Nimepata Sup 5 katika masomo 8 ninayo soma ,msaada tafadhali

Nimepata Sup 5 katika masomo 8 ninayo soma ,msaada tafadhali

Kabla sijakushauri chochote, nipe maana ya hiyo ID yako kwanza

sent from servant of God

Usivunjike moyo me mwenyewe nili supp masomo yote juzi nilipokuwa nasomea cz y clinical medicine to b honest nilivunjika moyo ila nilipiga pindi ya kutosha na nilichomoa yote cha msingi nikuwa na imani tu kwamba kama umepangiwa kufaulu hy coz utafaulu tuuuuuu
Ni pm mkuu.

Wakuu naombeni mnipe ushauri wa kunijenga kisaikolojia ,nimepata supplementary 5 katika masomo nane ninayo soma

Hapa nilipo sina amani kabisa yani ,najiona mkosaji mkubwa sana

Najaribu kutafuta visingizio kwa mzazi lakini nakosa

Natamani kusitisha masomo ili mwakani niombe upya kozi nyingine au kozi ile ile ili mradi nitengeneze cheti kisafi ili huko mbeleni nisisumbuke

Katika maisha yangu nilikuwa sijawahi kukutana na situation kama hii,kwa kifupi sijawahi kufeli sasa kwa marks nilizopata sasa naona kama nimedharirika sio uwezo wangu huo ,to be honest sikuwa serious katika masomo ,sasa chuo kumbe kila kitu kinahesabiwa kuanzia assignments mpaka test bila kusahau UE

Sasa mm assignments nilikuwa nafanya kimzaha mzaha ili mradi nikusanye nionekane nimefanya kazi

Najuta kwa kweli hata hamu ya kula sina ,please ndugu zangu wapendwa wa JF nipeni ushauri jamani tena mbaya zaidi masomo niliyopata sup ni magumu sana kwangu kusapua hivyo basi nahisi naenda kuya carry yote matano aisee roho inaniuma saana
kwa kawaida ukipata sup zaidi ya nusu ya kozi unazochukua hua ni disco ila inategemea na kipindi gani mnafanya hiyo mitihani kama kila baada ya semista mnafanya mitihani ya sup basi umedisco ila kama ni baada ya semista zote mbili basi jumlisha kozi zako zote kisha angalia kama unasup zilizozidi nusu ya hizo kozi umedisco kama ni nusu ama hazijazidi basi utakua na nafasi ya mwisho ya kusapua
Note. ni kwa levo ya shahada kama ni stashahada ama astashahada ni siwe muongo sijui utaratibu wake ndugu yangu

Inawezekana huyu jamaa kweli kasapua,,, ebu cheki huu uzi[emoji116]

Huu ni ukweli usiopingika kuwa wale wanafunzi wanaongoza ngazi ya sekondari hasa kidato cha tano au cha sita ni vipanga halisi ambao wanapatikana kwa kujua vitu vingi na kuwa serious kwenye masomo

Hii ni tofauti na ngazi ya chuo ni vice versa kidogo ,kwa ngazi ya chuo wale villaza ndio wanaonekana vipanga na wale vipanga wanaonekana vipanga

Hii ni kwa sababu vipanga wengi hawapendi kujihusisha na mambo ya chabo lakini villazaa wengi wanaingia na chabo kwenye mitihani wengine wanaingia mpaka na simu na ku gugo maswali yanayowashinda pia bila kusahau kugerezea kutoka kwa wanafunzi wengine hivyo basi matokeo yakitoka hawa villazaa wanapata alama nzuri kwa kigezo cha kupiga chabo lakini vipanga wanaanguka kwa kuwa wengi wanajiamini saaana na majibi yao na hawapendi mambo ya chabo hivyo matokeo yakitoka wanajikuta wameanguka kwa kuwa villaza wanafanya mtihani kwa kushirikiana lakini kipanga wa ukweli nafanya mtihani yeye kama yeye

Pia villazaa huwa wanahakikisha Coursework inasoma vizuri kwa kuwa wanajua wao hawako vizuri kwenye tests hii ni tofauti na vipanga ambao wao hawabase saana na coursework na wanategemea sana tests hivyo test ikiwa ngumu ndio basi tena

Pia mitihani ya chuo mingi lekchara anasema atakapo toa na mara kwa mara hawezi kutoa beyond na aliposema hivyo basi wale villaza watasoma saana hiyo area kuliko nyingine na mwisho wa siku wanatoka na alama nzuri maana villaza wengi wanasomea pepa sio ujuzi lakini kwa wale vipanga wao huwa hawaridhiki huwa wana penda kwenda extra miles hivyo basi hujikuta wanasoma mambo mengi ambayo hayapo kwenye pepa

Kwa ngazi ya sekondari inabidi usome sana kwa kuwa walimu wanapenda kwenda deep saaana hivyo basi wale vipanga halisi huwa wanapeta saana ila wale villaza wanaumia saana

Hajadisco banaaaa mtu ku disco lazma awe na GPA <2.....unaweza ku supp masomo yote na ukabakia umesupp na wala sio kudisco kinachokulinda ni GPA
haiwezekan mtu awe na sup zote alafu asi disco kwa sababu gpa ya 2.0 ni average ya C so mtu anapo sup yote lazima atakuw chini ya 2.0

haiwezekan mtu awe na sup zote alafu asi disco kwa sababu gpa ya 2.0 ni average ya C so mtu anapo sup yote lazima atakuw chini ya 2.0
Ila inabidi utambue kwamba zile continuous assesment hazikuwekwa buleeee......na Assigment.....halafu ili GPA iweze ku kokotolewa wanazingatia pia hzo Contins assesment na asigmnt....Na zungumza haya nikiwa na ushahidi maana nimemaliza chuo juzi

Pole, ishantokea hii. Niko second year kuingia 3rd nlikua na Sup 5 tena 6 kabisa moja nika appeal ikatoka zikabaki 5 (QM 1& 2, Business Law, Corporate finance na managerial economics ilikua ni balaa vitu hizo kwa kilaza wa namba mimi usiombe.

Weka malengo amua kufaulu so soma sana utapass na kuzitoa zote. Mi nlikaza sana nkachomoa zooote nkaingia 3rd year super clean. Kilichonfanya kufaulu pia ni kuamini kuwa naweza na kilichotokea ni makosa tu na uzembe. Nkakubali makosa nkakubali kujifunza upya kwa umakini. Kaza buti chomoa songa very possible.

Mkuu mimi nina sup 7 za semister 1 na 2... Sina presha... September naenda kuzichomoa zoote....

Ushauri.. Kabla hujafanya sup tambua ni wapi ulikosea na rekebisha haraka sana iwezekanavyo.....

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu mimi nina sup 7 za semister 1 na 2... Sina presha... September naenda kuzichomoa zoote....

Ushauri.. Kabla hujafanya sup tambua ni wapi ulikosea na rekebisha haraka sana iwezekanavyo.....

Sent using Jamii Forums mobile app
inategemea na chuo ulichopo kuna vingiine hapo ume disko..

Back
Top Bottom