwajibishwaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Hapa hizo tozo utakuja kusikia tu kuna mtu kajimilikisha sandarusi kisha watamuita Kisutu ila hafungwiπŸ˜…
 
Very nice explanation chief!
 
Umeifafanua kisomi - tax avoidance vs tax evasion. Yule mwingine anaongea ya kijiweni.
 
Umewahi sikia kodi za wazungu zinatumika hovyo na wanasiasa.
Mimi nikipata chance ya kuikwepa nashukuru aisee.
 
Wananchi wakiyaona maendeleo awatokwepa kodi.Pili kodi nyingi zinakiuka kanuni ya kodi.Huwezi ukafanya dabo taxation kwa pesa hio hio moja huku ni kuwapora wananchi pesa kinguvu.
Kodi yeyeto ikiwa kubwa itakwepwa tu hii ni principal
 
Mkuu mbinu uliotumia ni yakawaida tu na hata Tigo-pesa wenyewe wanaielewa, wewe hujatoa pesa kutumia namba ya wakala bali ulituma pesa kutumia namba ya simu ya wakala na huwenda ndio account ya namba ya simu ya wakala anayo pokelea pesa toka benki kulipia miamala ya wateja wa TIGO-PESA, na kwa njia hiyo tozo la laki moja ni 1600 bila kodi ya serikali kwa vile ni muamala unaotoka account ya simu kwenda account ya simu.
 
Natamani kujua ile kumtumia asiye na akaunti ya benki, ila akatoe kupitia ATM…. gharama zake zikoje?
Sina uhakika na hilo, lakini kuna sehemu niliona wanasema gharama ni zile zile za ATM kama kawaida. Lakini unaweza kupiga kwao wakupe taarifa
 
Uzuri kwa hao wazungu hamna mtu ambaye anadokoa pesa ya serikali na kujineemesha kizembe bila kuwajibishwaπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…

Hapa hizo tozo utakuja kusikia tu kuna mtu kajimilikisha sandarusi kisha watamuita Kisutu ila hafungwiπŸ˜…
Wanafunzi hawana hata madawati halafu unasikia kodi yako imetumika kuwajengea majumba na kuwanunulia wastaafu magari.
 
Sawa wewe ulilipa nini kwa wakala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…