Money Penny
JF-Expert Member
- Jun 20, 2016
- 17,694
- 17,131
- Thread starter
- #181
Eti ee, embu soma page ya 7 UONE kama kuna misinformationAcha kuspread misinformation...it's a coincidence
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Eti ee, embu soma page ya 7 UONE kama kuna misinformationAcha kuspread misinformation...it's a coincidence
Jamani mjifunze kumwamini Mungu alichokupa sio kilemavu(kinyonge) mbona mnakuwa hamna Imani mmejawa wasiwasiHongera kwake kizazi hiki ni nadra sana kuolewa bila kutoa sex ila Bwana amemuona achunge asikutane na yle jamaa naamini wanaume hawaachag x zao
Kopi Shem?!Nimejifunza kitu
Exactly,Hofu akishasettle anaweza kurudia mtu wake wa awali
kila mtu na bahati yakeskia hii, jana nilikuwa napewa stori na dada mmoja anakaribiwa kuolewa
nikamwuliza amempataje mpenzi wake
akanijibu
Dada: Nimempata kwenye morning and evening glory nilikuwa naenda kila siku kanisani, kumbe huyo kaka akaniona akanipenda akawa anapima frequency ya kuja kanisani kama na beep au namaanisha
basi baada ya mwaka mmoja akani approach asijue kuwa niko singo mimi tena kwa muda wa miaka 3
tuka exchange namba, tukaanza mawasiliano, baada ya mwaka akaomba wazee wake waje akutane na wazazi wangu!
Money Penny: Kwahiyo hamjazini mwaka wote huo?
Dada: Hatujazini boss hata ku kiss! nilimwambia nimetoka kwenye very painfull relationship, nimekaa miaka 3 sitaki kusikia kuzini mpaka kwenye ndoa. Ni kweli yale maombi ya morning na evening glory yamenisaidia sana, nilikuwa naenda kwa Bwana Yesu, Bwnaa Yesu akanipa Bwana Mume (My Lord)!
Money Penny: Haya haya sasa! nyie wenzetu mnaendaga wapi kupata waume?
jamani muende kanisani, ohooo! Yesu anatoa waume kama mvua huku Morning Glory!, ila usiende kudanga tu!
CoincidenceEti ee, embu soma page ya 7 UONE kama kuna misinformation
Ila huyu amepambana sana
Page ya 7 yakuhusu auCoincidence
Kuolewa siyo shida,Je ataweza ishii kwenye Ndoa!!?? Hapo ndiyo kinakuwaga kipengele kwenye Ndoa!!akiolewa ntakujuza!
AtawezaKuolewa siyo shida,Je ataweza ishii kwenye Ndoa!!?? Hapo ndiyo kinakuwaga kipengele kwenye Ndoa!!
CHAPTER 1 : NILIMPATAJE MUME WANGU KANISANI KWENYE MASIFU YA ASUBUHI NA JIONI!
Tarehe: 27/7/2015
Saa: 11 jioni
ENEO: Africa
Ofisi: inahifadhiwa
Nilikutana na mrembo mmoja kwenye ofisi moja, tukiwa wote kwenye subira ya Kuingia kwenye Ile ofisi, tulikaa zaidi ya Lisaa limoja tukaamua kuwa Marafiki WA foleni isiotembea
Money Penny: kwani mami, ilikuwaje mpaka ukampenda Sana huyu Yesu aliekuletea Mume kanisani?!
Mami: naitwa Yusra
Money penny: Yusra?! Kwani wewe NI mkristo??
Yusra: nilizaliwa kwenye familia ya kikislam Ila Kwa sasa nimeokoka nampenda Yesu,
Money Penny: wow, okay! Niiice, na sasa unaenda kuwa mkristo kamili Novemba
Yusra: Acha tu, NI kama naota kumbe kweli, sijawahi kufikiri ntafika hapa
Money Penny: Bwana Yesu ulikutana nae wapi mpaka akakuletea kanisani?
Yusra: kwenye Afya ya akili!
Money penny: weee, sasa alikutokea like taraaaa au like what happened?!
