Nimepata Mtaji wa TZS 20Mil, nataka mawazo mbadala ya Biashara

Nimepata Mtaji wa TZS 20Mil, nataka mawazo mbadala ya Biashara

Ni wazo zuri kweli.

Nimezisahau ABC za kampuni fulani ya maji. Ila walihitaji uwaonyeshe 10M kama mtaji halafu wanakupa gari, godown kitu cha tatu nimekisahau ndugu yangu.

Fuatilia.
Ni kampuni gani mkuu niifanyie kazi hii fursa
 
Kuwa wakala wa vinywaji jumla jimla..au kanunue mchele peleka dar
Maharage peleka dar
 
Bora hata ungekuja hapa Dom ningekupa mbinu ufanye biashara kama yangu ta majeneza na sanda ungepiga hela sana na wala hulipii mapato
 
Hivi karibuni nimepata mtaji wa takribani Mil 20. Nimekuwa nikipanga kuanza biashara ya electronics kama vilivyotajwa hapa chini, changamoto inayoniogopesha ni mamlaka za serikari kuhusu vibali na ushuru na ubora wa wazo lenyewe. Naombeni ushauri nini nizingatie, nini niongeze kwenye list au kipi nibadili
  1. Simu zenye thamani ndogo
  2. Earphones/Head phnones
  3. Phone covers
  4. Screen protectors
  5. Wireless speakers
  6. Batteries
  7. .......
Joniee, strctly wazo lako ni boashara hiyo tu? Na lazima ufanyie dsm?
 
Njoo nikuandalie bussiness plan kwa bei nafuu tuu
 
Twende pole pole mkuu, hizo 20M za mtaji umezipataje? Kama ni kwa biashara endelea kuikuza hiyo hiyo biashara iliyokupatia hizo pesa badala ya kuanzisha biashara nyingine. Otherwise unambie chanzo cha mtaji wako.
Sijawahi fanya biashara
 
Fungua duka la electrons then kaa mwenyewe kwa muda kidogo then pesa inayobaki fungua mgahawa au saluni kubwa mchezo umeisha.
 
Pharmacy huwa zinalipa sana pia...
Maduka ya hardware
Electronics
Wakala wa vinywaj kama pespi na cocacola na maji au wakala wa bia kama tbl...
All in all lazima ukifanyacho ukipende toka moyoni wewe kwanza...na usianze biashara mpya na hela ya mkopo tu ....
 
Naungana na wote wanaokutaka ufanye utafiti kwanza, hata kama itachukua miezi. Fikiria pia biashara ya mitungi ya gesi mkuu
 
Hivi karibuni nimepata mtaji wa takribani Mil 20. Nimekuwa nikipanga kuanza biashara ya electronics kama vilivyotajwa hapa chini, changamoto inayoniogopesha ni mamlaka za serikari kuhusu vibali na ushuru na ubora wa wazo lenyewe. Naombeni ushauri nini nizingatie, nini niongeze kwenye list au kipi nibadili
  1. Simu zenye thamani ndogo
  2. Earphones/Head phnones
  3. Phone covers
  4. Screen protectors
  5. Wireless speakers
  6. Batteries
  7. .......
Fungua mkuu hii ni moja ya biashara inayo lipa sana ukujua namna ya kuifanya
 
Ebu jaribu kuwekeza kwenye restaurants & catering services vizuri Kama inaweza kuwa ni kitu unachopenda na ujitume vizuri, sema usiwekeze pesa yote milioni ishirini, pesa kidogo nunua usafiri kama isuzu au maarufu kirikuu used ya Mil.6 ufanye shughuli nayo kubeba mzigo yako na ya watu watao itaji.
 
Back
Top Bottom