Nimepata uzoefu kuzuia wizi wa mtandaoni

Nimepata uzoefu kuzuia wizi wa mtandaoni

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kwanza nitafurahi nikipokea pole baada ya kuibiwa mara 2 kwa njia ya mtandao.Vile vile wanaoibiwa na serikali itafaidika ikinisikiliza namna wizi huo unavyoweza kama si kuzuilika basi kupunguzwa kwa kiasi kikubwa..
Wezi daima watakuwepo isipokuwa kama kuna nia safi ya kuwashughulikia basi huwa wanashindwa kuendelea na uovu wao.
Wizi wa mtandao upo wa kimataifa na upo wa kitaifa.Ule wa kimataifa ukikupata inakuwa ni ngumu zaidi kupata msaada.Huu wa kitaifa tumeambiwa pamoja na kuwepo kwa vikosi vya kipolisi vya kuushughulikia bado wezi hao wanaendelea kuwaibia watu mabilioni ya pesa na hawajaweza kupunguzwa. Hili linashangaza sana kiasi kwamba tunaoibiwa huwa tunapata dhana kuwa wezi hao si wa kawaida.Huwa wanasaidiana na hao hao ambao wanatakiwa wazuie wizi huo.
Kwanza wale wanaopiga simu ili wakuibie huwa wanakuwa na takwimu karibu zote zinazokuhusu wewe.Kinachobaki huwa ni namba yako ya siri tu.Huwa wanakuongoza hatua kwa hatua na kwa kujiamini mpaka unatoa namba yako ya siri ukidhani unazungumza na mtu wa karibu au mhudumu wa shirika la simu.Mtu wa kawaida hawezi kujiamini kufanya hivyo lazima anakuwa ana uzoefu kutoka mashirika ya simu.
Mapendekezo
1.Unapogundua umeibiwa ukipiga simu kwa shirika la simu inatakiwa hatua yoyote wanayochukua iwapo ni kuzuia muamala basi kuwe na mawasiliano ya kimtandao na kitengo cha polisi cha kuzuia wizi wa mtandao kama ilivyo taarifa ya matukio ya moto.Haitoshi wahudumu wa simu kusema ukaripoti polisi.Umuhimu wa polisi kusikia malalamiko na kuona namba ni kuwa watakuwa pengine wameshaona namba hiyo hiyo ikilalalamikiwa kwenye makampuni mengine ya simu muda si mrefu kabla.Hapo wao kimy kimya wamfuate mhusika kwa kutumia GPS ya simu ya mwizi.Wakati mwengine inatia aibu kwani wezi wa mtandao wanabaki hewani zaidi ya siku moja na ukiwapigia wanakutukana vibaya sana.
2.Namba iliyoripotiwa kufanya wizi baada ya dakika chache iwe imezimwa ili mwizi asiendelee kuibia watu kwa siku nzima.Kwa kufanya hivyo mwizi hatopata nafasi ya kuendeleza wizi na pesa inaweza kurudishwa kwa mwenyewe bila kupiga simu kuzidai kwa mwizi katika kipindi cha saa 24.
3.Masuala ya usajili wa laini za simu usifanyike mitaani. Wale wanaopita na spika za matangazo ya kusajili na kurudisha laini wapuuzwe moja kwa moja.Wengi wao wanafanya kazi mbili mbili.Na ukichunguza wana vifaa vya kuchukulia alama za vidole zaidi ya kimoja.Mwananchi usitoe vidole vyako kwa wapita njia.Huwa unawapa nafasi ya kusajili laini nyengine usizozijua kwa jina lako ambazo huzitumia kuibia watu.
4.Mwanachi ukipigiwa simu na mtu anayetaka takwimu kwenye simu akisema anatoka popote basi bora uwe na simu ya kurekodi mazungumzo yenu.Hizi sauti kama zina shaka au ukipata tatizo zipelekwe kwenye ofisi za mashirika ya simu wachunguze iwapo si watu wao wanaofanya kazi hizo baada ya muda wa kazi.
5.Laini iliyolalamikiwa kuiba pesa ambayo watu wa kampuni watakuwa wameiona baada ya kuripotiwa na kufungiwa ndani ya dakika mbili.Mwenye laini hiyo akiwa na hoja kwamba si yeye basi apige simu kampuni kwa simu nyengine yenye wasap hata ya kuazima ili aonekane sura yake bila kuona sura ya mhudumu.Pamoja na sura atakiwe kutaja vitambulisho vyake kama inavyofanyika kawaida.Pamoja na hivyo atoe maelezo kwanini imetokea hivyo.Iwapo hakuhusika arudishiwe pesa hapo hapo bila kuingiza masuala ya polisi.Akishindwa kufanya hivyo baada ya masaa 24 pesa arudishiwe aliyelalamika na namba iliyotumika kuiba iwe imefungwa moja kwa moja.Mara nyingi wezi hawatopiga simu.Itakuwa ni uthibitisho wa mwanzo wa madai ya mlalamikaji kuwa kweli ameibiwa.
Kwa hauta hizo pesa nyingi zitaokolewa na wezi watapungua sana na upande mwengine wateja watafurahia huduma za pesa mtandaoni.Kinyume cha hivyo tutafikiria kurudia enza za ujima.
 