Yusra: akaangalia SAA yake akasema appointment yangu ina DK 30 niingie ngoja nione kama nitamaliza kumueleza ikishindikana andika namba yangu tutaendelea
Money penny: nikaandika namba, Stori ikaendelea
Yusra: all my life sijawahi date wanaume WA kikislam, NI wakristo Tu, sijajua kwanini, mpaka sasa nimekuwa na ma boyfriend 6 Tu na huyu WA 7 ndio anataka kunioa na wote walikuwa wakristo
Sikuwahi kuwaza maana naipenda Sana dini yangu, mno, lakini ngoja tuanze na boyfriend WA Kwanza
Boyfriend WA Kwanza:
Aliitwa Ndumi, mnyakuysa, nilikutana nae sekondari kidato cha 4
He was my first if you know what I mean
Money penny: wow, you waited mpaka age 18?
Yusra: Yes hata nilitaka kukaa mpaka kwenye ndoa, but Ndumi alinichengua Sana, after all that nikapata mimba ya utotoni
Nikaogopa Sana kushea nyumbani, nikamweleza Ndumi akaikataa kabisa, akasema hausiki, hapo tumeshamaliza mitihani ya kidato cha nne,
Nikapaniki, nikauliza Kwa Marafiki wakaniambia kuhusu kuitoa maana wazazi wakijua NI aibu na wataniozesha haraka na Mimi sikutaka kuolewa haraka nilitaka kusoma maana nilikuwa na ndoto zangu, wakanielekeza Kwa dokta nikaitoe, nikiwa mdogo na mjinga nikakubali, kwenda kuitoa nikaacha kinoti nyumbani kwa naenda kutoa mimba, just incase nitakufa, mtanikuta sehemu Fulani, kweli sikufa, nikatoka salama, nilivyotoka nje nakutana na wazazi nikakimbizwa hospital Kwa matibabu, Kuangaliwa nikakutwa siko vibaya Sana wakanisafisha nikarudi nyumbani nikakaa muda nikapona, nikafanyiwa seminar na wazazi imagine tangu nitoke hospital kuja kupumzika wazazi wangu hawakutaka kujua why and why, nilipopona enough kujiunga na kidato cha tano ndio WAZAZI wakaniita kunipa seminar ya mimba, uzazi, kujamiiana,
Nikasomeshwa wiki mzima nikawaelewa wazazi nikawaomba msamaha,
Baada ya wiki 3 MATOKEO ya kidato cha nne yakatoka, nikawa nimefulia division one, nikapangiwa kusoma boarding form 5 shule nzuri Sana ya wasichana tupu
Nikaanza form 5 science, PCB nataka kuitimiza ndoto zangu, nikapita form 5 vizuri nikaingoa form 6, tukiwa tunamalizia form 6 ikapitishwa kongamano la injili pale shuleni tukaenda wote, watu wa dini zote maana ndio ilikuwa entertainment yetu Ukiwa bweni hamna kingine zaidi ya hivyo
Tukahubiriwa hapo penny, mahubiri yakaniingia, nikaokoka, watumishi wakachukua majina ya waliookoka basi Kila wiki wanakuja kutusalimia, kutufundisha neno, kuukulia wokovu n.k
Ikaenda wiki ya Kwanza ya pili, Yule mhubiri akawa anakuja na kijana wake WA kupiga vyombo, Yule kijana nikampenda bwana nae akawa amenielewa alikuwa anaitwa Samson
Kwahiyo tukapanga nakwambia watoto wa Yesu kuwa tunaonana Kila jumapili, jioni anamlipa.mlinzi natoka tunaenda kuzurura lakini hatu-do
Tukapeana ahadi nyingi Sana, za kuoana baada ya shule nikamweleza maono yangu tukawa tunaomba, kweli mapenzi Moto Moto, mitihani ya form 6 ikaja, tukafanya Tukarudi uraiani, kufika uraiani tunasubiria Matokeo, nikaanza kusali kanisani kwa.mpiga vyombo nikiwa najiiba, basi Yule Mtumishi kuniona akafurahi mno, akasema kondoo amekuja kumbe nimefuta mapenzi
Lakini Kwa sehemu niifuata both mapenzi na closure ya Mungu, unajua kutoa mimba mama sio kitu rahisi, Kila nikilala nikawa naskia sauti ya mtoto mchanga analia, lakini nikienda kanisani wka walokole naweza kaa hata miezi au mwaka sijaskia Ile sauti ya mtoto ikawa NI Siri yangu simambii MTU
Kanisani wakatufundisha Juu ya Kuongea na Mungu, kwangu ikawa ishu serious Sana nakamata Kila mahubiri na maombi kwasababu najua kinachonitesa
