Nimepata nafasi ya kujitolea miezi minne. Je, nichukue fursa au niachane nayo?

Nimepata nafasi ya kujitolea miezi minne. Je, nichukue fursa au niachane nayo?

Kaka Asante
Nilichogundua katika maelezo yako.
Akili yako ime focus zaid katika suala la kuajiriwa kuliko kutafuta fursa zingine tofauti na ajira.
Kitaa kina fursa nyingi Sana ila ni wachache wenye uwezo wa kuzitumia, kila uchwao Kuna watu kitaani jua linawawakia na wengine wanazidi kustawi hapo tofauti inakuja katika swala la mitizamo na kuchangamkia fursa.
One of the worst ever mistake I made in my life ni kujitolea Tena enzi zile maafisa elimu wanapita mashuleni kuchukua majina ya waliojitolea ili wapewe kipaumbele kwenye ajira za 2020 guess what, Hadi sasa Nina mwaka wa saba Niko mtaani (Chem & bios).
Kilichoniokoa nilifanya maamuz magumu nikapiga chini kujitolea baada ya kukosa ajira, japo Kuna watu walinishauri niwe na subira lakini niliamini zaidi katika njia zangu.
Hadi sasa japo sijatoboa kimaisha ila angalau familia yangu inaishi vizuri na huenda labda nisingejitolea ningekuwa nipo mbali kidogo.
Wangu ni ushauri ila fuata nn moyo wako unapenda, huenda huna muelekeo kimaisha sawa lakini akili yako haijafika mwisho kiasi kwamba umeshindwa kuziona fursa, ila ni kwamba hujaamua kuzitumia vyema.
Sana kwa ushauri mzuri, Kuna fursa nikeziona nyingi sana, ila issue jikwamba zinahitajika pesa ili niweze kuzi cultivate hizo fursa. So nahitaji sehemu nipate capital
 
Kaka Asante

Sana kwa ushauri mzuri, Kuna fursa nikeziona nyingi sana, ila issue jikwamba zinahitajika pesa ili niweze kuzi cultivate hizo fursa. So nahitaji sehemu nipate capital
Wakati mwengine Bahati katika maisha Ina nafasi japo asilimia zaidi ya 90 ya matokeo katika maisha yetu yanatokana na jitihada maarifa ubunifu na kutokukata tamaa,
Kama hauna ramani yoyote kajitolee ila trust me miezi minne ni muda mwingi Sana kuipoteza regardless wamekuhakikishia ajira, kwa maisha ya mtaan miezi minne hata kwa bodaboda tu yoyote anayejua kazi yake anauwezo wa kupiga hatua kubwa.
Ushauri wangu nenda kajitolee ila akili yako iwe inachanganua fursa kitaani, ukipata fursa yoyote kitaani hata Kama umejitolea kwa wiki mbili nakushauri kimbilia fursa, japo mambo sio marahis ila kitaa kikikubali hutakaa uwaze kuhusu ajira, kujitolea ni zaidi ya utumwa ndugu hasa staff members wakijua wewe ni wakujitolea utapigishwa mzigo hatar mixer na madharau Kama una roho ndogo unaweza ukapata sonona.
 
Mimi ni fresh graduate, nimehitimu katika moja chuo kikuu hapa jijini.

Taaluma yangu ni ualimu I have bachelor of science with education (biology and geography).

Sasa wakuu Katika harakati za kupambana na maisha huku mtaani Toka mwezi wa Saba nilipo maliza, Leo hii nimeitwa na moja ya shule ya private wamenambia nikajitolee kwa muda wa miezi minne (January hadi April 2025) Kisha watakuwa Wana screen utendaji wangu wa kazi kiasi kwamba kama tawalizisha watanipa mkataba.

Pia, katika wito wao huu, wamenambia Katika kipindi chote hiki Cha kujitolea Chakula na malazi vitakuwa juu yao (it's boarding school).

Wakuu hapa nipo dilemma, mana mtaani Sina Kazi yoyote zaidi ya kushinda na Saka vibarua visivyo onekana , wakuu naomba msaada wa mawazo juu ya hii fursa mana na hofu isijekuwa wanataka Kuni consume tu Kwa muda Kisha wani ache.
Uende ukafanye kazi ,sio kujifanya uko dillema kumbe ndiyo nyie mnatuibia kuku wetu ili mpate vocha za kuwahonga videmu vyenu.

Sasa uko dillema vipi huna kazi na chance imepatikana unaanza kujiwazisha
 
Back
Top Bottom