Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Nimepata milioni 50, nifanyie biashara gani niwe milionea?

Ushauri wangu kwako ndugu ni kwamba mimi naona kilimo cha viazi mviringo kinalipa na ni kizuri sana kwa kuwa kinachukua maxmum ya miez 4 lakini kawaida ni miez 3 kuvuna, na kiazi kina mahitaji makubwa sana sokoni na kwa mtumiaji wa mwisho pia...Kwa milion 50 unaweza kupata zaid ya milion 800 ikiwa unafanya kilimo kama kinavyotakiwa...Utaanza na kukod shamba la hekali 40 ambayo itakugharimu sh 60,000 kwa kila heka...Mbegu mpya ya kiazi ambacho hakina mabonde ni sh 100,000 kwa hekal moja ...Utanunua mashine za kumwagilia ambazo kwa makadilio itakughalimu sh milion 3 maximum ....Utanunua mbolea ambayo kila heka utanunua mbolea ambayo itakugharimu sh mil 6 kwa hekali 40 zote ...Utaweka vijana wa kulima ambao utaelewana nao kwa mazungumzo ya kawaida ambayo inaweza kukugharimu sh 400,000 maximum kwa hekali zote 40 ..ukipiga hesabu kwa ujumla utakuwa umetumia sh milion16 tu katika hiyo 50 uliyonayo..Na kiazi kwa hii mbegu mpya unatoa gunia 80-100 kwenye hekali moja...Kiazi kama hiki kisichokuwa na mabonde kina mahitaji makubwa sana sokoni na kikishuka bei kinauzwa 80,000 kwa gunia dar es salaam...Ndugu ukipiga kwa mahesabu ya haraka haraka unaweza kuvuna gunia 3,200 katika shamba la hekali 40 kwa msingi wa shiling milion 16 tu kati ya milion 50 ulizo nazo ...Na kama utauza kipind cha bei ya chini ya sh 80,000 kwa gunia utakuwa umejipatia tsh 256,000,000 ...ukitoa gharama za usafirishaji kutoka shamba hadi masoko ya dar es salaam itapungua hapo kidogo lakini haita affect hiyo figure ..May be 240,000,000... Huo ndo ushauri wangu ndugu na nina uhakika kabisa kama ukitumia kias chote cha sh mil 50 bas utapata faida zaid ya hiyo ambayo inaweza kufikia hadi milion 800...
Are you serious?
 
50 M not enough uwe billonea.calculate risk before u jump.

USIJARIBU KUWEKEZA HIYO PESA BONGO AFU UBAKI UFARANSA UTARUD ZIRO.
Kaa huko huko ongeza pesa nakuambia usibweteke umri mdogo nguvu unazo fanya kazi extra time ongeza pesa uwe na salio la maana na ukirud tz wekeza kwanza kwa fixed asset nunua viwanja..nunua nyumba ...jenga weka wapangaji wa aina zote wa kukodi nyumba nzima....chumba sebule ...na wale wa chumba kimoja una uhakika wa kupata pesa bila stress kila baada ya mwezi mmoja au sita na mwaka mmoj

Biashara zenye risk ni nzur ila ujue lolote laweza tokea ukarud kwenye ziro kuwa makin na chunguza kwa makin fanyia research biashara yako kabla ya kuanzisha
Kwahiyo ili uwe bilionea unatakiwa kuwa na kiasi gani?
 
Scania mende ni milioni 50 ikiwa nje, bado haujaileta bongo ushuru wapige zaidi ya 50m ifike kwenye mia na kitu. Msimpoteze jamaa
.. I'm talking from experience..
 
Mwanzo Uliandika Ulikaa Ufaransa ukapata milioni 50,Mara Hii ume-edit na hainyeshi hata hiyo milioni 50 umepataje,Acha Kutufanya wanaJF MAZWAZWA Sawa? Kama ulikaa UFARANSA Ukapata hizo mil 50 bora uendelee kukaa huko huko au kama mmeuza nyumba ya urithi kumbuka marehemu uenda na chake tunakupa miaka miwili utakuwa huna hata 100.
 
Mkuu hebu tafuta wataalam wakuelekeze vizuri hili ninalotaka kulisema hapa chini!

"Nunua hisa za kampuni za mawasiliano kama Voda ili pesa yako iwe kwenye mzunguko huku unaendelea na majukumu yako ya kila siku huko ufaransa bila kubughudhi ubongo wako kwa mawazo ya kupigwa endapo utaweka biashara na ndugu yako kuisimamia badala yako"

I stand to be corrected!
 
Heshima zenu wakuu.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 25, ni Mtanzania nnae ishi nchini ufaransa.

Nimebahatika kupata shillingi mil 50 za kitanzania na nahitaji kuwekeza nchini Tanzania.

Je ni fursa zipi nnazo weza kuzipata Tanzania kuweza ili kuimaximize hii pesa ili niweze kuwa Millionaire ndani ya miaka 10 kutoka sasa.?

Asanteni.
Wekeza kwenye construction business. Mimi mwenyewe nafungua kampuni ya ujenzi. Kuna pesa nyingi sana. Naomba tuwasiliane 0767102102 au wigotz@gmail.com.
 
Back
Top Bottom