Nikaendelea kusali pale natokea ya form 6 yakatoka, nikawa nimefaulu division 1 ya tatu, yule mchumbaangu Samson akafurahi Sana tukaenda kanisani kumweleza Mtumishi, akatuombea, tukato sadaka, basi siku ya kutoa SADAKA ya shukrani paaap, samsoni Kesha arrange anataka kunioa, yupo Chini na Pete, ananiomba Anioe, nilichoka nikazimia, kuja kushtuka Niko ofisini Kwa Mchungaji, namwona mama ananipepea, kujankukaa vizuri naambiwa kuwa walikuwa hawajui ndugu yangu simu ikaita, wakapokea kumbe ni mama, wakamwelekeza wanashangaa mama WA kiislam anaingia wakamkaribisha mama anafoka nini mwanangu mmemuokota wapi, wakajaribu kumweleza mama hasikii, akapiga simu taxi ije, wakiwa wanasubiria taxi nikazinduka,
Mama akawa ananiuliza vp
Imekuwa mwanangu mpaka umeingia kanisani, unaumwa husemi ulikotwa wapi? Haya haraka twende hospitari gari imekuja, mzobe mzobe hapo nikasahau kuaga mpaka kanisani, kufika hospital dokta ananiuliza vipi nikadanganya nimezimia, Tu nikaokotwa na wasamaria wema, basi doka hakuona shida yangu Kwa wakati hio Tukarudi nyumbani nikawa siendi tena kwenye Ile kanisa maana makelele ya mama wewe na wakristo Sisi NI waislam wakauliza unataka kusoma au kuolewa, nikasema nasoma huoni nimefaulu, mama akasema basi tumepata Matokeo umepangiwa chuo flani nikafurahi mnooo, akasema lakini huko hauendi, Mimi na babako tumepanga utaenda kusoma nje ya Africa, chuo tumeshapata na unaondoka kesho, panga nguo zako, Visa tayari, nikawa kwenye mshangao na mshtuko, lakini kwasababu ni kozi nayotaka nikakubali, imagine sikupataga muda WA kumuaga samsoni maana na simu nilinyang'anywa nikawa kwenye house arrest nisijetoroka nyumbani
Safari ikawadia nikaenda kusoma nje, nikasoma mwaka WA Kwanza, WA pili nikapata boyfriend mkristo tena, anaitwa lameck, tukaenda weee mpaka mwaka WA 3 alipojua Mimi mwislam kwetu akanikwepa, akatafuta mwanamke mwingine nikawa stranded, but kwasababu napenda Sana shule nikaendelea kusoma Kwa hasira nimefika mwaka WA 3 nikamaliza na first class, nikapataga KAZI hapo hapo nchini, nikaanza na KAZI, nikiwa kazini siku moja nikatumwa Kwa client, kufika Kwa client boss wa client akanipenda, akanifukuzia, Mimi nikawa nipo half half maana hii NI kazi, Yule boss client alinisumbua, nikawa muazi nikamweleza work ethics haziruhusu, akaniomba atakaa mbali, lakini lazima tuwe na mahusiano, ikanichukua muda kukubali, baada ya mwaka mmoja nikamkubali, alikuwa anaitwa Clark
Tukaenda na Clark, sababu yeye NI mzawa WA Ile nchi na NI Tajiri akawa ananizungusha nchi zima, sehemu zingine nalishindwa kwenda nikiwa mwanafunzi, akanipeleka tukasafiri Europe, America, ma boat cruise, nikasema hapa mume nimepata si KAZI ninayo, kuja kuwaambia wazazi wangu sasa walikataa Katu Katu
Hatukuelewana kwenye simu na wazazi, ikabidi TUFANYE hata video call wamuone walikataa Kwa kigezo cha dini, walitamani Sana niolewe na mwislam mwenzangu ikabidi sasa tuachane na Yule bwana, nikiwa kwenye mawazo ya kwanini kila.nikikaribia kitu changu cha ndoa kunakuwa na kukataliwa, sifikii hatima ya ndoa, nikaingia kanisani kuomba, akaja Bibi mmoja Mzee akakaa pembeni yangu, akawa anasali, Mimi nami naendelea na maombi, Yule Bibi aligeuka na kuniambia lazima utubie dhambi ya mtoto hata Kwa msaada wa Mchungaji ili upone, nikashangaa Sana Yale maneno, Bibi akarudi kwenye maombi na baadae akaondoka, nikiwa katika mawazo ya may be Bibi atakuwa mkweli nikafanya process za kumpata Mchungaji Kwa maongezi ya kutubu dhambi zangu sikufanikiwa Kila niliweka appointment inakubalika ikifika siku ya kumwona NI dharura kwake na kwangu, ikaenda hivyo miezi 6, nikaja kupata mchumba kanisani tena, huyu aliitwa James, alipagawa na Mimi kama ameona Mbingu hataki kusubiri anataka ndoa Tu, nikawa nakosa nguvu likija swala la ndoa maana najua sina baraka za wazazi, na hawa wanaume wote Kila nikifanya nao tendo la ndoa tukilala lazima nimwote mtoto analia nisiemjua, sasa Kila nikimwotea Yule mtoto haipiti muda mwanaume anataka ndoa then hatukai Tunaachana
