Nimepata Sup 5 katika masomo 8 ninayo soma ,msaada tafadhali

Upo chuo gani?
 
Reactions: kpi
Ahirisha mwaka maana mpak hapo ni tayari umedisko so ukisema uendelee itakua shida. ila mwakan ukirudi uache ujinga maana inaonyesha ulitoka secondary ukiwa na perception ya chuo bata. kuwa makini jifunze kutokana na makosa
 
Upo chuo gani?
 
 
Upo chuo gani?
 
Wengine tumemaliza zamani kidogo, tupe majibu haya kwanza:-
1. Upo mwaka wa ngapi?
2.Sheria ya chuo inasemaje ? ili ufanye sup inabidi usifeli zaidi ya masomo mangapi?
3.Unasomea kozi gani?
4.Upo chuo kipi?
5.Maelezo mengine yeyote yatakayoweza kutupa undani wako ?
 
WEWE SI NDIYO ULITUAMBIA KUWA UMEPATA DIV. ONE YA POINT 10,NA UNATAKIWA KWENDA FORM FIVE SASA LEO FORM FIVE TAYARI UNA SUP, MBONA UNATULETEA UGUNDUZI MPYA?
 
kama unajua hatma ya watu ambao wamedisko utajutia sana kipindi upo club na wenzako ambao nao wamefaulu ila wewe gundu linakuandma
 
Sup 5 means Disco, wewe umeichezea elimu na kupoteza muda katika mambo yasiyo ya Msingi,pole sana mpo wengi wa aina yako na kwa taratibu za mkopo uki Discontinue tu unatakiwa kuanza kulipa Deni lako bodi mara moja
 
Ahirisha mwaka maana mpak hapo ni tayari umedisko so ukisema uendelee itakua shida. ila mwakan ukirudi uache ujinga maana inaonyesha ulitoka secondary ukiwa na perception ya chuo bata. kuwa makini jifunze kutokana na makosa
Sawa mkuu nashukuru


Ila tatizo linakuja jinsi ya kuwashawishi wazazi waelewe yani shida ndio inaanzia hapo

Kwa maana najiona mkosaji sana


Ilikuwa ugomvi nikiomba nipewe hela halafu wachelewe kunitumia na walihakikisha wananipatia kiasi chochote kile cha pesa ninachokitaka bila ya kuwa na limit ya matumizi kws maana sina mkopo wa serikali (HESLB)


Sasa kitendo cha kuwaambia nimefeli aisee sijui nitaanzia wapi yani
Natamani ardhi ipasuke nijifiche
 
Usikate tamaa. Jaribu kukaa chini na uangalie mbinu nyingi ya kuweza kukuenrol hadi mwakani. Lakini kama unanafasi ya kuongea na wakufunzi watakusaidia.
 
Nipo mwaka wa kwanza
 
Cha msingi hapo kijana hakikisha semister ijayo hufeli hata somo moja na usome kwa bidii ili ufaulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…