Next time jaribu ku paragraph bandiko lako mkubwa. (Kurahisisha usomaji na kupata flow nzuri ya hoja)

Unless otherwise nice information [emoji106]
 
Sawa mkuu, ila ungeacha aya kati ya kufungu cha habari na kingine ingependeza zaidi.
 
Unaonekana ni mweupe kabisa au ng'ombe adi unaibiw kijinga kiasi hiki ebu kuwa smart
Zamu yako haiko mbali.Hata mimi niliwahi kujigamba kama hivyo. Huyo mwizi alikuja kwa sura tofauti na zote ninazozifahamu.Ni mzoefu na atakuwa hayuko peke yake.Ukipenda usiibiwe na wenzako nao wasiibiwe basi fuata ushauri wangu.
 
Watu wa mikoani utawajua tu, karibu mjini.
Umeibiwa kizembe sana.
 
Kwa ujinga ulionao unashindwa kutambua kama anaesajili laini amesajili laini moja au zaidi ya moja.
 
Uwe unatumia hio namba yako ya nida kutambua namba zilizosajiliwa na kidole chako.
 
Sio nyingi sana.Kilichoniuma ni kuwa nimeibiwa.Nilikusudia nisiingie kwenye historia ya kuibiwa mtandaoni.Ndio hivyo tena.
Mkuu usitoe nywila hata ukiombwa na Waziri mkuu sembuse Meneja wa tawi la Benki.

Hawa wezi primitive ambao wanatuma random messages hao huwa wanawapata Wazee,Washamba,na Low IQ wenzao.
 
Mkuu usitoe nywila hata ukiombwa na Waziri mkuu sembuse Meneja wa tawi la Benki.

Hawa wezi primitive ambao wanatuma random messages hao huwa wanawapata Wazee,Washamba,na Low IQ wenzao
Wale wanaotuma meseji za aina hiyo wala hawawezi kuniibia.Na wale wanaojifanya ni wahudumu wa makampuni ya simu nimeshawatimua mara nyingi sana.Huyu nimekwambia alikuja kwa sura tofauti.Kama hao niliowataja kuwa mstari wa mbele kuzuia wizi huu watachukua uzoefu wangu basi wanaweza kupata dokezo la kuzuia wizi huu.Kuhusu IQ ya kwangu nataraji haiko chini
 
Huyu alitumia nguvu za ziada.Atakuwa ni mwizi aliyekuwa akinifuatilia na muda mfupi kabla ya kunivamia atakuwa alituma wapelelezi wake ajue niko wapi na nafanya nini. Na wewe chukua tahadhari.
Tueleze ulitapeliwa vipi?
 
Jamaa jinga sana linataka kupunguza ajira za watu ambazo hazina athari kwa mtu makini.
Dharau na dhihaka kama hizi ni hatari kwako.Wizi usiudhihaki kuwa ni ajira.
 
Unaonekana ni mweupe kabisa au ng'ombe adi unaibiw kijinga kiasi hiki ebu kuwa smart
Usitukane mamba kabla hujavuka mto mkuu, binafsi sikua nawaelewa wanaotapeliwa mtandaoni mpaka pale yaliponikuta siku moja

Na mpaka sasa najilaumu kwa kuibiwa kizembe, walinilamba 750k hiyo hela mpaka leo inaniuma, laiti ningewakazia kama nnavowakaziaga sikuzote

Najiuliza yule sijui alikua ana dawa gani mpaka kuniingiza chaka kiasi kile.
 
Back
Top Bottom