Kwa huyu James ndoa haikuwa shangilio Sana maana wazazi hawataki, nafanyaje nami nimeokoka siwezi danganya nikaona Bora nimwambie James ukweli, nilipomweleza Juu ya kutoa mimba sikumwona tena NI kama aliyeyuka hakurudi, simu zikawa haziendi, hapokei, nimeblackistiwa basi nikarudi kwenye jitihada za kumpata mchungaji
Katika jitihada za kumtafuta Mchungaji na kumkosa, siku nikawa naenda sokoni, nikakutana na Kaka mwislam kavaa kabisa kiislam, akaja kunisalimia kama ananijua, nikamjibu, tukaongea akaomba mawasiliano tukawa tunawasaliana mara akaanza kunipenda lakini Mimi sikumpenda,
Tukakaa mwaka mmoja akaomba aonane na wazazi wangu nikajua Tu akishaenda huko basi naolewa nae, nikazuga miezi 6 mwingine mwishowe nikamweleza ukweli kuwa Mimi nimeokoka, sio mwisla itakuwaje?!
Akasema hatonizuia kwenda kanisani ataheshimu dini yangu, nikaona kweli, nikamtambulisha Kwa wazazi wakafuraha Sana kuwa sasa nimepata chaguo Lao lakini sio chaguo langu,
Tukiwa katika process za mahari nikamweleza ukweli juu ya Ile mimba iliotoka, nikamwambia ikitokea changamoto ya kutopata watoto basi ujue Nina historia, hakusema chochote, akaendelea na process za ndoa, baadae nikaja kupata simu ya Mchungaji anataka kunitembelea nyumbani maana nimemtafuta Sana Kwa muda bila mafanikio, namimi nilikuwa nimeshasahau Juu ya Mchungaji
Alipokuja nikamweleza Kila kitu sikumficha, tukaomba Sana Sana tukatubia uovu WA Ile mimba, baada ya akaondoka tukawa TUNAENDELEA kuwasiliana Kwa maendeleo yangu binafsi, mama yangu akaja nilipo Kwa ajili ya maandalizi ya mahari, huwezi amini siku mahari inataka kupokelewa nikawa kama nimechanganyikiwa naongea mwenyewe kama chizi sikukumbuka what next nikajikuta hospita nimefungwa kamba milembe ndogo, namwuliza mama nimekaa muda gan anasema Miaka 2, tumelipa matibabu mpaka tumechoka, hivi kesho unarudi Africa ukaendelee matibabu huko, nikauliza na ajira je, akasema umeshaipote hakuna Mzungu angekuvumilia Miaka 2 ya uchizi, hakuna NI Bima yako Tu imetusogeza maana tuliona tutumie Bima kule Africa huwezi pata matibabu Bora kama huku
Basi baada ya wiki nikaondoka Ulaya, kurudi Africa, nikatafutiwa psychologist nikaanza matibabu, maana Afya ya akili yangu iliharibika Sana sikuwa hivi nilivyo sasa, sijajua kwanini Yule mtoto niliemtoa alinizuia ndoa wakati nilishatubu Kwa Mungu
Money penny: kwahiyo Yusra haukuwahi kuolewa
Yusra: ndio, sikuwahi mpaka majuzi, nilipopona, nikatafuta church hapa hapa Africa maana niliwaambia wazee my sanity inakuwaga nikienda church na wasinizuilie mtu WA kunioa tena maana nilishapoteza mara 6, tulidiscuss Juu ya ishu ya mtoto nikapata msaada WA kimwili na kiroho
Maana Afya yangu ya akili haikuwa sawa, imagini nilikuwa namiliki zaidi ya pound 300,000 zote zimeisha, nilivyotoka rehab, nikasema nimepona, haikuwa hivyo, nikaanza kwenda night clubs, nakula, nakunywa, nanunulia watu vitu, nanunua designer clothes, shoes, perfumes, bags, clutches, ili NI belong, ili niwe fulfilled, natembea na waume za watu, Yani fujo mwanzo mwisho jamaan, wazazi wakahisi wananipoteza maana nilikuwa nakaa kwangu sasa, wakawa wanakuja kunikota baa, mara sijui nimegoma kulipa taxi Niko polisi, mara nimelala mtaroni
Money penny: na why ulikuwa unafanya hivyo?
Yusra: my dia nilikuwa overly stressed, nikiangalia wenzangu wooote Wana makwao, Mimi Niko kwetu, agemates sinao wote wako kwao
Siwezi pata mtoto kama navyotaka, Mindoto na misauti ya Yule mtoto bado ilikuwapo, nimempelekea Kwa masheikh, Kwa wachungaji, padri, wapi Hali iliobakia hapo hapo
Money penny: uli recover VP sasa
Yusra: ndugu walikusanyika, wakasema sasa huu mzigo tunawatua wazazi wako, tunaingia Kati Sisi, kama utagoma kupona utaponea kwetu maana wazazi wanasumbuka Sana na kuteseka, inabidi ukasirike na uamue kujisamehe la SIVYO utazidi kuteseka
Nikaomba nipelekwe kanisani, kule Kwa mchumbaangu nilietenganishwa nae nikakuta alishao na watoto wengi kama siafu, Mchungaji Yule nae alishaoa, wakaniombea Sana, Kila week wakajilaumu kwanini sikuwaeleza Juu ya kutoa mimba
Money penny: Tangu umepata huu msaada WA kiroho imechukua muda gan na hii pschology ili kufanya Afya ya akili kukaa sawa?
Yusra: Miaka 2 mbele ndio nimekaa Sawa, nikajifunza Vitu vingi mno, kuwa msamaha unatakiwa uanzie ndani, sio mdomoni, tangu nimejisamehe, na kuamini kuwa Mungu alishanisamehe
Na kumkemea shetani Aache ujinga
Money penny: how are you now?!
Yusra: naingia my last session Leo, naonekana nime-improve Sana kiasi cha kwenda kufanya kazi
Money penny: wow am happy for you
What about your love life??
Who is the lucky dude?!
Yusra: am happily single my dia
Muhudumu: Yusra Mwamkazie
Yusra: here here!
Haya my dia will talk more you have my number
Money penny: absolutely!
Nikamwona Yusra huyoo anapepea kwenda ofisini, huwezi amini kama NI yeye alikutwa na matatizo yote hayo, nikamhurumia!
Niliendelea kuwasiliana na Yusra Kila week, progress ilikuwa nzuri kwake, tukawa marafiki kama dada mtu na mdogomtu, kwa miaka 2 mbele.
Mwaka WA 3 akapata mchumba aliefiwana na mkewe, huko kanisani kwenye masifu ya asubuhi na jioni au (Morning and evening Glory)
Huyo mwanaume alikuwa mjane, baada ya kufiwa na mke alikaa Miaka 10 bila kuoa, siku alikutana na Yusra alimpenda ghafla, wakakaa kwenye mahusiano Miaka 2, wakaoana
Hivi sasa wana watoto mapacha 3, wanaishi Los Angeles California.
Tukutane kwenye sehemu ya 2 ya hadithi hii ya ''nimepata mchumba kanisani kwenye morning and evening glory''
HAYA MZIGO NDIO KAMA HUU UMESHUKA MKUJE Smart911 Kyalow mshamba_hachekwi moneytalk Mtoto halali na hela sab Ushimen Azarel Babu Njunju mtu chake Akilinjema Number ni 26 Accumen Mo Bujibuji Simba Nyamaume 50thebe uttoh2002 Azarel EMMYGUY MastaKiraka Mrs Van The king 07 vvm Dan wick bongo dili Vito Corleone Cr wa familia Akilinjema neno ni upanga antimatter Folk Part II zege la nyasi The Shah of Tanganyika steveachi Hbzoo Slim5 makedonia father-xmas loviesundy@wa stendi steveachi cotyledon Smart Gang Sir Midabwada
anasbo Mwiba1 Watu8 jkipaji heartbeats @